Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Moja ya kauli nzito ambayo Rais wetu amekuwa akiirudia na kuongea kwa uzito na msisitizo ni ile ya kwamba dhamira yake ni kuchukua hatua kwa uozo wowote kwa maslahi ya Umma hata kama ungemuhusu mke wake Janneth.
Ni bahati mbaya sana. tena sana. kwamba namna Rais anavovuta miguu kuhusu tuhuma dhidi ya RC wake huyu, zimepoteza kabisa imank ya kama kweli Rais wetu ni mkweli na anasimamia dhamira hiyo aliyotuaminisha.
RC ametuhumiwa vyeti, kashindwa kujibu kwa kutoa vyeti. imekuwa mjadala nchi nzima miezi sasa. mamlaka za Serikali zipo kimya. pengine zinaogopa mapenzi yako kwa RC huyu. na wewe tofauti na kawaida yako tumeona kwa RC huyu unavuta miguu tuuu. unashindwa japo kuzitaka mamlaka zithibitishe au zikanushe mzozo umalizike
Hilo halijaisha, zimefuata tuhuma za uhusiano kati ya RC na wanaosadikiwa kuwa wathhumiwa wa biashara za madawa. nchi nzima inasoma. zimewekwa mpaka kadi za magari na nyaraka za TRA. mtuhumiwa yupo kimya na mamlaka husika hazikanushi wala kuthibitisha.
Sasa leo kuna tuhuma za RC wako kuvamia kituo cha Clouds akitumia askari wako. na kwamba lengo ikiwa kushinikiza matakwa yake katika vita yake na Gwajima kuhusu vyeti, vita ambayo kwa maoni yangu imekuwa ya Gwajima vs Makonda sababu yako wewe Rais kutochukua hatua kwani inahusu uadilifu na agenda yako ya vyeti feki kwa maslahi ya taifa.
Mhe Rais binafsi sina chuki na wewe, nakwambia ukweli kama washauri wako hawakwambii, nikwamba namna ulivoshindwa katika suala la Makonda umethibitisha kwamba wewe sio mpenda haki na usawa kama ambavyo ulipenda tukuone siku zote. tuhuma na video inayosambaa kumwonesha RC wako anavamia Radio Clouds ni mfano mbaya kabisa unaopatikana kwenye nchi zenye tawala za hovyo kabisa kama Burundi na sio nchi kama Tanzania yenye historia kubwa Afrika.
Mhe Rais suala hili limechefua kila mzalendo nchi hii. na tunahoji uzalendo wako upo wapi sasa? Haya mambo anayofanya msaidizi wako ni kiburi na ushamba mkubwa ambao usingevumilika kwenye nchi yenye mfumo imara wa utawala! Imefika mahala hata ukichukua hatua baadae tayari umekwishakuondoa imani ya watu kwamba wewe ni Rais usiepepesa macho inapokuja suala la kuchukua hatua hata kwa mtu anaekuhusu! Imani ya Umma ndio mtaji kwa Kiongozi. ukiwa na imani ya Umma ni wazi hutaongoza kwa amri kwani kila kauli yako itapata ufuasi mkubwa. lakini ukipoteza imani ya Umma utahitaji dola kutawala.