N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,990
- 12,019
Foleni jijini Dar es Salaam zimekuwa kero kubwa kwa uchumi na maisha ya wananchi. Muda unapotea, gharama za usafiri zinaongezeka, na uzalishaji unapungua. Haya hapa Mapendekezo mahsusi ya kuchukua:
1️⃣ Marufuku Malori Zaidi ya Tani 7 Kuingia Katikati ya Mji (Mchana)
Iwekwe marufuku kwa malori yote zaidi ya tani 7 kuingia CBD na maeneo ya katikati ya jiji kuanzia asubuhi hadi jioni.
Yaruhusiwe kuingia usiku kuanzia saa 5 hadi saa 10 alfajiri tu.
Hii itapunguza msongamano mkubwa unaosababishwa na magari makubwa barabarani wakati wa shughuli nyingi za kiuchumi.
2️⃣ Ratiba Maalum kwa Malori ya Usiku
Malori yatakayoruhusiwa kuingia usiku yawe yale ya mizigo ya mali mbichi (perishable goods/ raw materials) yanayoelekea bandarini pekee.
Hakuna kuingia kiholela.
Bandari ni muhimu kwa uchumi, lakini shughuli zake zisimamishe mji mzima mchana?. Mizigo yake ama ibebwe usiku au ipelekwe ICD ya Kwala.
3️⃣ Kuhamisha Kituo cha Kupakilia Mizigo – Jangwani
Eneo la Jangwani si rafiki kwa mizigo mikubwa kutokana na jiografia ya eneo lenyewe na ufinyu wa barabara kwa malori mengi yanayokusanyika pale kila uchao.
Kituo cha kupakilia mizigo:
📍 Kihamishiwe Mbezi Mwisho – kwa mizigo ya mikoa ya Magharibi, Lake Zone na Juu Kusini.
📍 Kituo cha Mizigo ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha) ihamishiwe Bunju ‘B’.
Hatua hii itazuia malori kupita katikati ya jiji bila sababu.
4️⃣ Marufuku Kali ya Kuegesha Malori Mjini
Malori yasiruhusiwe kuegeshwa ndani ya mji, hasa barabarani au pembeni ya biashara.
Utekelezaji uwe wa kweli – si wa msimu.
5️⃣ Kuongeza Ushuru wa Maegesho Katikati ya Mji (Double)
Ushuru wa maegesho CBD uongezwe mara dufu ili:
Kupunguza watu wanaoingia mjini kwa magari binafsi
Kuhamasisha matumizi ya usafiri wa umma
Hatua hii imesaidia katika miji mingi duniani (Dar jiji mnaweza kwenda ku-benchmark).
6️⃣ Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT) Kuongeza Ruti Mpya
Mabasi ya mwendo kasi yaongeze ruti maalum za:
🚌 Posta
🚌 Kariakoo
Maeneo haya ndiyo moyo wa biashara – bila usafiri wa uhakika, foleni hazitaisha.
Mfumo wa Dar Rapid Transit uongeze mabasi na safari katika ruti hizi ili kupunguza utegemezi wa magari binafsi na ikibidi yaanzishwe mabasi ya executive nauli ianzie 3,000 TZS kwa ruti ili executives watumie hayo maana wabongo tunapebda sana class.
Hitimisho
Suluhisho la foleni halihitaji miujiza – linahitaji maamuzi magumu na utekelezaji thabiti.
Dar es Salaam ni kitovu cha uchumi wa Tanzania; haiwezekani jiji litembee kwa kasi ya konokono kila siku.