David Haye amuita Klitscho "laghai" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

David Haye amuita Klitscho "laghai"

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, May 20, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  101222064234_klitschko_haye_386x217_ap_nocredit.jpg

  David Haye amembandika jina la "laghai" Wladimir Klitschko katika mkutano na waandishi wa habari mjini Hamburg wakati wa mchakato wa kutangaza pambano lao la ubingwa wa dunia wa kuunganisha mataji.

  Haye Muingereza anayeshikilia mkanda wa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na WBA, atakabiliana na Klitscho raia wa Ukraine bingwa dunia wa uzito wa juu unaotambuliwa na IBF na WBO katika ukumbi wa Imtech Arena tarehe 2 mwezi wa Julai.

  "Nimeona mtindo wake na kushuhudia anavyofanya ulingoni ni laghai tu," alisema Haye mwenye umri wa miaka 30.

  Haye awali alipangiwa kupambana na Klitschko mwezi wa Juni mwaka 2009, alilazimika kujitoa baada ya kuumia, lakini Muingereza huyo ameongeza "miungu wa masumbwi wameamua tarehe 2 Julai ndiyo nitatawazwa kuwa bingwa wa dunia kwa kuunganisha mikanda yote mitatu".

  "Nimeaangalia macho ya Klitschko kwa dakika 20 na nimegundua nitamuangamiza," aliongeza Haye, ambaye ameshashinda mapambano 25 kati ya 26.

  "Nimetazama macho yake kwa makini na nimemuona amekwishapigika na kuvunjika moyo. Hajawahi kupigana na bondia yeyote mwenye uwezo kama wangu, hili ni jimbo jipya kwangu na kwake.

  "Atafanya kile anachokifanya mara zote. Nimekwishapigana na watu wa aina hii, akimuita mpinzani wake 'robots' siku za nyuma- Hwajawahi kunipiga katika kiwango cha ngumi za ridhaa ama za kulipwa, kutoka mabondia wa Ulaya mashariki na hilo halitabadilika kamwe, aliendelea kujigamba Haye.

  "Ana ngumi kali, nimekwishashuhudia akiwaumiza watu na ngumi hiyo, lakini siamini kama pambano letu litafika hadi raundi ya 12.

  Akizidisha majigambo Haye alisema alikwenda Paris na akafanikiwa kumchapa bingwa wa uzito wa cruiser Jean Marc Mormeck, akaenda Ujerumani akamtandika bondia mwenye umbo kubwa Nikolay Valuev, ambaye amesema Wladimir na kaka yake Vitali wamekuwa wakimkwepa kwa miaka kadha.

  Akijibu tambo hizo za maneno, Klitschko, mwenye umri wa miaka 35, alitaka kushikana mkono na Haye lakini Muingereza huyo akakataa na Klitscho akaahidi "atamfunza somo la adabu" Haye tarehe 2 Julai.

  "Ninamuheshimu sana, ni bondia hodari akiwa na rekodi nzuri," alisema Klitschko. "Ana makonde mazito na kasi kubwa pamoja na hamasa na safari hii mvuke unatoka katika masikio yake kwa sababu ana hasira na nadhani nitatawala ulingo.

  Klitscho aliongeza:"Nitahakikisha najiandaa ipasavyo kwa pambano hili. David Haye atakuwa mtu wangu wa 50 kwenda chini kwa knockout. Mabondia 49 tayari walisalimu amri kwa knockout katika miaka 15 iliyopita na David Haye amewavunjia heshima wote hao.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Huyu haye mdomo saana....

  Na atadundwa very badly......
  We muache tu...
   
 3. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 613
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  makonde yataongea julai 2.....wapenzi wa masumbwi tusitegemee kuona matokeo ya kushangaza kwani klitschos brothers wataendelea kutawala ulimwengu wa masumbwi mpaka watapoamua kustaafu...haye kwa style ya upiganaji wake wa kukimbia kimbia na ngumi zake za sungura "rabbit shots" kama alivyofanya kwa valuev asitegemee kushinda!kwa maneno yeye mshindi ila masumbwi hapana!...katika medani hii mtu nilikuwa nikimtegemea kuleta ushindani k brothers alikuwa solis peke yake!
   
Loading...