David Kafulila na kesi mpya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma…

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
kafulila.jpg



Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015 jimbo la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye sentensi zake; – David Kafulila

20150731001754.jpg

David Kafulila

Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembo tangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila

David-Kafulila1.jpg


Bado msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu, kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za mashitaka yote yaKafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainia na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila

chanzo.David Kafulila na kesi mpya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma.... - TZA_MillardAyo
 
Sasa huyu Tumbili analalamika nini? Kwani DPP si ndo Mkurugenzi wa mashtaka yote nchini? Yeye alitaka asaini nani?
 
Kati ya wanangu natamni mmoja wao awe mwansheria kwani hii nafasi inatumika kunyanyasa watu sana.
 
Pamoja na hila zote wanazomfanyia David Kafulila hawa maccm kuna siku wataachia wenyewe
 
Kati ya wanangu natamni mmoja wao awe mwansheria kwani hii nafasi inatumika kunyanyasa watu sana.
Sheria haiitaji mtu wa kuisoma tu bali uwe kichwa haswa, mkapa sio mwanasheria ila aliweza kujivika uwakili kwenye kesi ya balozi costa mahalu hadi akashinda.
 
Wanataka asiwe na muda wa kufanya au kufikiria mambo mengine. Anapigwa vita ya kisaikologia na kuzuiwa kujizalishia (uchumi).
 
Back
Top Bottom