Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Harakati za kumsaka mahali alipo kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, Mdude Nyagali zimeendelea kushika kasi. Makada na viongozi wa Chadema wameendelea kuweka kambi kwenye ofisi za chama hicho, sasa wametangaza dau la Sh10 milioni kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alitangaza dau la Sh5 milioni kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa kada huyo ambaye leo imetimia siku nane bila kujulikana mahali alipo.
Mdude alitoweka nyumbani kwake eneo la Iwambi, jijini Mbeya, baada ya kuvamiwa, kupigwa na watu waliodaiwa kujitambulisha kama askari. Tangu tukio hilo, hatima yake haijajulikana, hali iliyozua sintofahamu na hofu miongoni mwa wanachama na familia yake.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa, Mei 9, 2025, Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Hamad Mbeyale, alisema dau hilo limetokana na michango ya wadau wa ndani na nje ya nchi, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wanapata taarifa kuhusu alipo Mdude – akiwa hai au amefariki.
“Dau hilo ni kuhakikisha tunapata taarifa za uwepo wa Mdude Nyagali awe amekufa au hai,” amesema Mbeyale.
Mbali na kutangaza dau hilo, Mbeyale pia alilitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu madai kwamba, linamshikilia Mdude.
Pia soma
Pre GE2025 - RC Mbeya atoa TSh 5 Milioni kwa atakayetoa taarifa za Mdude, aagiza Polisi kuwasaka waliomteka