fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,598
- 4,472
Habari wakuu, niende kwenye mada husika.
Imepita week sasa tangu Waziri wa mambo ya nje kuileta nchini Dawa inayosadikika kutibu Covid-19 toka Madagascar na kisha kutangaza kuifanyia test kwanza kabla ya kuitumia.
Sisi kama wananchi wa kawaida, tuliipokea tofauti maneno ya Mh. Rais JPM alivyotutangazia kwenda kuifata dawa hyo madagascar ije kutumika, kiasi watu wengi walipost jambo hilo alilolisema Rais na kisha kusubiri kwa hamu kuletwa hiyo dawa.
Dawa hii kweli iliingizwa kama alovyoagiza Rais japo sasa ikawa tofauti kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje Prof.Kabudi na hakika maneno yake yalikua kama msumari ndan ya moyo kwa watu wengi, ila subra huvuta kheri watu wakaamua kusubiri huku wakitegemea matokeo yake kutoka kwa haraka ukizingatia imefanyiwa majaribio Madagascar na hawakuonyesha hata lepe la wasiwasi pale walipo ikabizi kwa Nchi zilizohitaji.
Tunajua NIMR wanafanya kazi kubwa wakishirikiana na wataalamu wengine ktk kuithibitisha hyo dawa,lakini uharaka wahitajika zaid kama walivyofanikiwa kuipitisha ile dawa yao waliyoitengeneza kwa mchanganyik wa vitu mbalimbali.
Ni wazi kwa sasa watu wengi wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi mkubwa kiasi hata kushindwa kupata usingizi kwa hofu ya corona huku wakishindwa kung'amua kama wameambukizwa ama laa. Kumbuka Watanzania wengi wanaishi na magonjwa mbali mbali hasa ya vifua n.k na hii Covid ina dalili nyingi mfanano wake, kiasi hata wengi wakienda hospital na kuambiwa hawaumwi basi huendelea kuamini vipimo ndo havijaonyesha ila ye ana hilo gonjwa. Kupatikana kwa hyo dawa kuta ondoa yote haya. Na kama haionyeshi kutibu basi wafahamishwe pia.
Asante