elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
MKUU wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja, Rajab Ali Rajab amepiga marufuku masheha kufanya suluhu ya kuwapatanisha watu wanaobainika kufanya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kuwaozesha.
Rajab amesema imebainika kwamba masheha wamekuwa wakisuluhisha matukio ya kuozeshana bila kujali kwamba vitendo hivyo ni vya udhalilishaji wa kijinsia, ikiwamo ubakaji na wahusika wanatakiwa wafikishwe katika mkondo wa sheria.
Alisema makosa hayo yanatakiwa kutolewa taarifa Polisi na si suluhu.
“Zipo taarifa ya baadhi ya masheha wamekuwa wakileta suluhu na kuozesha wananchi wanaobainika kufanya vitendo vya udhalilishaji ikiwemo ubakaji...masheha wa aina hiyo tutawachukulia hatua za kinidhamu,” alisema.
Mapema Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Wilaya ya Kaskazini "B", Salma Shaib alisema kongamano hilo limetayarishwa kwa ajili ya masheha, madiwani, walimu wa wakuu, viongozi wa kisiasa na dini limefanyika kutokana na muongozo wa Jumuiya ya Wazazi Ngazi ya Taifa.
Shaib amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia jumuiya hiyo kiliamua kuandaa makongamano hayo yatakayotoa fursa kwa kila mwanajamii kuchangia mbinu zitakazosaidia kurejesha maadili ya Mtanzania yanayoonekana kutawaliwa zaidi na utamaduni wa kimagharibi.
Alisema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa imebainika kwamba maadili yameshuka na hicho ndiyo chanzo kikubwa cha kuwepo kwa wingi wa talaka pamoja na ndoa kuvunjika ambapo watoto hukosa matunzo ya wazazi wawili.
“Tumefanya kongamano hili kwa ajili ya kutathmini hali halisi ya kuporomoka kwa maadili katika jamii yetu na hivyo kuwepo kwa wingi wa talaka na ndoa kushindwa kudumu,” amesema.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliitaka Ofisi ya Mufti Zanzibar kuanzisha mafunzo kwa watu wanaotarajiwa kuoana ili kuweza kuyafahamu majukumu yao ya msingi kabla ya ndoa yenyewe.
“Moja ya jambo ambalo linaweza kudhibiti talaka ni kwa wanandoa kupewa mafunzo ambayo yatawawezesha kufahamu majukumu yao ya msingi ikiwemo kujenga tabia ya uvumilivu,” amesema.