Dawa ya Katiba Mpya Kura ya Maoni - Membe

Dawa ya Katiba Mpya Kura ya Maoni - Membe

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,428
Reaction score
6,344
membe.jpg

Dar es Salaam. Kama ilivyo kwa makada wengine wa CCM, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anaona kuwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilifanya kosa moja; iliamua kuwateulia Watanzania idadi ya serikali za Muungano.

Membe anaona dawa pekee ya kumaliza mgogoro huo unaotishia kupatikana kwa Katiba Mpya, ni kuitisha kura ya maoni ili wananchi waamue kwanza wanataka Muungano wa serikali ngapi ndipo mchakato uendelee.

Katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita, Waziri Membe alisema kama ni kuepuka gharama, basi kura ya maoni ifanyike sambamba na Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka 2015.

"Kwa maoni yangu, utengenezaji wa katiba uko sawa na safari inayoanzia Dar es Salaam kwenda Kigoma," alisema Membe ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba kutokana na kuwa Mbunge wa Mtama na kuongeza, "Kwa hiyo mnapotaka kusafiri, ni lazima mkubaliane aina ya usafiri kabla ya kuanza safari. Mkishaamua kusafiri kwa treni, mnajua safari itakuwaje."

Alisema sura ya kwanza kwenye katiba yoyote ni muhimu kwa kuwa ndiyo inayoamua mambo mengine yanayofuata. Kwa maana hiyo, Waziri Membe anasema ingekuwa busara kwanza kuamua muundo wa Muungano kwa kuwa sura nyingine zinazofuata zinarejea kwenye sura ya kwanza, jambo ambalo halikufanyika.

"Sura hii ndiyo itakayoleta mwanga wa nini kijadiliwe kwenye sura nyingine zote. Sasa kama hatukubaliani hapo, tutajadilije vifungu vingine ndani ya katiba hiyo?" alihoji.

Akizungumzia kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, alisema ilifanya kosa moja tu la kuandika rasimu moja tu na kuwateulia Watanzania idadi ya serikali na kuiwasilisha kwenye Bunge la Katiba.

Alisema wakati Tume ya Warioba ilizunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi na kwamba wapo waliosema wanataka serikali mbili, wapo pia waliotaka serikali moja na vilevile wapo waliotaka tatu.

"Ilipaswa kurekodi maoni hayo kama yalivyo na kuyapeleka bungeni ili Bunge liyapitie na kufanyia uamuzi kulingana na mahitaji yaliyopo. Alipokosea Warioba na timu yake ni kupeleka bungeni rasimu moja yenye maoni ya pendekezo moja tu la serikali tatu," alisema Membe ambaye alijinadi kuwa ana uzoefu mkubwa katika masuala hayo ya kuandika katiba kutokana na kushiriki kutatua migogoro sehemu nyingi duniani, ikiwamo Zimbabwe.

"Walitakiwa kuja na rasimu tatu; ya serikali tatu, mbili au moja. Duniani kote panapokea tofauti ya mawazo katika mambo ya msingi kama hilo, kunapelekwa rasimu nyingi bungeni ili Bunge lijadiliane kwanza na kufikia maafikiano, kabla ya kuendelea na kupitisha vifungu vingine.

"Hata kina Warioba walitakiwa waje na rasimu tatu bungeni; moja iwe ile ya watu wanaotaka serikali moja, nyingine iwe ya wale waliotaka serikali mbili na pia iletwe rasimu ya wale wanaotaka serikali tatu. Kisha wangesema (kina Warioba) maoni yetu sisi (tume) ni Serikali tatu. Sasa wao, mengine wameyamaliza wenyewe na bungeni wakaleta rasimu moja tu ya serikali tatu."

Alisema pamoja na kosa hilo, bado Tanzania ina fursa ya kujisahihisha kwa kuitisha kura ya maoni... "Sasa, dawa yake ni moja tu. Twendeni kwa wananchi ili waamue kwa kupewa swali moja. Unataka serikali ngapi?" alisema.

"Tunaweza kufanya kura ya maoni kwa njia mbili. Kwanza kuitisha kura ya maoni ili wananchi wajibu swali moja tu na pili, kama hiyo ni gharama, basi wakati wa uchaguzi mwakani, tupige kura nne. Moja ya Rais, nyingine ya mbunge, ya diwani na boksi jingine liwe la idadi ya serikali."

Waziri Membe alisema suala la idadi ya Serikali ni moyo wa mchakato mzima wa Katiba, hivyo linapaswa kupatiwa ufumbuzi kwanza kabla mambo mengi hayajaendelea.

Kuhusu Ukawa

Alipotakiwa kuzungumzia hatua ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vya chombo hicho cha kuandika Katiba, alisema: "Jumuiya ya kimataifa inawashangaa. Wamekuwa wakiwaunga mkono kwa mambo mengi, lakini katika hili hawako pamoja nao."

Alisema kitendo cha wachache kususia Bunge ni cha ajabu na hakijawahi kutokea katika nchi nyingine zaidi ya Tanzania.

"Ni ajabu wachache kujigeuza kuwa pressure group (wana harakati). Ukiachia watu wazuie Bunge (la Katiba) kwa sababu tu hawapo, unaua dhana ya demokrasia. Kama wachache wanatumia vibaya kutambuliwa kwao au mwaliko, tutaiharibu nchi. Nguvu ya wachache haiko kwenye kususia vikao, bali ndani ya Bunge la Katiba. Ninaamini baadhi yao wanajuta kwa kususia vikao."

Alitetea kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake wakati akizindua Bunge la Katiba kwa maelezo kuwa alifanya hivyo ili kuwapa changamoto.

"Ilikuwa ni food of thought (kitu cha kusaidia kutafakari). (Kikwete) Halazimishi. Hakwenda pale kama Kikwete, bali kama presidency (taasisi ya urais)," alisema.

Membe alisema hakuna mshindi katika mchakato wa Katiba Mpya, hivyo hakuna maana watu wakavutana kiasi cha kutaka kuuathiri mchakato huo ambao tayari umetumia mabilioni ya shilingi.


Chanzo:Mwananchi
 
Dar es Salaam. Kama ilivyo kwa makada wengine wa CCM, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anaona kuwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilifanya kosa moja; iliamua kuwateulia Watanzania idadi ya serikali za Muungano.

Membe anaona dawa pekee ya kumaliza mgogoro huo unaotishia kupatikana kwa Katiba Mpya, ni kuitisha kura ya maoni ili wananchi waamue kwanza wanataka Muungano wa serikali ngapi ndipo mchakato uendelee.

Katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita, Waziri Membe alisema kama ni kuepuka gharama, basi kura ya maoni ifanyike sambamba na Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka 2015.

“Kwa maoni yangu, utengenezaji wa katiba uko sawa na safari inayoanzia Dar es Salaam kwenda Kigoma,” alisema Membe ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba kutokana na kuwa Mbunge wa Mtama na kuongeza, “Kwa hiyo mnapotaka kusafiri, ni lazima mkubaliane aina ya usafiri kabla ya kuanza safari. Mkishaamua kusafiri kwa treni, mnajua safari itakuwaje.”

Sura hii ndiyo itakayoleta mwanga wa nini kijadiliwe kwenye sura nyingine zote. Sasa kama hatukubaliani hapo, tutajadilije vifungu vingine ndani ya katiba hiyo?” alihoji.

Akizungumzia kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, alisema ilifanya kosa moja tu la kuandika rasimu moja tu na kuwateulia Watanzania idadi ya serikali na kuiwasilisha kwenye Bunge la Katiba.

Alisema wakati Tume ya Warioba ilizunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi na kwamba wapo waliosema wanataka serikali mbili, wapo pia waliotaka serikali moja na vilevile wapo waliotaka tatu.

“Ilipaswa kurekodi maoni hayo kama yalivyo na kuyapeleka bungeni ili Bunge liyapitie na kufanyia uamuzi kulingana na mahitaji yaliyopo. Alipokosea Warioba na timu yake ni kupeleka bungeni rasimu moja yenye maoni ya pendekezo moja tu la serikali tatu,” alisema Membe ambaye alijinadi kuwa ana uzoefu mkubwa katika masuala hayo ya kuandika katiba kutokana na kushiriki kutatua migogoro sehemu nyingi duniani, ikiwamo Zimbabwe.

“Walitakiwa kuja na rasimu tatu; ya serikali tatu, mbili au moja. Duniani kote panapokea tofauti ya mawazo katika mambo ya msingi kama hilo, kunapelekwa rasimu nyingi bungeni ili Bunge lijadiliane kwanza na kufikia maafikiano, kabla ya kuendelea na kupitisha vifungu vingine.

Hata kina Warioba walitakiwa waje na rasimu tatu bungeni; moja iwe ile ya watu wanaotaka serikali moja, nyingine iwe ya wale waliotaka serikali mbili na pia iletwe rasimu ya wale wanaotaka serikali tatu. Kisha wangesema (kina Warioba) maoni yetu sisi (tume) ni Serikali tatu. Sasa wao, mengine wameyamaliza wenyewe na bungeni wakaleta rasimu moja tu ya serikali tatu.”

Alisema pamoja na kosa hilo, bado Tanzania ina fursa ya kujisahihisha kwa kuitisha kura ya maoni… “Sasa, dawa yake ni moja tu. Twendeni kwa wananchi ili waamue kwa kupewa swali moja. Unataka serikali ngapi?” alisema.

Tunaweza kufanya kura ya maoni kwa njia mbili. Kwanza kuitisha kura ya maoni ili wananchi wajibu swali moja tu na pili, kama hiyo ni gharama, basi wakati wa uchaguzi mwakani, tupige kura nne. Moja ya Rais, nyingine ya mbunge, ya diwani na boksi jingine liwe la idadi ya serikali.”

Waziri Membe alisema suala la idadi ya Serikali ni moyo wa mchakato mzima wa Katiba, hivyo linapaswa kupatiwa ufumbuzi kwanza kabla mambo mengi hayajaendelea.

Kuhusu Ukawa
Alipotakiwa kuzungumzia hatua ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vya chombo hicho cha kuandika Katiba, alisema: “Jumuiya ya kimataifa inawashangaa. Wamekuwa wakiwaunga mkono kwa mambo mengi, lakini katika hili hawako pamoja nao.”

Alisema kitendo cha wachache kususia Bunge ni cha ajabu na hakijawahi kutokea katika nchi nyingine zaidi ya Tanzania.

“Ni ajabu wachache kujigeuza kuwa pressure group (wana harakati). Ukiachia watu wazuie Bunge (la Katiba) kwa sababu tu hawapo, unaua dhana ya demokrasia. Kama wachache wanatumia vibaya kutambuliwa kwao au mwaliko, tutaiharibu nchi. Nguvu ya wachache haiko kwenye kususia vikao, bali ndani ya Bunge la Katiba. Ninaamini baadhi yao wanajuta kwa kususia vikao.”

Alitetea kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake wakati akizindua Bunge la Katiba kwa maelezo kuwa alifanya hivyo ili kuwapa changamoto.

“Ilikuwa ni food of thought (kitu cha kusaidia kutafakari). (Kikwete) Halazimishi. Hakwenda pale kama Kikwete, bali kama presidency (taasisi ya urais),” alisema.

Membe alisema hakuna mshindi katika mchakato wa Katiba Mpya, hivyo hakuna maana watu wakavutana kiasi cha kutaka kuuathiri mchakato huo ambao tayari umetumia mabilioni ya shilingi.

Membe hataki serikali 3 na hataki Tanganyika irudi. Mimi nataka tuwe na serikali 2 na ya 3 iwe dola
 
Kwaiyo membe anaungana na CCM wenzake kuikebehi Tume ya mabadiliko ya katiba? mana huyu inasemekana ni rais mtarajiwa wa JMT sasa kwa mpango huo inaonekana wazi hatakuwa na nia njema kuleta maridhiano na maslahi katika nchi. Ile tume haikuwa na mtazamo wake binafsi s3 zilikuja baada Tume kuchambua maoni ya wananchi na migogoro iliyopo tume ikaona muarubaini ni kuwepo shirikisho la serikali 3. Sasa membe anaposema Tume iliwachagulia watu s3 anakuwa anakosa mvuto kuwa rais wa nchi iliyo na mgogoro wa muungano kama ilivyo Tanzania sasa. bado atakuja na system ile ile Tanganyika kujivalisha koti la muungano.
 
Membe anatapatapa. Yeye ni member wa baraza la mawaziri, alikuwapo wkt baraza linapitia terms of reference walizopewa tume ya Warioba. Kwa asitoe hoja hizi then? Sheer hypocrisy!!
 
weneywe CCM hawaamini wanachokifanya ndio maana unasikia mara kura ya maoni mara hili. Kwa nini asishauri sasa bunge lisitishwe ipigwe hiyo kura ya maoni?
 
Jambo moja alilosema la MAANA ni la kura ya maoni kuhusu muundo wa serikali. Na hii ndiyo practical solution. Lakini sidhani kama CCM watakubali kwani CCM S2 NI LAZIMA.

Kuhusu kuandika rasimu 3, ameniacha hoi pale aliposema wangeandika hata rasimu ya S1. Inaelekea huyu mheshimiwa hafahamu kwamba tume ya mabadiliko katiba, hadidu za rejea ilizopewa pamoja na nyingine, lakini iliambiwa lazima itambue uwepo wa SMZ. Kwa mantiki hiyo hoja ya S1 ilikuwa imshauwawa from the day one.

CCM wapo wenye akili lakini tatizo lao ni wanafiq. Kama Membe anasimamia anachokisema, basi aishauri CCM yao wasitishe BMK, 2015 wakati wa uchaguzi mkuu pia iitishwe kura ya maoni ya muungano tunaotaka S1, S2, au S3.

Lakini CCM ikikubari hili wazo basi ARDHI na MBINGU vitashikana.

Kosa ni letu Watanzania tumeamua kucheka na manyani (CCM) basi tutegemee kuvuna mabua (katiba mbovu)
 
Namuunga mkono hapa..."nguvu ya wachache haionekani nje ya bunge kwa kujifanya kama pressure group bali ndani ya bunge"
Kumshinda adui si kwa kukimbilia vichakani ila kwa kuingia kwa umakini ktk uwanja wa vita
 
Membe anatapatapa. Yeye ni member wa baraza la mawaziri, alikuwapo wkt baraza linapitia terms of reference walizopewa tume ya Warioba. Kwa asitoe hoja hizi then? Sheer hypocrisy!!

Na sio hilo la kuwa alishiriki baraza la mawaziri tuu.huyu nae ni mmoja wa wapuuzi kama alivyo 6 na magamba leaders .ina maana hajui kuwa serikali moja haitakiwa na wazanzibar .kwakuwa itawameza .na ina maana hajui kuwa. Serikali mbili ndio katiba tunayo tumia sasa.ambayo ina matatizo kibao .ambayo tumeshindwa kuyatatua .ina maana hajui kuwa kuna aina 3 tuu za miungano ya nchi .na kwamba ni mmoja tuu uliobaki ambao ni wa serikali 3 .,madai yake yanaonesha ni jinsi gani ccm wanatuwekea mawaziri mburula .shame on him Membe
 
Mh. Membe anatuchanganya na kujichanganya. Sheria iliyoanzisha mchakato wa Katiba na kuunda inavyojulikana kama Tume ya Warioba haikuelekeza anavyopendekeza. Wao walitakiwa wakusanye na kuyachambua maoni ya wananchi na watoe Rasimu moja ya Katiba na siyo mbili au tatu. Lakini pia maoni yake yangefuatwa, yangeonyesha mtu/Tume isiyo na maamuzi. Mzee Warioba na timu yake siyo wa jinsi hiyo, walifuata sheria ilivyowaelekeza na wakatenda vyema na kutoa kitu bora ilivyotakiwa.
 
Kila mtu kawa mtaalamu wa katiba. Hivi kweli tunajitambua sisi?
Tume ya warioba ilipewa nyenzo zote muhimu ikiwa ni pamoja na wataalamu bobezi wa sheria na katiba. Inakuwaje leo wanasiasa wa vyama ndio watuamulie eti wale hawakujuwa kazi yao?!
Huku ni kupotea njia ya sawa kwa makusudi.
Mimi nadhani kura ya maoni isiwe juu ya idadi ya serikali tu bali hata muungano wenyewe umetuchosha mno,wanaume hawashikiani hatamu farasi.
Tuulizwe "JE MUNAUTAKA MUUNGANO? na
Kama jibu ndio,
SSERIKALI NGAPI?
 
Back
Top Bottom