Asante Kdany kwa kuonesha nia ya kutoa maarifa ya ujuzi kwa vijana wenzako ambapo na wewe unajipatia ujira kidogo.
Binafsi nimekuwa nikisaka kila kona mafunzo ya aina yoyote ya ujuzi wa kuzalisha bidhaa aina yoyote ambayo itanisaidia kuongeza kipato changu.
Katika taarifa yako, kitu kilichonivutia ni utengenezaji wa sabuni ya kipande mche na maji. Natamani kujifunza vitu hivi. Swali je naweza kumudu gharama za vitendea kazi na kutengeneza bidhaa zitakazoingia sokoni kwa ushindani?
Je mafunzo hayo yanachukua muda gani?
Kwa sasa mimi nina biashara ya genge (nyanya,vitunguu,chumvi na vinginevyo...)