David Kafulila amkera Pinda

David Kafulila amkera Pinda

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2]Friday, November 9, 2012[/h]
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, kuacha kumshinikiza kutoa kauli bungeni zinazoweza kushughulikiwa na halmashauri yake.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kipindi cha maswali ya hapo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, baada ya Kafulila kuhoji utaratibu unaotumika wa kuwapa wawekezaji wa nje maeneo makubwa ya ardhi kuyamiliki huku wazawa wakikosa haki hiyo kama ilivyo katika mkoa wake.

Alimataka Waziri Mkuu kutoa kauli kwa kuwa Watanzania na nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ardhi ni alama ya ujamaa ambayo wanaweza kuishika kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

“Utaratibu wa kuacha ardhi mikononi mwa mabeberu na wananchi kunyang’anywa na watu wanaojiita wawekezaji…tunataka Waziri Mkuu utoe kauli,” alisema Kafulila.


Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema serikali inazingatia maslahi ya wananchi wake na kwamba hakuna kitakachofanyika katika ugawaji wa ardhi bila halmashauri husika.


“Hili jambo kwanza mngelizungumza katika halmashauri ya Kasulu kabla ya kulileta hapa kama likishindika ndio muishauri serikali ili tufanyekaze kwa pamoja,” alisema.


Pinda alimshauri Kafulila akiwa sehemu ya baraza la madiwani kulishughulikia suala hilo kwenye halmashauri kwa kuwa liko ndani ya uwezo wa halmashauri yao.


“Kafulila amekiri kwamba jambo hilo limepita kwenye halmashauri yake. Mashinikizo yasiyo na msingi, mambo yamefanyika kwenye halmashauri yenu halafu unakuja kunikoromea hapa na kunishinikiza nitoe kauli nenda kaongee na halmashauri yako,” alisema Pinda huku akiokenaka kukerwa na shinikizo la mbunge huyo.


Hata hivyo, alisema kama kuna watu wanataka kuwekeza kwenye ardhi kwa ajili ya kuiendeleza, haoni kama ni dhambi na kutaka wawekezaji wasikatishwe tamaa.


Katika swali lake la nyongeza, Kafulila alimwambia Waziri Mkuu kuwa yeye anaona wawekezaji kupewa ardhi ni dhambi na kuhoji utaratibu uliotumika kutoa hekta 10,000 na ekari 25,000 za ardhi kwa mwekezaji wa Agroso na Felisa.





CHANZO: NIPASHE






 
Tatizo CCM na SERIKALI yake waligawa ARDHi ya Watanganyika kama NJUGU; Sasa Waliopewa Wengine ni VITAPELI; Investor-UCHWARA...

Waziri Mkuu anaulizwa swali; Sababu alishangilia sana hao INVESTORs yeye na RAIS... ANACHUKIA UKWELI!!!
 
Pinda siku hizi ananiudhi sana, ana majibu mabaya sana Bungeni.Bado hajajifunza toka kwa maswali ya akina Mbowe?Kaona wapi Rais anaulizwa kitu anasema ulipaswa pitia chini,wakati anajua hakuna sheria inakataza entry point yoyoye ya kudai haki.Sasa speaker wa Bunge kwanini asimwambie Pinda swali limeshanfikia na anapaswa tolea majibu.Kama walihisi Halamshauri ndizo zinahusika kwa nini asiwasiliane nao ?
 
Hata hivyo title ya thread haistahili kubeba uzito uliomo kwenye habari hii.
 
Back
Top Bottom