siyoi koroi
Senior Member
- Sep 6, 2016
- 177
- 214
Kilikuwa ni kikao cha ghafla sana kilichoitishwa na Dc wa Arumeru Bw Alexander Mnyeti na hii ni mara tu baada ya kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya meru kushindwa kuendelea baada ya DED Kufunga ukumbi tarehe 20 february 2017. Jioni hiyo hiyo DC Mnyeti Aliitisha kikao kesho yake tarehe 21 kwa njia ya sms kupitia kwa watendaji wa kata kuwa anawahitaji watendaji wote wa kata na vijiji wenyeviti wote wa vijiji na wah madiwani wote. katika kikao hicho alitangaza kuwa amepiga marufuku vikao vyote vya baraza la madiwani wa halmashauri ya meru. Cha kushangaza ni kuwa yeye Dc siyo sehemu ya baraza la madiwani na wala yeye hana mamalaka ya kusimamisha kikao chochote cha baraza la madiwani. Kisheria baraza la madiwani linaongozwa na kanuni na Dc wakati anatangaza kusimamisha vikao hakutaja kanuni inayompa mamlaka hayo.
Sasa ni dhahiri kuwa hata vikao vinavyoshindwa kuendelea halmashauri ya meru ni kwa amri ya DC Mnyeti. katika kikao hicho alitumia muda mwingi kuwashambulia madiwani na kuwabeza . Tena aliwaambia wenyeviti wa vijiji kuwa kuna haja na wenyewe wasusie kuhudhuria vikao vya WDC kwani madiwani wengi hawapendi kuhudhuria vikao vyake