Chango la uzazi baada ya kujifungua
Wanawake wengi wamekuwa wakilalamikia maumivu ya tumbo mara baada ya kujifungua hasa wakati wanapokuwa wananyonyesha. Wenyewe huita chango la uzazi. Hali hiyo ni ya kawaida.
Je hali hiyo husababishwa na nini?
Mara baada ya mama kujifungua mwili wake unakuwa unatoa homoni iiitwayo oxytocin. Homoni hii kazi yake kubwa ni kusaidia maziwa kutoka. Sasa mama anapokuwa ananyonyesha homoni hii inatolewa kwa kiasi kikubwa. Homoni hii inakwenda kwenye mfuko wa uzazi ambako inasababisha mfuko wa uzazi kujikamua. Mfuko wa uzazi unapokuwa unajikamua ndipo unasikia maumivu makali na pia utaona hata damu zinatoka kwa wingi.
Iwapo unapata maumivu haya unaweza kutumia dawa za maumivu. Mara nyingi maumivu huisha yenyewe baada ya siku kumi.