Dc aliyewapiga viboko walimu, kikwete anasita kumpa barua ya kumvua madaraka

mwenyewe

Member
Apr 18, 2008
37
3
Kutokana na info zilizonifikia, rais Jakaya Kikwete ameshangazwa na support aliyopiwa DC Albert Mnali kutoka kwa sehemu kubwa ya jamii kwa kitendo cha kuwatandika mboko walimu wazembe wilayani mwake.

Mpaka leo hii, Rais Kikwete anakua anasita kumkabidhi barua rasmi ya kumvua madaraka mtumishi huyo wa umma. Inasemekana bado anajadili uamuzi wake wa kumvua madaraka kama ulikua wa busara au alikurupuka.

Shime bwana Mnali wengine 10 kama wewe, naamini tungekua waliopo nchi kama Malaysia, Singapore, Thailand, India hata China.
 
Inamaana Rais hajiamini kama raisi ila kwa wezi wa kuku na mabata,ndio maana yake.
 
Naona kwa kua tunaelekea kwenye election year, sasa rais anakua very careful na maamuzi yake......... anaweza akaoneka ni kikwazo kwa viongozi wenye uchungu na nchi na wasiotaka ujinga, uzembe na ubadhirifu kama ule wa wizara zake na mawaziri wake.
 
uamuzi wa busara anaopaswa kufanya ni kumpandisha cheo awe mkuu wa mkoa ili atandike ma dc manake matatizo mengi sana ya nchi yamejikita wilayani huko kwa hao miungu watu!
 
Naona kwa kua tunaelekea kwenye election year, sasa rais anakua very careful na maamuzi yake......... anaweza akaoneka ni kikwazo kwa viongozi wenye uchungu na nchi na wasiotaka ujinga, uzembe na ubadhirifu kama ule wa wizara zake na mawaziri wake.

Tatizo la wanasiasa kama JK all the time maamuzi yake yanategemea upepo wa kisiasa unavuma kuelekea wapi na sio kutoa maamuzi kulingana na leadership and professional ethics. Kusupport ujinga kwa sababu ya kuogopa wapigakura kukumwaga kwa maamuzi sahihi uliyo yatoa is rabish. A leader should be decisive and stand on his decision. Should be able to say yes, is me, I did this and that because of 1, 2, 3, etc. No single fool will not vote for him if he was right.
 
Kutokana na info zilizonifikia, rais Jakaya Kikwete ameshangazwa na support aliyopiwa DC Albert Mnali kutoka kwa sehemu kubwa ya jamii kwa kitendo cha kuwatandika mboko walimu wazembe wilayani mwake.

Mpaka leo hii, Rais Kikwete anakua anasita kumkabidhi barua rasmi ya kumvua madaraka mtumishi huyo wa umma. Inasemekana bado anajadili uamuzi wake wa kumvua madaraka kama ulikua wa busara au alikurupuka.

Shime bwana Mnali wengine 10 kama wewe, naamini tungekua waliopo nchi kama Malaysia, Singapore, Thailand, India hata China.

Yale yale aliyoyasema Kitine ya nchi kuendeshwa kienyeji!!! Anatangaza hadharani kwamba kamfukuza kazi halafu kuona Mnali anasupport kubwa ya Watanzania anaanza kugwaya!!!! Sasa kama huwa anaangalia support kubwa ya jamii kinamshinda nini kuwashughulikia mafisadi, kumchunguza Mkapa na kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa dhahabu!? Maana vyote hivi vinasupport kubwa toka kwa Watanzania walio wengi. Uongozi siyo lelemama!!!
 
Naona kwa kua tunaelekea kwenye election year, sasa rais anakua very careful na maamuzi yake......... anaweza akaoneka ni kikwazo kwa viongozi wenye uchungu na nchi na wasiotaka ujinga, uzembe na ubadhirifu kama ule wa wizara zake na mawaziri wake.

Hakuna kitu kama hiki, Kikwete hajakosea na hajutii uamuzi aliofanya!!! wanaosupport wendawazimu wa namna hii aliofanya mnali ni wachache sana; wala kura zao hazina effect yoyote i kwenye uchaguzi kilinganishwa na mass ya walimu wote ambao ndio msingi wa ushindi wa ccm kwenye chaguzi zote!!

Kama mnali hawezi kukumbuka jambo dogo tu la kujua muundo halali wa kushughulikia masuala ya nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa serikali, ni wapi anaaminiwa kusimamia mambo makubwa na nyeti kwa taifa??? alichofanya kinaonyesha dalili zote za wendawazimu!!!

Wanaomtetea watuambie ni lini mwendawazimu akaaminiwa kufanya kazi zenye maslahi kwa umma??
 
Maslahi yepi hayo ya umma??

Hebu fafanua! Sii lazima walimu wachapwe fimbo..ila ktk large picture we need to overhauil mfumo wa utawala wa sheria!

Nachosema mafisadi, wezi wazembe wachapwe fimbo tena mbele ya wake zao..iwe fundisho!

Mambo gani makubwa hayo kwa taifa ktk kulinda uzembe, ifisadi na ubadhirifu?

Kwani tz ndo nchi ya kwanza kuwashughulikia watu kama hawa?

Ndo maana Hu alipokuja Tz watu walisema aombwe ile sheria yao ya kuwashughulia wazembe itumike tu kwa mda Tz!
 
Hivi enzi za Mwalimu Nyerere ni waziri gani alikula henzerani nakurudishwa kwao sijui Tabora vile? na baada ya hapo mawaziri wote walikuwa na adabu na Ikulu, nasikia enzi hizo mtu alikuwa akiitwa ikulu basi hupitia nyumbani kuongeza kaptura ndani ya suruali na kuwaambia anzeni kufungasha mambo si mazuri kabisa!
 
kama ni hivyo rais asiyekuwa na uhakika na maamuzi yake hafai
 
CCM imepoteza dira ,haina haja ya kumpa kichwa DC wala Kikwete wote hawafai ,Nakumbuka Kikwete aliruka na kusema kazi hiyo ya kufukuza inawahusu wakuu wa Mikoa au Waziri husika ,naikumbukia ile habari iliyotoka Ikulu ambayo ilikuwa imejifunga funga.

Kwa ufupi CCM imepoteza dira ya kuongoza Nchi ,na kila tunapopiga hatua kunazuka mepya ,kila mmoja ni mbabe. Ndipo walipotufikishia uongozi wa Nchi hii.
 
huyu DC, alitakiwa kuadhibiwa alipo tongoza/au kumnyanyasa kijinsia Mke wa Mtu kule Mwanza, kwa hili la Kagera kwa hali ilivyo Tz, unaweza ukampongeza kidogo, kwani watu/punda haendi sharti kiboko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom