Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Dawa ya Aspirin yawasaidia baadhi ya watu kukinga ugonjwa wa moyo na saratani ya utumbo mpana (colon)
Kikundi cha huduma ya kinga cha Marekani USPSTF kimesema, matumizi ya kidonge kimoja cha aspirin kila siku kinawasaidia baadhi ya watu kukinga ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kiharusi na saratani ya utumbo mpana.
Kikundi hicho cha USPSTF ni kikundi kinachoundwa na madaktari na wanasaynasi amabcho kinaungwa mkono na serikali ya Marekani. Kikundi kimependekeza kuwa mchago wa aspirin katika
kinga ya maradhi ya moyo na saratani ya utumbo mpana ni mkubwa kuliko hatari ya kutokwa damu inayoletwa na dawa hiyo, lakini swala la ikiwa mchango huo ni mkubwa au la unategemea na umri wa wagonjwa na hatari ya ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo inayowakabili.
Pendekezo limesema, kutumia aspirin miligramu81 kila siku kutawanufaisha wagonjwa wa ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo wenye umri wa miaka 50 hadi 59. Kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 60 hadi 69, mchango wa aspirin ni mdogo. Kwa wagonjwa wenye umri chini ya
miaka 50 au zaidi ya miaka 70, mchango wa aspirin bado unahitaji utafiti zaidi.
Ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo na saratani ya utumbo mpana ni chanzo kikuu cha wamarekani, na asilimia 30 ya vifo vya wamarekani inatokana na ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa kiharusi.
Mkuu.@Asprin upo?