DC ashauri ngariba wafunzwe ujasiriamali

DC ashauri ngariba wafunzwe ujasiriamali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameyashauri mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayojishughulisha na mapambano dhidi ya ukeketaji kupanua wigo kwa kuanza kutoa elimu juu ya kilimo cha kibiashara na ujasiriamali.

Amesema elimu juu ya kilimo cha kibiashara na ujasiriamali itawasaidia ngariba wachache waliobaki na wananchi kwa jumla kupata shughuli mbadala za kujiingizia kipato cha kukidhi mahitaji yao.

“Serikali inaunga mkono mapambano haya ya kutokomeza ukeketaji na ukatili wa kijinsia, lakini mtafanya vizuri zaidi endapo katika mradi wenu mtatenga muda wa kutoa elimu na kuhamasisha kilimo cha kibiashara na ujasiriamali. Hapa lengo ni wananchi wetu waondokane na umasikini,” amesema.

Amesema halmashauri ya Ikungi imejipanga kuanzisha kilimo cha korosho msimu ujao ambalo ni zao la biashara na litasaidia kutunza mazingira.

Mtaturu alikuwa akizindua mradi wa uhamasishaji masuala ya ukatili wa kijinsia na ukeketaji kwa wanawake na wasichana unaotekelezwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la SMCCT kwa ufadhili wa taasisi ya The Foundation for Civil Society.


Mwananchi
 
Back
Top Bottom