Dawa ya maradhi ya moyo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,861
30,279
Kila maradhi yana pozo.. na dawa ziko za aina tofauti tu kuna dawa za miti shamba kuna dawa za chemical yaani tunazopatiwa hospitali na kuna dawa zinatokana na matunda alitojaaliwa Allah S.W. Mimi binafsi napenda kujitibu kwa dawa za matunda kwani hamna atrificial ndani yake. Inshallah nitaandika juu ya matunda mawili matatu ambayo husaidia kuondoa maradhi ya moyo.

Apples: Matunda haya yana wingi wa potassium na phosphurus na kiwango kidogo cha sodium, miaka ya nyuma walikuwa wakitumia tunda hili pamoja na asali kwa ajili ya matatizo ya moyo, kuwa na wingi wa potassium katika mwili husaidia kuepukana na maradhi ya moyo kwahivo mtu mwenye maradhi ya moyo ni vizuri kula matunda haya asubuhi na jioni na uzuri zaidi akila pamoja na asali.

Grapes(zabibu): Zabibu au juice ya zabibu husaidia sana katika maumivu ya moyo yaani cardiac pain. Maradhi ya moyo yanaweza kuondoka kwa mgonjwa akitumia zabibu kwa muda.

Orange(machungwa): Juice ya machungwa ukichanganya na asali husaidia kuondoa maumivu ya moyo kama coronary ischaemia.

Garlic(kitunguu saum):Kitunguu saum kinalinda upatikanaji wa heart attack, husaidia kuondoa mafuta katika mishipa ya moyo pia husaidia artiries kupeleka damu upesi (artiries huwa nzito na hii hupelekea kupatikana kwa high blood perssure na heart attack) Mgonjwa wa moyo akitumia garlic kwa muda maradhi hayo humuondokea atumie kila siku asubuhi chembe 2 na usiku chembe 2.

Onion(kitunguu maji): Onion kazi yake ni kama ya kitunguu saum .

Wheat(ngano): Majani ya ngano husaidia moyo kufanya kazi yake pia husaidia na mapafu, pia capillary hufanya kazi uzuri zaidi na kuongeza damu.

Honey (Asali):Asali ni dawa bora kulikoni zote nilizozitaja hapo juu. Mwenye maradhi ya moyo anywe kila siku glasi ya maji achanganye na asali pamoja na maji ya ndimu na pia anywe kama ataamka usiku na aendelee kufanya hivi kadri awezavyo na Inshallah maradhi hayo yatamuondoka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom