Dawa ya kuzuia kutapika kwa mtoto

Dawa ya kuzuia kutapika kwa mtoto

Kapuku83

Senior Member
Joined
Sep 8, 2012
Posts
146
Reaction score
35
Wadau habari,

Nakuja jukwaani hapa kuomba msaada wenu,nina mtoto mwenye mwaka na nusu, alikua anasumbuliwa na kutapika, kuharisha na homa toka wiki iliyopita, tulimpeleka hospital na akapata tiba kuharisha na homa vikakata, tatizo kubwa ni kwamba bado tatizo la kutapika linamsumbua sana, tulimrudisha hospital wakampatia dawa inaitwa PHENAGAN (nimesahihishwa) lakini kwa kweli bado haijamsaidia kitu, kwani bado anatapika, mfano leo ametapika mara nne na ameishiwa nguvu kabisa kwa maana ya kulegea mwili kabisa!

Wadau naombeni msaada wenu wa kiushauri!

Asanteni
 
Mpeleka mtoto hospitali ndugu yangu,ikiwezekana hospitali nzuri. Kama ataendelea kutapika anapoteza maji mwilini. Ukiona mtoto anatapika inawezekana tatizo bado lipo mwilini na hivyo anahitaji uchunguzi na matibabu zaidi au labda ni side effect ya dawa alizotumia.

Sio busara kukimbilia kumpa mtoto dawa ya kuzuia kutapika kabla kwanza huja-rule out sababu ya kutapika kwake na kumtibu inavyofaa. Sina hakika uliporudi hospitali walikuambia sababu ya mtoto kutapika, ila nadhani walitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo. Pamoja na hivyo inawezekana kweli mtoto amelegea kwa sababu ya hiyo phenagan aliyotumia, lakini inawezeka pengine labda mtoto bado anasubuliwa na ugonjwa. So, to be in the safe side,you better bring back you child to hospital.
 
Mpeleka mtoto hospitali ndugu yangu,ikiwezekana hospitali nzuri.Kama ataendelea kutapika anapoteza maji mwilini.Ukiona mtoto anatapika inawezekana tatizo bado lipo mwilini na hivyo anahitaji uchunguzi na matibabu zaidi au labda ni side effect ya dawa alizotumia.

Sio busara kukimbilia kumpa mtoto dawa ya kuzuia kutapika kabla kwanza huja-rule out sababu ya kutapika kwake na kumtibu inavyofaa.Sina hakika uliporudi hospitali walikuambia sababu ya mtoto kutapika,ila nadhani walitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo.Pamoja na hivyo inawezekana kweli mtoto amelegea kwa sababu ya hiyo phenagan aliyotumia,lakini inawezeka pengine labda mtoto bado anasubuliwa na ugonjwa.So,to be in the safe side,you better bring back you child to hospital.



Asante sana mkuu Mrimi kwa ushauri wako,nitauzangatia sana,na nimemrudisha mtoto hsptl,wamempa drip na amegundulika ana malaria,hata hivyo natarajia kumpeleka kwa madaktari bingwa wa watoto siku hizi mbili tatu ili kubaini tatizo zaidi!asante sana ndugu yangu!
 
Habari zenu..

Nina mtoto wa miezi 10 ..tangu jana naona anatapika na kuharisha ila hachemki na ana uchangamfu tu..ameanza kuota meno..kuna jino la chini ndo linaota.

Hii hali ya kutapika ina sababishwa na nini jamani na tiba yake ikoje nisaidieni.

Nina mpango asubuhi nimuwahishe hospital
 
Habari zenu..

Nina mtoto wa miezi 10 ..tangu jana naona anatapika na kuharisha ila hachemki na ana uchangamfu tu..ameanza kuota meno..kuna jino la chini ndo linaota.

Hii hali ya kutapika ina sababishwa na nini jamani na tiba yake ikoje nisaidieni.

Nina mpango asubuhi nimuwahishe hospital
Umempeleka mtoto hospitali?vipi hali yake?
 
Back
Top Bottom