Dawa za milioni 294 zilizokamatwa zakabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
BARAZA la Famasia Tanzania limekabidhi dawa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda zenye thamani ya Sh. milioni 294 zilizokamatwa katika operesheni safisha maduka ya dawa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea dawa kutoka kwa Msajili wa baraza la Famansia , Elizabeth Shakalaghe ambazo walizikamata katika operesheni safisha maduka ya dawa leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymont Mushi akipokea baadhi ya maboksi ya dawa jijini Dar es Salaam leo.

DSC_0827.jpg


Akizungumza wakati wa kukabidhi dawa hizo Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shakalaghe amesema operesheni hiyo iliyofanyika katika Mikoa tisa na walifanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 336 na kati ya dawa hizo dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 11 hazifai kwa matumizi ya binadamu.Alisema dawa hizo zitasambazwa katika hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam na zimehakikiwa.

Amesema katika Mkoa wa Dar es Salaam majalada 10 yamefunguliwa mahakamani kwa wale waliokamatwa na dawa za serikali ambayo kwa sasa yapo katika hatua za upelelezi.

"Bado kumekuwa na ongezeko la maduka ya dawa ambayo yanaanzishwa kinyume na sheria na taratibu hususani katika Mkoa huu na tumebaini kwamba maduka yaliyofugwa wakati wa operesheni yanafunguliwa wakati wa usiku na kuendelea kutoa huduma za dawa .amesema.

Elizabeth amesema lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kuvunja sheria ya famasi katika uendeshaji na utoaji wa huduma za dawa nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa dawa hizo, Mkuu wa Mkoa huu,Paul Makonda alisema wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali wanatakiwa kufunga maduka hayo mara moja au kuzirudisha walikonunua huku wengine wakifanya huduma nyingine ambayo ni tofauti na leseni walizoomba.

Makonda amevitaka vyombo vya dola na watendaji wa ngazi ya mkoa , manispaa, kata na mitaa kuhakikisha wanayafunga na kuyaondoa maduka yote ambayo hayana vibali na yanayoendeshwa kinyume na sheria ya famansi nchini.

Aidha amevitaka vyombo vya dola kufanya operesheni nyakati za usiku ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki kwa wale watakaokaidi maagizo ya awali na kufanya biashara wakati wa usiku kwa kizingizio serikali imelala wakati huo.
 
Kwa hiyo dawa zinataifishwa kwenye maduka binafsi ya dawa halafu zinasambazwa kwenye hospiali za serikali?, hii haijakaa vizuri
 
Kwa ili la dawa inabidi tutafakari sana,kiutaratibu dawa kama hizo inabidi ziwe condemned kwani ziliisha toka kwenye mfumo rasmi na huko zilikokutwa hapakuwa na quarantee ya utunzaji etc,ni sawa unakamata nyama kwenye mabucha au mama ntilie and then unagawia hospitali,haiko vizuri hii
 
Kwa hiyo dawa zinataifishwa kwenye maduka binafsi ya dawa halafu zinasambazwa kwenye hospiali za serikali?, hii haijakaa vizuri
Mwenzangu yaani ni pure dhuluma nakwambia labda sijui sheria inasemaje poor us kweli namba lazima isomeke kha si kwa mwendo huu .
 
Huu ubinafsi wa mkoa wa Darsalam umepitiliza. Dawa zimetaifishwa kutoka mikoa mingi halafu zote zigawiwe dar peke yake,ni umimi ulopitiliza.
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Dawa zimekamatwa toka mikoa 6 lakini dawa wamegawiwa watu wa Dar es salaam tu! Haipendezi kuna mikoa masikini kama Lindi, kagera, pwani, dodoma...wangepewa hizo dawa
Umesahau Mwanza na Kagera mkuu,nayo ni mikoa mskini kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.
 
kuna uonevu nabupendeleo hapo jambo ambalo sio sawa kabisa!!! kuna mikoa maskini kiasi hata kumudu dawa shida kwa nn wasigawiwe??? ukizingatia zimekamatwa mikoa mbali mbali
 
kila mkoa ungepewa dawa zilizokamatwa mkoan kwake...sasa kumpa makonda ndo ina maana gan sasa au ndo kufanya kazi ili watu waoekane wanafanya..........
 
Mimi nilivyoelewa ni kwamba zoezi lilifanyika katika mikoa tisa nchini ili kubaini maduka yenye vibali lakini yakawa yanauza madawa yenye nembo za MSD na pia maduka yanayouza dawa (zenye nembo au zisizo na nembo za MSD) wakati hayana vibali vya kuuza dawa. Na thamani ya madawa yote yaliyokamatwa kwa mikoa hiyo tisa ni milioni 336.

Lakini kwa upande wa mkoa wa Dar es Salaam pekee yake wakaguzi ambao ni Baraza la Famasia Tanzania waliweza kukamata dawa zenye thamani ya milioni 294 ambazo ndizo zilizokabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Hizo dawa za Dar zenye thamani ya milioni 294 ni sehemu ya dawa zenye thamani ya milioni 336 zilizokamatwa kwa mikoa yote tisa.
 
Dawa zimekamatwa toka mikoa 6 lakini dawa wamegawiwa watu wa Dar es salaam tu! Haipendezi kuna mikoa masikini kama Lindi, kagera, pwani, dodoma...wangepewa hizo dawa
labda sababu dar ndo tv zipo fasta, huko sumbawanga utamtoa wapi mpiga picha?
 
Back
Top Bottom