Ni kweli kabisa AshaDii NA SABABU NI HIZI HAPA
miaka 5 ya kwanza ya ndoa inachangamoto sana, manake mnakuwa hamjajuana kivile kwahiyo kila hupelekea wapendanao kuona kuwa mwenzie anaboa.
miaka 10 ndiyo miaka inayopita mkiwa mnatafuta maisha yaaani mnajenga, huku mnazaa na isitoshe pia ndugu wanawatizama.
ndani ya miaka hii pia kwasababu ya ulezi wa watoto waogo wenzetu wababa wengine wanakuwa siyo wavumilivu. kwahiyo kama usipokuwa makini wewe mama unaweza kumpoteza kabisa baba. manake unamnyonyesha mtoto huku unatakiwa umnyonyeshe baba.
ndani ya miaka hii ndio wale wapinzani wako hasa ndugu wanajiinua sana na hawa huwa ni mwiba mkali nani ya ndoa. ila ukiwapuuzia tu umewashnda, kwani baada ya 10 yrs mnakuwa sasa wewe baba na mama mmeshajuana vizur hivyo hata mtu aseme nini haliwapi shida.
Lakini pia Asha wanaume huwa wanabadilika kurudia ujana unapomaliza majukum ya kujenga na kuzaa na kama hajafikisha miaka 45 na siyo mwaminifu basi lazima atacheat tu. ila akifikisha umri huo wa 45 basi hurudi tena nyumbani kwa nidhamu. yapo mengi nitakuandikia baadae.