David Kafulila atofautiana na Zitto Kabwe

kibokomchapaji

Senior Member
Aug 18, 2017
165
307
ZITTO AJIBIWA KWA MIKWAJU 10 YA KAFULILA.👇soma iyo!

NATOFAUTIANA NA ZITTO KUHUSU RIPOTI ZA CAG NA MWENENDO WA UCHUMI

Na David Kafulila!
Aprili 12,2020-SONGWE

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W.Bush alipata kusema kwamba uongo ukirudiwa una nafasi ya kugeuka kuwa ukweli wa watu! Pengine ni sababu hiyo, pamoja na kupongeza uamuzi wa Mhe. Zitto Kabwe kama Kiongozi wa Chama Cha Upinzani kuchambua mwenendo wa awamu ya tano katika muktadha wa uchumi na utendaji kwa kurejea ripoti za CAG, napenda kutoa maoni yangu binafsi katika mafungu10 kutofautiana na uchambuzi wake kwa lengo la kuwekana sawa kwa faida yetu sote kama watanzania!

1.Hoja kwamba Serikali ya JPM imeshindwa kukusanya mapato kulinganisha na awamu ya nne ina matobo matatu;

# Kwanza Zitto ametoa ulinganisho wa miaka3 ya mwisho wa awamu ya nne na miaka 3 ya kwanza ya JPM kwa kutaja kiasi na asilimia ya makadirio( estimates)na makusanyo(actual collections)kwa upande wa awamu ya 5 lakini akaishia kutaja asilimia ya kutofikiwa lengo bila kutaja kiasi halisi kilichokusanywa katika miaka hiyo 3 ya mwisho wa awamu ya nne.Najua alivokuwa anakwepa!

#Zitto kafanya hivyo kwa makusudi kwasababu alijua kwamba kwa mujibu wa ripoti hizo za CAG, makusanyo ya miaka3 kamili ya mwisho ya awamu ya nne( 2012/13, 2013/14 na 2014/15) yalikuwa sawa na jumla ya TZS.28trilioni karibu sawa na makusanyo ya mwaka 1 tu wa 2017/18 chini ya JPM yaliyofikia TZS.27.7Trilion.

# Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba, makusanyo ya miaka ya 2012/13 (TZS.8Trilion), 2013/14( TZS.9.28Trilion.) , na Mwaka 2014/15 ( TZS.10.77Trilion) sawa na jumla ya (TZS.28Trilioni) ambayo ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwaka mmoja tu (2017/18) chini ya JPM.

Kifupi kulinganisha uwezo wa kukusanya kodi kati ya awamu ya4 na awamu ya 5 inahitaji kuwa na nia OVU kupotosha au chuki binafsi kwani hizo awamu mbili ni mlima na kichuguu katika eneo hilo.

# Kifupi makusanyo ya awamu ya nne kwa mwezi yalikuwa wastani wa TZS. 850bn, kiasi ambacho hakikutosha hata kumudu malipo ya deni la Taifa kwa mwezi na mshahara. Malipo ya deni kwa mwezi yalikuwa wastani wa 650bn, na Mshahara kwa mwezi ilikuwa wastani 550bn sawa na 1100bn. Hivyo ilibidi kukopa kuweza kumudu kulipa mshahara.

#Pengine ndio msingi wa kejeli za Rais Uhuru Kenyatta miaka hiyo kwamba ilikuwa Kenya peke yake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoweza kumudu kulipa mshahara watumishi wake bila kukopa.

Wastani wa makusanyo ya sasa ya kodi tu kwa mwezi yanatosha kumudu deni na mshahara na hivyo Serikali haikopi tena kulipa mshahara watumishi wake.

2. Hoja kwamba Serikali inakopa sana ndani na hivyo kuathiri fursa ya sekta binafsi. Hoja hii ina matobo ya aina mbili;

# Kwanza inafahamika sura ya deni la Taifa mpaka sasa asilimia 75% ni la nje na hivyo deni la ndani ni asilimia25%. Katika mazingira ya kawaida inashauriwa Serikali ikope zaidi ndani ili inapolipa fedha hiyo sehemu kubwa ibaki kwenye uchumi ndani badala ya kwenda nje.

# Pili,Serikali ingeathiri sekta binafsi kama ingekopa kwa riba kubwa kwani kwa kufanya hivyo ingesababisha riba za benki za biashara kwa sekta binafsi kupanda kwani moja ya kigezo cha kiwango cha riba za benki ni kiasi cha riba katika soko la hatifungani( TBs auctions).

Aidha Serikali ingekuwa inakopa kwa riba kubwa ingesababisha watu binafsi wenye ukwasi kukopesha zaidi Serikali kuliko kuweka bank au kuwekeza maeneo mengine ya uzalishaji.

#Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu kuhusu minada hiyo, Mwaka 2020, Serikali inakopa soko la ndani kwa riba isiozidi asilimia 5% kwa mikopo ya siku365 kulinganisha na riba ya silimia 17% mwaka 2015.

# Kutokana na Serikali kukopa soko la ndani kwa riba chini ya asilimia 5% kulinganisha na asilimia17% mwaka 2015, ni moja ya sababu ya riba za bank za biashara kushuka kutoka asilimia 24% mwaka 2015 mpaka asilimia 16%.

3. Hoja kwamba Serikali inaficha madeni ya mifuko ya hifadhi. Hii ina matobo ya aina tatu;

# Kwanza ni changamoto ya madeni yenyewe kwa namna yalivyopatikana. Sio siri kwamba kabla ya JPM, mifuko ya hifadhi iligeuzwa shamba la bibi na mali ya genge fulani.Huu ni ukweli unaothibitishwa na taarifa ya taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya E& Y ya Disemba2015, habari za uchunguzi za majarida makubwa ya kimataifa kama Africa Confidential na Africa Research Institute.

#Kwa mfano, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, mifuko ilikuwa ikidai jumla ya TZS 5.3Trilioni lakini baada ya ukaguzi deni halali likakutwa TZS.3.2Trilion sawa na deni hewa la zaidi ya TZS.2.1Trilion.

Sielewi Kiongozi anaesisitiza deni lilipwe kama lilivyo kama kweli ana mapenzi na watanzania walipa kodi? Hata kama hana mapenzi na walipa kodi wa nchi hii vema awe japo na huruma basi!

4. Hoja kwamba Serikali ya JPM ina kesi nyingi kwa kuvunja mikataba.
Hapa ni vema ikaeleweka kwamba;

# Kwanza kesi hizo ni matokeo ya mikataba mibovu ya zamani ambayo JPM amerithi kutokana na udhaifu mkubwa huko tulikotoka na sio mikataba ndani ya awamu ya tano

# Mfano, uamuzi wa Serikali kufuta mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion iliyorithi mitambo ya Dowans/ Richmond, imepunguza mzigo wa kinachoitwa tozo ya gharama ya uwekezaji ( capacity charges) kwa mwezi kutoka dola milioni 16.35( zaidi ya bilioni 37.6)mpaka dola milioni 9.75 ( sawa na bilioni 22.4) kwa mwezi( Rejea CAG report 2017).

Inahitaji ukatili sana kwa Taifa lako kumlalamikia JPM kufuta mikataba mibovu kama Symbion kwani kinachoitwa tozo ya ya gharama za uwekezaji ni mfano wa mbaya wa mikataba ya hovyo ambapo mwekezaji analipwa bila kujali amezalisha umeme au la eti kufidia gharama alizotumia kuwekeza.

# Vema kufahamu kwamba zama za Serikali kulipa madeni ya mikataba mibovu tumeshavuka. Huko tulikotoka Serikali iliwahi kulipa deni la Dowans kinyemela kiasi cha dola milioni 94 ( zaidi ya bilioni 200 wakati huo).Hakika inahitaji roho kutamani zama hizo, ni Taifa la 'wapumbavu' linaloweza kupigania Serikali yao ilipe madeni ya aina hii!

5. Kwamba Serikali ya JPM ni ya ufujaji! Labda nikubaliane kwamba vita dhidi ya Ufisadi ni endelevu duniani kote na inaendelea Tanzania. Hata hivyo inahitaji upofu kusema Serikali hii inatatizo hilo kuliko tulikotoka. Unaweza ukabaki peke yako kwani hali halisi na Tafiti zote kitaifa na kimataifa zinathibitisha mapinduzi makubwa eneo hili;

# Mwaka 2019, Serikali ya Tanzania ilitangazwa kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha za Umma( World Economic Forum,Executive Opinion Survey 2019).Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi za Kenya ilishika nafasi ya 70, Uganda 100, Ethiopia 48, Malawi 106, Msumbiji 118 , Ghana 61, Zambia 68 na Botswana 37.

6. Hoja kwamba Serikali imeshindwa usimamizi wa uchumi, Hapa nisiguse mapinduzi makubwa sekta za miundombinu, maji, Elimu na Afya..twende na ripoti za Tafiti tu;

# Mwaka 2017, kwa mara ya kwanza katika historia, ilifanyiwa uhakiki kuhusu uthabiti wa kiuchumi kuweza kukopesheka ( Credit rating), kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Moody's ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika kazi hizi( inamiliki asilimia 45% ya soko), ilitoa matokeo yake mwezi Machi2017, kuonesha kwamba Tanzania ina daraja la B1 juu ya Kenya, Uganda ambazo zilikuwa na B2. Ripoti hii ilizua mjadala mkali sana Kenya( Business Daily, 4th, March2017).

# Mwaka 2018, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu( Inclusive Economy) , na ya tatu kwa bara zima ikitanguliwa na Algeria na Tunisia( World Economic Forum 2018).Sikatai kwamba kuna mengi ya kufanyia kazi zaidi, lakini rekodi hizi ni kubwa na fahari kwetu kama Taifa kwamba tunakwenda vizuri katika maeneo mengi kuhusu ujenzi wa uchumi

# Mwaka 2017, IMF, iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa manne ya Afrika yanayoelekea safari ya Vietnam katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nchi zingine ni Nigeria, Kenya na Ethiopia. Rejea mahojiano ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF), Bi Christine Lagarde, alipohojiwa na Jarida la Quartz akiwa Addis nchini Ethiopia alipotembelea Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika( UN- Economic Commission for Africa).

7. Hoja za Mhe. Zitto kutaka watanzania wapoteze imani na Serikali kwa hoja za kuokoteza ni kupoteza muda. Tazama ripoti hizi;

# Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuwa nchi ya 96 kati ya nchi 186 duniani katika vigezo vya kupambana na rushwa. Mwaka 2015 kabla ya JPM, Tanzania ilikuwa ya 119.( Rejea Ripoti ya Transparency Internation 2019).

# Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuongoza Afrika katika nchi 35 zilizofanyiwa utafiti kuhusu imani ya wananchi kwa Serikali katika vita dhidi ya rushwa.( Transparency International, Global Corruption Barometer 2019 report).

# Ripoti hiyo hiyo ya kimataifa imeonesha kwamba asilimia 72% ya watanzania mwaka 2019 wanaamini kuwa Serikali yao inapambana na rushwa kulinganisha na asilimia 13% mwaka 2015.

8. Mapinduzi makubwa Sekta ya miundombinu na rasilimali watu yanaonekana bayana kwa kila mtanzania. Naamini kasi ya sasa ingekuwepo miaka 30 nyuma , ni wazi leo tungekuwa washindani wa Mataifa kama Vietnam.

Kwa mujibu wa Benk ya dunia,kufikia mwaka 1990, uchumi wa Tanzania ulikuwa dola 4.5bn nyuma ya Vietnam ikiwa na dola 6.5bn huku Kenya ikiwa mbele ya Vietnam kwa uchumi wa dola 8.4bn. Leo mwaka 2020, ikiwa ni miaka30, Uchumi wa Vietnam ni dola 260bn, ikiipita Kenya yenye dola bilion 90 na Tanzania dola 60bn.

# Ujenzi wa miradi mikubwa kimkakati kama Stirglers Gorge utakaozalisha umeme zaidi ya 2100MW na Ujenzi wa Reli ya kati ya sanjari na kufufua shirika la ndege ndio majibu kuelekea huko.

Nisisi watanzania tuliopiga kelele Serikali kumiliki ndege1 tena mbovu na wakati mwingine kukodi ndege kwa gharama kubwa kuliko gharama ya kununua ( CAG report 2015/16). Nisisi tuliopiga kelele reli iliyozeeka kutoka uwezo wa tani milioni 5 mpaka tani laki4.

Nisisi tuliopiga kelele kuhusu sekta ya umeme ilivyonyonga uchumi wetu kwa biashara za mitambo ya kukodi ambayo imekamua uchumi na kuacha nchi mifupa mitupu.

# Kinachofanyika sasa ndio safari kuelekea vietnam japo ilipaswa tuanze zamani.Mikopo kwa miradi ya kimkakati kama hii ina uhalali kulinganisha na tulikotoka ambapo tulikopa kulipa mishahara na kuendesha Serikali ( Recurrent Expenditure)

9. Hoja ya ujenzi wa rasilimali watu. Haihitaji miwani kuona mapinduzi makubwa haya. Sekta ya Elimu, Afya na Maji zimepiga hatua kubwa. Tafiti zinaonesha kwamba kila dola1 inayowekezwa kwenye maji inaokoa dola 4.2 ambazo zingewekezwa kwenye dawa ambazo ni matokeo ya tatizo la maji safi. Kuna mafanikio makubwa lakini changamoto za sekta hii kwa kiasi kikubwa ni miradi ya kurithi tulikotoka.

# Kuongeza mikopo elimu ya juu kutoka 360bn mwaka 2015 mpaka 450bn ni juhudi zilizo bayana. Kupeleka 23bn kila mwezi kuhakikisha Elimu- bure ni ndoto iliyogeuka kweli na kusababisha takribani watoto 1m waliokuwa wakikosa shule kila mwaka sasa wanasoma.Changamoto za ubora ni suala endelevu kuhakikisha tunazalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kuhimili ushindani wa soko la ajira.

#Aidha mapinduzi ya Sekta ya afya nayo ni bayana. Ripoti za NHIF zinaonesha mwamko mkubwa kwa watanzania kuwa na bima ya afya kutoka milioni 9 kabla ya awamu ya tano mpaka zaidi ya milioni16.

# Ongezeko la fedha za dawa na vifaa na tiba kutoka 31bn mwaka 2015 mpaka 269bn sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 700% ni mafanikio ya mfano.

# Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonesha kasi ya maambukizi ya malaria kushuka kutoka asilimia 14% mwaka 2015 mpaka asilimia7%.

Hii msingi wake pamoja na mambo mengine, ni ongezeko la upatikanaji dawa kiasi kwamba mtu mwenye malaria haimchukui muda mrefu kupona hata kuambukiza wengine kabla hajapata matibabu kutokana na ukaribu wa huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati mpaka Hospital ya Mkoa.

10. Nihitimishe kwa kurudia kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi.Thereza May na falsafa yake ya kuendesha Serikali inayozingatia maslahi ya wote ikiwemo wasio na sauti( Government works for all).

Alisema kwamba ni kiu ya waingereza kuona Serikali ya namna hiyo, lakini sio jambo jepesi kulitimiza kwa muda mfupi, linahusu kuyakabili maslahi ya wachache ambao kwa muda mrefu walifanya Serikali iendeshwe kwa maslahi yao. Naye aliyekuwa Rais wa Marekani JF. Kennedy alipata kusema kuwa Kiongozi bora ni yule anayesimamia maslahi ya Umma hata kama kwa kufanya hivyo atachukiwa na jamaa zake na hata makada wa chama chake.

Kifupi haya mawili ndio nayatazama kama mapito ya JPM. Anajenga msingi wa Taifa ambalo tuendako kijana hatokosa fursa ya elimu bora kwasababu ya umasikini wa wazazi wake, wala mama hatokosa huduma ya afya sababu ya umasikini wa familia yake au mume wake!

Kufumua na kusuka upya Taifa lilodumu kitambo katika uchumi wa 'missiontown' kuna changamoto nyingi ingawa tupo kwenye mstari sahihi!
 
Wakuu mliosoma hoja za tumbili naomba msaada amejibu nini kuhusu CAG kutokagua mifuko ya jamii( deni la sirikali), pamoja na miradi mikubwa kama SGR, bwawa la Nyerere na mengineyo!!
 
Good analysis first half kafulira 2 zito 0 ngoja tusubirie second half. Ukifuatilia comment yangu kwenye uzi ule nilisema zito anaweza kuwadanganya wale tu wasiokuwa na elimu ya uchumi make hoja zake zilikuwa za kuokoteleza mno.
 
Hoja kwa hoja, raundi ya kwanza Kafulila won, tusubiri comeback ya Zitto

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Zito ana Nini hapo unadhani..hana lolote. Na Wala hawezi kujibu mapigo hayo..Kaka na report ya kisaniisanii anadhani woote hawana akili..jinga Sana hili
 
Good analysis first half kafulira 2 zito 0 ngoja tusubirie second half. Ukifuatilia comment yangu kwenye uzi ule nilisema zito anaweza kuwadanganya wale tu wasiokuwa na elimu ya uchumi make hoja zake zilikuwa za kuokoteleza mno.

Mpe Kafulila 1000 Zitto 0. Lakini bado ukweli unabaki pale pale. Halafu muulize Bwana Tumbili: kwa kuwa serikali hii inakusanya kodi kiasi cha kuweka rekodi (wakati mwingine tunaambiwa duniani kote hakuna mfano wa serikali hii kwa kukusanya kodi na mapato mengine):

1. SGR kipande cha Dar - Morogoro kitakamilika lini? Kinachochelewesha leo kukamilika ni kipi? (Maana ilikuwa ikamilike Nov 2018).

2. Mradi mpya wa umeme umefikia hatua ipi hadi sasa?

3. Hospitali ngapi zenye ventilators Leo kukabiliana na ugonjwa wa Covid 19?

4. Tuliambiwa treni za kisasa za umeme na mabehewa yake vimeagizwa, vitakuja lini?
 
Alichofanya kafulila Ni kutetea ugali wake tu hana hoja, yaani riport ya CAG imeonyesha mapungufu makubwa sana ya serikali ya awamu ya tano, kwa mfano kutumia pesa bila kuingiza mfuko Mkuu Wa hazina unaiteteaje? Mapungufu Ni mengi sana.
 
ZITTO AJIBIWA KWA MIKWAJU 10 YA KAFULILA.👇soma iyo!

NATOFAUTIANA NA ZITTO KUHUSU RIPOTI ZA CAG NA MWENENDO WA UCHUMI

Na David Kafulila!
Aprili 12,2020-SONGWE

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W.Bush alipata kusema kwamba uongo ukirudiwa una nafasi ya kugeuka kuwa ukweli wa watu! Pengine ni sababu hiyo, pamoja na kupongeza uamuzi wa Mhe. Zitto Kabwe kama Kiongozi wa Chama Cha Upinzani kuchambua mwenendo wa awamu ya tano katika muktadha wa uchumi na utendaji kwa kurejea ripoti za CAG, napenda kutoa maoni yangu binafsi katika mafungu10 kutofautiana na uchambuzi wake kwa lengo la kuwekana sawa kwa faida yetu sote kama watanzania!

1.Hoja kwamba Serikali ya JPM imeshindwa kukusanya mapato kulinganisha na awamu ya nne ina matobo matatu;

# Kwanza Zitto ametoa ulinganisho wa miaka3 ya mwisho wa awamu ya nne na miaka 3 ya kwanza ya JPM kwa kutaja kiasi na asilimia ya makadirio( estimates)na makusanyo(actual collections)kwa upande wa awamu ya 5 lakini akaishia kutaja asilimia ya kutofikiwa lengo bila kutaja kiasi halisi kilichokusanywa katika miaka hiyo 3 ya mwisho wa awamu ya nne.Najua alivokuwa anakwepa!

#Zitto kafanya hivyo kwa makusudi kwasababu alijua kwamba kwa mujibu wa ripoti hizo za CAG, makusanyo ya miaka3 kamili ya mwisho ya awamu ya nne( 2012/13, 2013/14 na 2014/15) yalikuwa sawa na jumla ya TZS.28trilioni karibu sawa na makusanyo ya mwaka 1 tu wa 2017/18 chini ya JPM yaliyofikia TZS.27.7Trilion.

# Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba, makusanyo ya miaka ya 2012/13 (TZS.8Trilion), 2013/14( TZS.9.28Trilion.) , na Mwaka 2014/15 ( TZS.10.77Trilion) sawa na jumla ya (TZS.28Trilioni) ambayo ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwaka mmoja tu (2017/18) chini ya JPM.

Kifupi kulinganisha uwezo wa kukusanya kodi kati ya awamu ya4 na awamu ya 5 inahitaji kuwa na nia OVU kupotosha au chuki binafsi kwani hizo awamu mbili ni mlima na kichuguu katika eneo hilo.

# Kifupi makusanyo ya awamu ya nne kwa mwezi yalikuwa wastani wa TZS. 850bn, kiasi ambacho hakikutosha hata kumudu malipo ya deni la Taifa kwa mwezi na mshahara. Malipo ya deni kwa mwezi yalikuwa wastani wa 650bn, na Mshahara kwa mwezi ilikuwa wastani 550bn sawa na 1100bn. Hivyo ilibidi kukopa kuweza kumudu kulipa mshahara.

#Pengine ndio msingi wa kejeli za Rais Uhuru Kenyatta miaka hiyo kwamba ilikuwa Kenya peke yake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoweza kumudu kulipa mshahara watumishi wake bila kukopa.

Wastani wa makusanyo ya sasa ya kodi tu kwa mwezi yanatosha kumudu deni na mshahara na hivyo Serikali haikopi tena kulipa mshahara watumishi wake.

2. Hoja kwamba Serikali inakopa sana ndani na hivyo kuathiri fursa ya sekta binafsi. Hoja hii ina matobo ya aina mbili;

# Kwanza inafahamika sura ya deni la Taifa mpaka sasa asilimia 75% ni la nje na hivyo deni la ndani ni asilimia25%. Katika mazingira ya kawaida inashauriwa Serikali ikope zaidi ndani ili inapolipa fedha hiyo sehemu kubwa ibaki kwenye uchumi ndani badala ya kwenda nje.

# Pili,Serikali ingeathiri sekta binafsi kama ingekopa kwa riba kubwa kwani kwa kufanya hivyo ingesababisha riba za benki za biashara kwa sekta binafsi kupanda kwani moja ya kigezo cha kiwango cha riba za benki ni kiasi cha riba katika soko la hatifungani( TBs auctions).

Aidha Serikali ingekuwa inakopa kwa riba kubwa ingesababisha watu binafsi wenye ukwasi kukopesha zaidi Serikali kuliko kuweka bank au kuwekeza maeneo mengine ya uzalishaji.

#Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu kuhusu minada hiyo, Mwaka 2020, Serikali inakopa soko la ndani kwa riba isiozidi asilimia 5% kwa mikopo ya siku365 kulinganisha na riba ya silimia 17% mwaka 2015.

# Kutokana na Serikali kukopa soko la ndani kwa riba chini ya asilimia 5% kulinganisha na asilimia17% mwaka 2015, ni moja ya sababu ya riba za bank za biashara kushuka kutoka asilimia 24% mwaka 2015 mpaka asilimia 16%.

3. Hoja kwamba Serikali inaficha madeni ya mifuko ya hifadhi. Hii ina matobo ya aina tatu;

# Kwanza ni changamoto ya madeni yenyewe kwa namna yalivyopatikana. Sio siri kwamba kabla ya JPM, mifuko ya hifadhi iligeuzwa shamba la bibi na mali ya genge fulani.Huu ni ukweli unaothibitishwa na taarifa ya taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya E& Y ya Disemba2015, habari za uchunguzi za majarida makubwa ya kimataifa kama Africa Confidential na Africa Research Institute.

#Kwa mfano, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, mifuko ilikuwa ikidai jumla ya TZS 5.3Trilioni lakini baada ya ukaguzi deni halali likakutwa TZS.3.2Trilion sawa na deni hewa la zaidi ya TZS.2.1Trilion.

Sielewi Kiongozi anaesisitiza deni lilipwe kama lilivyo kama kweli ana mapenzi na watanzania walipa kodi? Hata kama hana mapenzi na walipa kodi wa nchi hii vema awe japo na huruma basi!

4. Hoja kwamba Serikali ya JPM ina kesi nyingi kwa kuvunja mikataba.
Hapa ni vema ikaeleweka kwamba;

# Kwanza kesi hizo ni matokeo ya mikataba mibovu ya zamani ambayo JPM amerithi kutokana na udhaifu mkubwa huko tulikotoka na sio mikataba ndani ya awamu ya tano

# Mfano, uamuzi wa Serikali kufuta mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion iliyorithi mitambo ya Dowans/ Richmond, imepunguza mzigo wa kinachoitwa tozo ya gharama ya uwekezaji ( capacity charges) kwa mwezi kutoka dola milioni 16.35( zaidi ya bilioni 37.6)mpaka dola milioni 9.75 ( sawa na bilioni 22.4) kwa mwezi( Rejea CAG report 2017).

Inahitaji ukatili sana kwa Taifa lako kumlalamikia JPM kufuta mikataba mibovu kama Symbion kwani kinachoitwa tozo ya ya gharama za uwekezaji ni mfano wa mbaya wa mikataba ya hovyo ambapo mwekezaji analipwa bila kujali amezalisha umeme au la eti kufidia gharama alizotumia kuwekeza.

# Vema kufahamu kwamba zama za Serikali kulipa madeni ya mikataba mibovu tumeshavuka. Huko tulikotoka Serikali iliwahi kulipa deni la Dowans kinyemela kiasi cha dola milioni 94 ( zaidi ya bilioni 200 wakati huo).Hakika inahitaji roho kutamani zama hizo, ni Taifa la 'wapumbavu' linaloweza kupigania Serikali yao ilipe madeni ya aina hii!

5. Kwamba Serikali ya JPM ni ya ufujaji! Labda nikubaliane kwamba vita dhidi ya Ufisadi ni endelevu duniani kote na inaendelea Tanzania. Hata hivyo inahitaji upofu kusema Serikali hii inatatizo hilo kuliko tulikotoka. Unaweza ukabaki peke yako kwani hali halisi na Tafiti zote kitaifa na kimataifa zinathibitisha mapinduzi makubwa eneo hili;

# Mwaka 2019, Serikali ya Tanzania ilitangazwa kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha za Umma( World Economic Forum,Executive Opinion Survey 2019).Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi za Kenya ilishika nafasi ya 70, Uganda 100, Ethiopia 48, Malawi 106, Msumbiji 118 , Ghana 61, Zambia 68 na Botswana 37.

6. Hoja kwamba Serikali imeshindwa usimamizi wa uchumi, Hapa nisiguse mapinduzi makubwa sekta za miundombinu, maji, Elimu na Afya..twende na ripoti za Tafiti tu;

# Mwaka 2017, kwa mara ya kwanza katika historia, ilifanyiwa uhakiki kuhusu uthabiti wa kiuchumi kuweza kukopesheka ( Credit rating), kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Moody's ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika kazi hizi( inamiliki asilimia 45% ya soko), ilitoa matokeo yake mwezi Machi2017, kuonesha kwamba Tanzania ina daraja la B1 juu ya Kenya, Uganda ambazo zilikuwa na B2. Ripoti hii ilizua mjadala mkali sana Kenya( Business Daily, 4th, March2017).

# Mwaka 2018, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu( Inclusive Economy) , na ya tatu kwa bara zima ikitanguliwa na Algeria na Tunisia( World Economic Forum 2018).Sikatai kwamba kuna mengi ya kufanyia kazi zaidi, lakini rekodi hizi ni kubwa na fahari kwetu kama Taifa kwamba tunakwenda vizuri katika maeneo mengi kuhusu ujenzi wa uchumi

# Mwaka 2017, IMF, iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa manne ya Afrika yanayoelekea safari ya Vietnam katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nchi zingine ni Nigeria, Kenya na Ethiopia. Rejea mahojiano ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF), Bi Christine Lagarde, alipohojiwa na Jarida la Quartz akiwa Addis nchini Ethiopia alipotembelea Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika( UN- Economic Commission for Africa).

7. Hoja za Mhe. Zitto kutaka watanzania wapoteze imani na Serikali kwa hoja za kuokoteza ni kupoteza muda. Tazama ripoti hizi;

# Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuwa nchi ya 96 kati ya nchi 186 duniani katika vigezo vya kupambana na rushwa. Mwaka 2015 kabla ya JPM, Tanzania ilikuwa ya 119.( Rejea Ripoti ya Transparency Internation 2019).

# Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuongoza Afrika katika nchi 35 zilizofanyiwa utafiti kuhusu imani ya wananchi kwa Serikali katika vita dhidi ya rushwa.( Transparency International, Global Corruption Barometer 2019 report).

# Ripoti hiyo hiyo ya kimataifa imeonesha kwamba asilimia 72% ya watanzania mwaka 2019 wanaamini kuwa Serikali yao inapambana na rushwa kulinganisha na asilimia 13% mwaka 2015.

8. Mapinduzi makubwa Sekta ya miundombinu na rasilimali watu yanaonekana bayana kwa kila mtanzania. Naamini kasi ya sasa ingekuwepo miaka 30 nyuma , ni wazi leo tungekuwa washindani wa Mataifa kama Vietnam.

Kwa mujibu wa Benk ya dunia,kufikia mwaka 1990, uchumi wa Tanzania ulikuwa dola 4.5bn nyuma ya Vietnam ikiwa na dola 6.5bn huku Kenya ikiwa mbele ya Vietnam kwa uchumi wa dola 8.4bn. Leo mwaka 2020, ikiwa ni miaka30, Uchumi wa Vietnam ni dola 260bn, ikiipita Kenya yenye dola bilion 90 na Tanzania dola 60bn.

# Ujenzi wa miradi mikubwa kimkakati kama Stirglers Gorge utakaozalisha umeme zaidi ya 2100MW na Ujenzi wa Reli ya kati ya sanjari na kufufua shirika la ndege ndio majibu kuelekea huko.

Nisisi watanzania tuliopiga kelele Serikali kumiliki ndege1 tena mbovu na wakati mwingine kukodi ndege kwa gharama kubwa kuliko gharama ya kununua ( CAG report 2015/16). Nisisi tuliopiga kelele reli iliyozeeka kutoka uwezo wa tani milioni 5 mpaka tani laki4.

Nisisi tuliopiga kelele kuhusu sekta ya umeme ilivyonyonga uchumi wetu kwa biashara za mitambo ya kukodi ambayo imekamua uchumi na kuacha nchi mifupa mitupu.

# Kinachofanyika sasa ndio safari kuelekea vietnam japo ilipaswa tuanze zamani.Mikopo kwa miradi ya kimkakati kama hii ina uhalali kulinganisha na tulikotoka ambapo tulikopa kulipa mishahara na kuendesha Serikali ( Recurrent Expenditure)

9. Hoja ya ujenzi wa rasilimali watu. Haihitaji miwani kuona mapinduzi makubwa haya. Sekta ya Elimu, Afya na Maji zimepiga hatua kubwa. Tafiti zinaonesha kwamba kila dola1 inayowekezwa kwenye maji inaokoa dola 4.2 ambazo zingewekezwa kwenye dawa ambazo ni matokeo ya tatizo la maji safi. Kuna mafanikio makubwa lakini changamoto za sekta hii kwa kiasi kikubwa ni miradi ya kurithi tulikotoka.

# Kuongeza mikopo elimu ya juu kutoka 360bn mwaka 2015 mpaka 450bn ni juhudi zilizo bayana. Kupeleka 23bn kila mwezi kuhakikisha Elimu- bure ni ndoto iliyogeuka kweli na kusababisha takribani watoto 1m waliokuwa wakikosa shule kila mwaka sasa wanasoma.Changamoto za ubora ni suala endelevu kuhakikisha tunazalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kuhimili ushindani wa soko la ajira.

#Aidha mapinduzi ya Sekta ya afya nayo ni bayana. Ripoti za NHIF zinaonesha mwamko mkubwa kwa watanzania kuwa na bima ya afya kutoka milioni 9 kabla ya awamu ya tano mpaka zaidi ya milioni16.

# Ongezeko la fedha za dawa na vifaa na tiba kutoka 31bn mwaka 2015 mpaka 269bn sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 700% ni mafanikio ya mfano.

# Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonesha kasi ya maambukizi ya malaria kushuka kutoka asilimia 14% mwaka 2015 mpaka asilimia7%.

Hii msingi wake pamoja na mambo mengine, ni ongezeko la upatikanaji dawa kiasi kwamba mtu mwenye malaria haimchukui muda mrefu kupona hata kuambukiza wengine kabla hajapata matibabu kutokana na ukaribu wa huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati mpaka Hospital ya Mkoa.

10. Nihitimishe kwa kurudia kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi.Thereza May na falsafa yake ya kuendesha Serikali inayozingatia maslahi ya wote ikiwemo wasio na sauti( Government works for all).

Alisema kwamba ni kiu ya waingereza kuona Serikali ya namna hiyo, lakini sio jambo jepesi kulitimiza kwa muda mfupi, linahusu kuyakabili maslahi ya wachache ambao kwa muda mrefu walifanya Serikali iendeshwe kwa maslahi yao. Naye aliyekuwa Rais wa Marekani JF. Kennedy alipata kusema kuwa Kiongozi bora ni yule anayesimamia maslahi ya Umma hata kama kwa kufanya hivyo atachukiwa na jamaa zake na hata makada wa chama chake.

Kifupi haya mawili ndio nayatazama kama mapito ya JPM. Anajenga msingi wa Taifa ambalo tuendako kijana hatokosa fursa ya elimu bora kwasababu ya umasikini wa wazazi wake, wala mama hatokosa huduma ya afya sababu ya umasikini wa familia yake au mume wake!

Kufumua na kusuka upya Taifa lilodumu kitambo katika uchumi wa 'missiontown' kuna changamoto nyingi ingawa tupo kwenye mstari sahihi!
Tumbili arudi Songwe tu akale mahindi. Zitto siyo saizi yake
 
Zito ana Nini hapo unadhani..hana lolote. Na Wala hawezi kujibu mapigo hayo..Kaka na report ya kisaniisanii anadhani woote hawana akili..jinga Sana hili
Kafulila anasema mwaka 2011/12 hadi 2013/14 Serikali ya Kikwete ilikusanya jumla ya Tshs.28t ambazo ni sawa na makusanyo ya mwaka mmoja tu wa Magufuli 2017/18. Lete huo ushahidi hapa kwamba mwaka huo zilikusanywa 28t, yaani bajeti ya mwaka huo ya Tshs. 31t zilipungua 3t pekee? Usipoleta huo ushahidi wewe ndo Kafulila kumbe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa wa Tanzania ni kama bendera fuata upepo! Ukimpa ulaji, atausifia mfumo mpaka utashangaa! Ukimnyima ulaji, atalalamika na kuponda mpaka basi.

Sina muda wa kuwaamini wanasiasa wachumia tumbo wa Tanzania. Siyo Zitto, siyo Kafulila, siyo nani! Wote wapo kimaslahi tu.
 
Back
Top Bottom