Dawa ya Aspirin yawasaidia baadhi ya watu kukinga ugonjwa wa moyo na saratani ya utumbo mpana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Asprin.jpg
Asprin dawa.jpg


Dawa ya Aspirin yawasaidia baadhi ya watu kukinga ugonjwa wa moyo na saratani ya utumbo mpana (colon)


Kikundi cha huduma ya kinga cha Marekani USPSTF kimesema, matumizi ya kidonge kimoja cha aspirin kila siku kinawasaidia baadhi ya watu kukinga ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kiharusi na saratani ya utumbo mpana.

Kikundi hicho cha USPSTF ni kikundi kinachoundwa na madaktari na wanasaynasi amabcho kinaungwa mkono na serikali ya Marekani. Kikundi kimependekeza kuwa mchago wa aspirin katika

kinga ya maradhi ya moyo na saratani ya utumbo mpana ni mkubwa kuliko hatari ya kutokwa damu inayoletwa na dawa hiyo, lakini swala la ikiwa mchango huo ni mkubwa au la unategemea na umri wa wagonjwa na hatari ya ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo inayowakabili.

Pendekezo limesema, kutumia aspirin miligramu81 kila siku kutawanufaisha wagonjwa wa ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo wenye umri wa miaka 50 hadi 59. Kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 60 hadi 69, mchango wa aspirin ni mdogo. Kwa wagonjwa wenye umri chini ya
miaka 50 au zaidi ya miaka 70, mchango wa aspirin bado unahitaji utafiti zaidi.
Ugonjwa wa mishipa ya damu na moyo na saratani ya utumbo mpana ni chanzo kikuu cha wamarekani, na asilimia 30 ya vifo vya wamarekani inatokana na ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa kiharusi.

Mkuu.@Asprin upo?
 
Je kuanzia miaka 27kushuka chini tutumie asprin junior au yoyote
 
Nimekua nikiitumia asprin nachanganya na pipi Kali kutibu kikoozi, nazitafuna kwa pamoja asprin 2 kwa pipi moja.
 
Ninaziponda sana Dawa za kizungu zina madhara mwilini Huwa wanapenda kutaja faida zake tu lakini hasara hawazitaji ndio ninaziponda Dawa za kizungu kwangu mimi ni sumu.

Kwanini unashauri watu watumie aspirin na wakati ni dawa ya kizungu

Waambie watu wakatafune gome la Willow Tree badala yake
 
Ninaziponda sana Dawa za kizungu zina madhara mwilini Huwa wanapenda kutaja faida zake tu lakini hasara hawazitaji ndio ninaziponda Dawa za kizungu kwangu mimi ni sumu.
Bosi madhara ya dawa pia huwa yanaandikwa kwenye leaflet ya kila dawa.Na vilevile suala la kutokuyasema madhara wajibu unao wewe mwenyewe kuuliza kwa mtoa huduma husika..mfano aspirin si kwamba Asprin ni nzuri tu poa ina madhara yake pia
 
Kwanini unashauri watu watumie aspirin na wakati ni dawa ya kizungu

Waambie watu wakatafune gome la Willow Tree badala yake
Nina washauri watumie Aspirin ninajuwa watakapo umwa watakuja kunitafuta nipate kuwatibia si unajuw adawa za kizungu zina madhara ukitumia muda mrefu. Kukiwa hakuan wagonjwa Ma Daktari na waganga wa kienyeji watakula wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom