Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Huyu jamaa kiukweli nilikuwa nasikia tu jina lake na ni msanii wa rap ila kama ingetokea tukapishana wala simjui kama ambavyo hanijui. Hata ungeniambia kaimba wimbo upi ningeshindwa kukutajia. Nawafahamu kina Godzilla, FA, Fid Q, etc. Sasa kama ilivyo kwa wengine naona nyota ya Jaha imemdondokea huyu msanii. Niliufahamu wimbo kupitia ile clip ya wale jamaa waliopagawa hadi kuachia usukani. Baada ya hapo nikaanza kumsikia kwenye vyombo vya habari. Nikasiliza na wimbo wake ila bado sikuona kipya.
Sasa ikawa kila nakopita nausikia huu wimbo. Boda boda, redio na tv, kwenye biashara za watu. kwenye simu za watu, n.k. Kiukweli nami taratibu nikaona unaanza kuniteka. Nikaupenda. Umekuwa wimbo wa taifa. nilipita duka moja kuna jamaa alikuwa kauweka huu wimbo na unajirudia rudia. Kwa muda niliopita pale ni kuwa ulishajirudia kama mara kumi hivi.
sasa baada ya kipindi hiki cha mpito we jamaa utafanyaje ukae hapo juu? Kwa sasa usichekelee sana. Anza kujiuliza utafanya nini? Kama ni matatizo basi ndio hayo umejitakia. Jipange tena