Dawa ya kukatika kwa umeme,TANESCO ibinafsishwe

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,490
96,054
Ndugu wana jamvi tumeshuhudia umeme ukiwa unakatika katika kila uchao na kupelekea baadhi ya watanzania wenzetu kupoteza mali zao kwa kuungua baada ya umeme kurudi kwa nguvu na wafanya biashara wengine kupata hasara kwa bidhaa zao kuoza kutokana na umeme usiokuwa na uhakika.

Ni kwanini serikali inazidi kulikumbati TANESCO?kwanini wasibinafsishe kama mashirika mengine?
 
Licha ya Changamoto zote walizopitia Tanesco sasahivi imeanza kurudi Katika ubora tuliokuwa tukiutaka tena Kwa speed sioni haja ya shirika kubinafsishwa maana ndio tutaharibu kabisa kama tulivyowahi kubinafsisha shirika la reli Kwa wahindi hakuna chochote walichofanya zaidi ya kulifilisi shirika la reli mpaka ikafka kpndi miundombinu ya reli zetu ikaanza kuuzwa kama chuma chakavu

Kwa upande wa tanesco sasa hivi ukiangalia shirika limeanza Kuinuka Kwa kasi ya Hali ya juu.

Ni ndani ya kipindi kifupi tu cha Muda usiozidi miaka minne wamepandisha namba ya nyumba(wateja) waliounganishiwa umeme kutoka laki 6 waliokwepo hapo awali mpaka milioni3 Mwaka uliopita(ongezeko la zaidi ya asilimia 400 ndani ya kipindi kifupi cha miaka isiyozidi mnne)

Kwa upande wa uzalishaji ndani ya kipindi kifupi tu wameongeza megawat za umeme kutoka 400 mpaka 1500megawat zilizoungwa kwenye gridi ya taifa mpaka hivi sasa ukiachana na zile 76 zinazozalishwa Katika vituo vya nje ya gridi kama nyumba ya mungu,mtwara,kigoma na kwingineko. Ongezeko hili Ni ongezeko lisilo la asilimia 400 ongezeko ambalo si la kawaida kabisa.

Tukija sekta ya usambazaji umeme pia, mbali na Changamoto zote Tanesco wanazokumbana nazo za kuhujumiwa na wananchi wasiokuwa na nia njema Kwa kuiba miundombinu ya umeme kama nyaya,mafuta ya transfoma,nguo pamoja na wateja wasio waaminifu wanaoibia shirika umeme Kila siku,pamoja na shirika kuweka kwenye mufilishi Kwa kipindi kirefu utawala wa mkapa (maana yake Ni kwamba hawakuruhusiwa kufanya shughuli yoyote ya kujiendeleza Ama kuboresha miundombinu yake) lakini bado Kwa kipindi kifupi wameweza kurepea na kuboresha huduma zao mpaka sasa angalau usiku tunaonana.

Aidha kukatika Kwa umeme kunakokea mara nyingi Ni Kwa vipindi vifupi ambavyo vimetengwa na tanesco kwaajili ya marekebisho ya miundombinu ya usambazaji umeme ambayo mingi Ni ya Muda mrefu na imechakaa kutokana na shirika kuwekwa Katika mufilisi kama nilivyoeleza hapo awali na mara zote wakikata umeme Kwa matemgenezo maalumu wamekuwa wakitoa taarifa mapema kwanza.

TANESCO KAMA NI KAZI INAFANYIKA YA NGUVU BINAFSI NAIONA BAADA YA KUWAFATILIA VZURI.
 
Ndugu wana jamvi tumeshuhudia umeme ukiwa unakatika katika kila uchao na kupelekea baadhi ya watanzania wenzetu kupoteza mali zao kwa kuungua baada ya umeme kurudi kwa nguvu na wafanya biashara wengine kupata hasara kwa bidhaa zao kuoza kutokana na umeme usiokuwa na uhakika,ni kwanini serikali inazidi kulikumbati tanesco?kwanini wasibinafsishe kama mashirika mengine?
Na walivyo bobea kwa uongo basi, kuanzia mkurugenzi mkuu mpaka Customer care station zao na kinara ni kituo kidogo cha MBEZI TANGI BOVU umeme ukikatika na wao simu zao wanazima wakipatikana kila ukipiga anaye pokea ana sababu yake tofauti.
 
HALI YA UZALISHAJI UMEME NCHINI
Hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbali mbali tunazokabiliana nazo kwa sasa. Kuanzia taerehe 17 Septemba tulipoanza kutumia gesi inayotoka Mtwara tumeweza kuongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi kutoka Megawati 260 zilizokuwepo kabla hadi Megawati 560 ikiwa ni ongezeko la jumla ya Megawati 300 au asilimia 115 ya umeme wa gesi uliokuwa unazalishwa. Hii imechangia sana kuboresha hali ya umeme tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Tunategemea kuongeza umeme wa Megawati 130 zaidi kutokana na vyanzo vya Gesi kati ya sasa na mwishoni mwa mwezi Januari 2016. Hii itafanya jumla ya umeme wote unaotokana na gesi kufikia Megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Haya ni mapinduzi makubwa kwani kwa miaka mingi vyanzo vya maji ndivyo vimekuwa vikichangia zaidi ya asilimia 70 ya umeme nchini na hivyo kusababisha athari za mara kwa mara kila unapotokea ukame.
Pamoja na hayo yaliyokwishafanyika, Mkandarasi wa mradi wa pili wa Kinyerezi (KII) wa Megawati 240 anatarajia kuanza kazi wakati wo wote kuanzia sasa baada ya kuwa amekwishalipwa sehemu ya fedha za awali za kuanza kazi hiyo.

2. MIUNDOMBINU YA TANESCO
Miongoni mwa kero kubwa inayolalamikiwa sana na wateja wetu ni kukatika umeme kunakosababishwa na uchakavu wa miundombinu. Ukweli ni kwamba baadhi ya miundombinu tuliyo nayo ni ya siku nyingi wakati matumizi ya umeme
yameendelea kuongezeka kwa kasi sana. Kwa mfano nyingi ya Substations katika jiji la Dar es Salaam zimejengwa katika miaka ya 80 na 90. Wakati huo wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa chini ya milioni 3. Sasa hivi wakazi wa jiji ni zaidi ya milioni 5 na hivyo miundombinu iliyopo inaelemewa sana.
Jitihada za kurekebisha hali hii zilikwishaanza ambapo sasa kuna miradi mikubwa inaendelea katika jiji la Dar es Salaam na itakapokamilika itasaidia sana kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme. Kwa kiasi fulani kukatika huko kwa umeme hasa katika jiji la Dar es Salaam kunatokana pia na utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi inayotekelezwa ni pamoja na ule unaojengwa kusini mwa Dar es Salaam kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambao utaboresha umeme maeneo ya Kigamboni, Kurasini, Mbagala, Mkuranga, Kisarawe, Gongolamboto, Ukonga, Kitunda, Vingunguti na Tabata
Mradi mwingine ni unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan ambao utasaidia kuondoa matatizo yaliyo katika maeneo ya Muhimbili na Upanga, Mwananyamala na Kinondoni, Oysterbay na Masaki, Jangwani Beach, Bahari Beach na Mbezi Beach.
Mradi mwingine ni ule unaotekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ambao unaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Shinyanga, na Geita.
Mradi mwingine ni ule unaofadhiliwa na Serikali ya Finland ambao utasaidia sana kuimarisha umeme kati kati ya jiji la Dar es Salaam na kusaidia kuimarisha umeme katika eneo lenye majengo mengi marefu la Samora, Azikiwe, Kariakoo na Sea view.
Sambamba na miradi hiyo inayotekelezwa Dar es Salaam, mradi mkubwa wa kupeleka umeme wa 400KV kutoka Iringa kupitia Mtera, Dodoma, Singida hadi Shinyanga uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika na hivyo kutuhakikishia umeme wa uhakika katika kanda ya ziwa hasa jiji la Mwanza.
Kazi ya kuunga Songea na Gridi ya Taifa kutokea Makambako kwa 220KV inaendelea na Makandarasi wako kazini.
Kazi za kuunga Tanzania na Kenya kwa umeme wa 400KV inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani zabuni za kuwapata Makandarasi ziko katika hatua za mwisho. Ujenzi unategemewa kuanza mwakani.
Kazi nyingine ambazo hazijaanza lakini zitaanza hivi karibuni ni pamoja na Dar es Salaam – Somanga (400KV), Bulyankhulu – Geita – Nyakanazi – Rusumo (220KV)
Miradi hii ya kuimarisha miundombinu ikikamilika itasaidia kulipunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme kutokana na mfumo wa Usambazaji.
Nawaomba wateja wetu, wakati kazi hii kubwa inapoendelea, wawe na subira na uvumilivu kwa usumbufu wa hapa na pale utakaokuwa unatokea. Hata hivyo TANESCO itajitahidi kurekebisha kasoro zinazoweza kurekebishwa katika miundombinu ya sasa ili kupunguza usumbufu huo wakati marekebisho makubwa yakiendelea.
 
Hapana simu huwa azizimwi, sambamba na hilo tanesco walitoa namba za simu za mameneja wa Kanda na Mikoa iwapo hujahudumiwa vizuri na customer care, unawasiliana nao moja kwa moja.
 
Sijui una pinga kama mfanyakazi au vipi ila kwa nafasi yoyote uliyo nayo iwe kwenye shirika au vipi ukweli ndio huo na unaweza hata kufanya utafiti kwani kuzimika umeme mbezi beach bila ya taarifa ni mambo ya kawaida sana mara ya mwisho ni jana tu usiku wa manane na kwenye Tv na vyombo vya habari Viongozi wana jinadi kwa uongo na mbwembwe kuwa sasa wamedhibiti matatizo, hebu acheni kucheza na uvumilivu na akili za watu.
 
Na walivyo bobea kwa uongo basi, kuanzia mkurugenzi mkuu mpaka Customer care station zao na kinara ni kituo kidogo cha MBEZI TANGI BOVU umeme ukikatika na wao simu zao wanazima wakipatikana kila ukipiga anaye pokea ana sababu yake tofauti.
Mkuu hili tatizon tumelivumilia vya kutosha na hatuoni nini sababub ya serikali kuendelea kuwabeba tanesco
 
TANESCO inapata faida kwa wateja wa kubwa
wenye viwanda na biashara kubwa asilimia 75

wananchi wanachangia asilimia 25 tu..

mtu binafsi unafikiri atajali sana hao wananchi wanaoleta faida asilimia 25?
mtu binafsi atajali wanaomletea faida tu ya kutosha
kuna mikoa na vijiji umeme watausikia kwa redio tu

Ili umeme uwe ni huduma inayopatikana kwa kila mtu
serikali lazima ibebe dhamana
 
Hapana simu huwa azizimwi, sambamba na hilo tanesco walitoa namba za simu za mameneja wa Kanda na Mikoa iwapo hujahudumiwa vizuri na customer care, unawasiliana nao moja kwa moja.
Mkuu hali halisi ya upatikanaji wa umeme ni mbaya sana( ya chini ) sana siyo tu kwa dsm tu bali tanzania mzima,ukiondoa mkoa wa kagera kidogo ambao wanapata umeme toka nchini uganda,tuwache kudanganywe na takwimu za kwenye makaratasi
 
Mkuu hili tatizon tumelivumilia vya kutosha na hatuoni nini sababub ya serikali kuendelea kuwabeba tanesco
Wana lelewa sana hawa wakati ni jipu la kupasua kwa sululu ukiwasikiliza ni ulaghai mtupu na kutumia fedha nyingi kwenye vyombo vya habari kujinadi.
 
HALI YA UZALISHAJI UMEME NCHINI
Hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbali mbali tunazokabiliana nazo kwa sasa. Kuanzia taerehe 17 Septemba tulipoanza kutumia gesi inayotoka Mtwara tumeweza kuongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi kutoka Megawati 260 zilizokuwepo kabla hadi Megawati 560 ikiwa ni ongezeko la jumla ya Megawati 300 au asilimia 115 ya umeme wa gesi uliokuwa unazalishwa. Hii imechangia sana kuboresha hali ya umeme tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Tunategemea kuongeza umeme wa Megawati 130 zaidi kutokana na vyanzo vya Gesi kati ya sasa na mwishoni mwa mwezi Januari 2016. Hii itafanya jumla ya umeme wote unaotokana na gesi kufikia Megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Haya ni mapinduzi makubwa kwani kwa miaka mingi vyanzo vya maji ndivyo vimekuwa vikichangia zaidi ya asilimia 70 ya umeme nchini na hivyo kusababisha athari za mara kwa mara kila unapotokea ukame.
Pamoja na hayo yaliyokwishafanyika, Mkandarasi wa mradi wa pili wa Kinyerezi (KII) wa Megawati 240 anatarajia kuanza kazi wakati wo wote kuanzia sasa baada ya kuwa amekwishalipwa sehemu ya fedha za awali za kuanza kazi hiyo.

2. MIUNDOMBINU YA TANESCO
Miongoni mwa kero kubwa inayolalamikiwa sana na wateja wetu ni kukatika umeme kunakosababishwa na uchakavu wa miundombinu. Ukweli ni kwamba baadhi ya miundombinu tuliyo nayo ni ya siku nyingi wakati matumizi ya umeme
yameendelea kuongezeka kwa kasi sana. Kwa mfano nyingi ya Substations katika jiji la Dar es Salaam zimejengwa katika miaka ya 80 na 90. Wakati huo wakazi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa chini ya milioni 3. Sasa hivi wakazi wa jiji ni zaidi ya milioni 5 na hivyo miundombinu iliyopo inaelemewa sana.
Jitihada za kurekebisha hali hii zilikwishaanza ambapo sasa kuna miradi mikubwa inaendelea katika jiji la Dar es Salaam na itakapokamilika itasaidia sana kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme. Kwa kiasi fulani kukatika huko kwa umeme hasa katika jiji la Dar es Salaam kunatokana pia na utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi inayotekelezwa ni pamoja na ule unaojengwa kusini mwa Dar es Salaam kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambao utaboresha umeme maeneo ya Kigamboni, Kurasini, Mbagala, Mkuranga, Kisarawe, Gongolamboto, Ukonga, Kitunda, Vingunguti na Tabata
Mradi mwingine ni unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan ambao utasaidia kuondoa matatizo yaliyo katika maeneo ya Muhimbili na Upanga, Mwananyamala na Kinondoni, Oysterbay na Masaki, Jangwani Beach, Bahari Beach na Mbezi Beach.
Mradi mwingine ni ule unaotekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ambao unaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Shinyanga, na Geita.
Mradi mwingine ni ule unaofadhiliwa na Serikali ya Finland ambao utasaidia sana kuimarisha umeme kati kati ya jiji la Dar es Salaam na kusaidia kuimarisha umeme katika eneo lenye majengo mengi marefu la Samora, Azikiwe, Kariakoo na Sea view.
Sambamba na miradi hiyo inayotekelezwa Dar es Salaam, mradi mkubwa wa kupeleka umeme wa 400KV kutoka Iringa kupitia Mtera, Dodoma, Singida hadi Shinyanga uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika na hivyo kutuhakikishia umeme wa uhakika katika kanda ya ziwa hasa jiji la Mwanza.
Kazi ya kuunga Songea na Gridi ya Taifa kutokea Makambako kwa 220KV inaendelea na Makandarasi wako kazini.
Kazi za kuunga Tanzania na Kenya kwa umeme wa 400KV inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani zabuni za kuwapata Makandarasi ziko katika hatua za mwisho. Ujenzi unategemewa kuanza mwakani.
Kazi nyingine ambazo hazijaanza lakini zitaanza hivi karibuni ni pamoja na Dar es Salaam – Somanga (400KV), Bulyankhulu – Geita – Nyakanazi – Rusumo (220KV)
Miradi hii ya kuimarisha miundombinu ikikamilika itasaidia kulipunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme kutokana na mfumo wa Usambazaji.
Nawaomba wateja wetu, wakati kazi hii kubwa inapoendelea, wawe na subira na uvumilivu kwa usumbufu wa hapa na pale utakaokuwa unatokea. Hata hivyo TANESCO itajitahidi kurekebisha kasoro zinazoweza kurekebishwa katika miundombinu ya sasa ili kupunguza usumbufu huo wakati marekebisho makubwa yakiendelea.
Hizi ni hadithi zile zile mkuu watanzania tumeshazizowea tuangalie uhalisia wenyewe site,mfano hapa dsm kukatika katika umeme ni jambo la kawaida sana,nenda mkoani mtwara akotok gesi ndio utazimia kabisa wilaya za tandahimba,newala,masasi,ruangwa, nachingwea umeme ukimaliza siku haujakatika watu wanashangilia
 
Wana lelewa sana hawa wakati ni jipu la kupasua kwa sululu ukiwasikiliza ni ulaghai mtupu na kutumia fedha nyingi kwenye vyombo vya habari kujinadi.
Mkuu hawa jamaa wamejisahau sana na ukifika mikoani ndio balaa yaani mfanyakazi wa tanesco anaanza kulewa pombe kuanzia saa 4 na lugha za kilaghai
 
Hapana simu huwa azizimwi, sambamba na hilo tanesco walitoa namba za simu za mameneja wa Kanda na Mikoa iwapo hujahudumiwa vizuri na customer care, unawasiliana nao moja kwa moja.
Pokea namba hizi 0658-768581/0713-768581 fanyia utafiti, kuna wakati akiwa Waziri wa nishati Simbachawene ali pata matokeo flani kwenye ofisi zenu za customer care kama ni mfuatiliaji uta kumbuka kuwa aliondoa mtu, so jaribu kuwa mfuatiliaji.
 
TANESCO inapata faida kwa wateja wa kubwa
wenye viwanda na biashara kubwa asilimia 75

wananchi wanachangia asilimia 25 tu..

mtu binafsi unafikiri atajali sana hao wananchi wanaoleta faida asilimia 25?
mtu binafsi atajali wanaomletea faida tu ya kutosha
kuna mikoa na vijiji umeme watausikia kwa redio tu

Ili umeme uwe ni huduma inayopatikana kwa kila mtu
serikali lazima ibebe dhamana
Kwa maana yako mkuu huu mradi wa rea utaishia kusimika nguzo tu?
 
Asante nitakujibu, ngoja nifuatilie
Sijui na si hitaji kujua nafasi yako ila kama ni kweli nitashukuru sikupenda utetee tu bila kujua hali ikoje maana kuna muda tuna lazimika kupiga mikocheni kuuliza matatizo ya mbezi beach kwa ajili ya uzembe wa kituo cha Tangi bovu.
 
Ndugu wana jamvi tumeshuhudia umeme ukiwa unakatika katika kila uchao na kupelekea baadhi ya watanzania wenzetu kupoteza mali zao kwa kuungua baada ya umeme kurudi kwa nguvu na wafanya biashara wengine kupata hasara kwa bidhaa zao kuoza kutokana na umeme usiokuwa na uhakika,ni kwanini serikali inazidi kulikumbati tanesco?kwanini wasibinafsishe kama mashirika mengine?
Lisibinafsishwe. Ila yaruhusiwe makampuni kuwekeza kwenye umeme maana mm kilio changu ni bei za umeme zisizoendana na maisha ya mtanzania wa hali ya chini
 
Back
Top Bottom