Dawa kumi ambazo mama mjamzito hatakiwi kutumia

ricksily

Member
Mar 9, 2017
89
125
Wanasema "sharing is caring" so, nkaona kuna umuhimu wa kushare hili.

Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda
sana kuzitumia lakini bahati mbaya baadhi ya
dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito
kabisa kulingana na madhara makubwa
yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto
aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.

1.Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa
mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani
una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.

2.Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano (most common), mara nyingi hutumika
kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii
huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu
kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi
kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza
kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani
kiziwi.

3.Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana
kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara
nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa
ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa.
Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na
huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.

4.Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa
mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama
capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika
kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya
huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa
mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na
kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo
pungufu au zaidi.

5.Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni
salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi
mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza
kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya
mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na
viungo vya kawaida.

6.Metronidazole au fragyl; hii dawa ipo kwenye
kundi la anti protozoa lakin pia hushambulia
bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua
minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko
wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi
mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa
utengenezaji wa viungo vya mtoto.

7.Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye
kikundi maarufu cha prostanglandins analogue,
hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi
kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu
madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii
kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno
ikiwemo kutoa mimba kabisa.

8.Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo
humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi
tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha
kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata
matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio
dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.

9.Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu
minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za
maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama
wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa
mtoto.

10.Frusemide: hii ni dawa ambayo inapatikana
kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi
hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya
mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu
presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa
akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na
presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha
chini kabisa[intravascular volume depletion].

Together we can maintain healthy for the people
 
ben10jr

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
223
500
Mkuu naomba ufanye masahihisho kidogo hapo namba 6:
Metronidazole = Flagyl (Sio Fragile). Na hii sio antibacteria bali ni antiprotozoa ( inaua vimelea aina ya/kundi la Protozoa na sio Bacteria)
Na mwisho, hivi vimelea aina ya Protozoa sio minyoo, ni tofauti kabisa na wadudu walio kwenye kundi la minyoo (Helminths/Worms). Ni hayo tu mkuu
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,701
2,000

Inatumika pia kama anti bacteria, na inafanya kazi nzuri sana ikichanganywa na dawa nyingine kama vile ciproflaxin kupambana na bacteria sugu aina ya gram negative
 
Yes broda Kavulata, it acts as an antibacteria only when in combination with another drug (double or triple therapy). Lakini hapa haimaanishi yenyewe itaenda kuua bacteria bali itaua Protozoa wanaoweza kuwepo kama co infection
 
TRUVADA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,520
2,000
Frusemide:
Hivi mama akiwa mja mzito anakuwa na presure ya kupanda au kushuka
Ok
Oral hypoglycemic agent÷

Sulfonylureas ( insulin secretogogies)- glimepiride, 5glipizide, glyburide,Chlorpropamide

Biguanides - eg metformin.

Thiazolidinediones -eg pioglitazone,

Hata sodium valproic acid has terratoginicity effect result to neurotube
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,701
2,000
Yes broda Kavulata, it acts as an antibacteria only when in combination with another drug (double or triple therapy). Lakini hapa haimaanishi yenyewe itaenda kuua bacteria bali itaua Protozoa wanaoweza kuwepo kama co infection
pamoja sana
 
play synergism with other drugs on anti bacterial effect.
 
y-ran

Member
Mar 14, 2017
25
45
Inatumika pia kama anti bacteria, na inafanya kazi nzuri sana ikichanganywa na dawa nyingine kama vile ciproflaxin kupambana na bacteria sugu aina ya gram negative
Thanks nakuheshim mkuu hata mm nliliona hlo
 
y-ran

Member
Mar 14, 2017
25
45
Mkuu ilisahau kama ipo Gentamycin cream au bado upo shule hujatoka darasani njoo nje uwone mambo ila hongera sana kwa elimu mungu atakusaidia
0990ed4dffa2e9f33c1adcfbb7064230.jpg
 
lopinavir

Senior Member
Jul 11, 2015
180
250
Bandiko zuri sana hili.....!!
-Kuna dawa ya chunusi inaitwa Isotretinoin,mwanamke anaetarajiwa kushika mimba ndani ya mwezi au aliyetayari na mimba hatakiwi pia kuitumia

-
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom