Kama Prednisolone na Cetirizine hazijafua dafu, ni vyema kurudi nyuma na kutafuta chanzo cha allergy yenyewe.
Mfano:
1: kuna kitu kipya unatumia, chakula, mafuta ya kupaka vs kupikia, sabuni, nguo
2: Kuna mtu mwingine kwenye familia/kama ipo ana tatizo kama lako?
3: Vipele viko sehemu gani hasa ya mwili?
4: Kuna mtu alikuja kukutembelea au ulienda sehemu kwa kipindi ambacho muwasho ulianza?
5: Muwasho ni mkali zaidi wakati gani usiku vs mchana?
NB: Hii inaepusha kumwaga maji kuzima moto huku ukiacha petroli inaendelea kumiminika kwenye moto huohuo. Tuanze kuzuia kisababishi.