Dawa ya kidonda cha kuchomwa na mwiba

Mangusha942

Member
Jan 15, 2020
86
220
Habari za leo wana jamii,

Naomba sana msaada wenu katika hili. Nina baba yangu mkumbwa alichomwa na mwiba kwenye goti akautoa then baada ya siku 3 pakaanza kuwasha pale alipochomwa na mwiba katika kujikuna kumbe ndani kulikua na kipande kidogo cha mwiba kilibakia basi akakitoa then akaenda kuchomwa sindano ya tetenasi.

Baaada kama ya nusu saa tu baada ya kuchomwa sindano ya tetenasi akaanza kusikia maumivu makali sana na mguu ukaanza kuvimba mpaka kutembea akawa hawezi tena. Baada kama ya siku moja mguu ukaanza kuvimba na maumivu makali sna, tukampeleka hospitali mguu ukaanza kutoa ngozi pale kwenye goti kidonda kikawa kikubwa sana mpk wakamuhamishia Temeke hospitali.

Yaani hapa ninapoongea anazaidi ya siku 20 yupo temeke na mguu mzima umekua kidonda kuanzia kwenye paja mpaka chini kwenye kifundo. Naomba kujua kama kuna dawa za kukausha kidonda kama hichi coz kule hospitali kidonda hakikauki licha ya kutumia dawa na kusafishwa kila siku.

Au kama kuna hospitali nzuri zaidi yenye kutibia vidonda vya aina hiyo au kama kuna mwanajamii alishawahi kupata tatizo kama hilo na njia walizotumia kupona. Naomba kuwasilisha. Samahani kwa uandishi mbaya sio mzuri sana kwenye kuandika but i hope nimeeleweka
 
Hapo Temeke wanaweza kuwa rufaa kwenda Muhimbili muonane na team ya vascular wounds.
 
Duuh ishu hapo mzee! Seems kuchelewa kuchomwa TT ni ishu hapo sasa kama yupo Temeke na hakuna dalili za kupona better aamie hosp kubwa ya rufaa hii itasaidia zaidi.
 
Back
Top Bottom