Darasa la Saba kuongoza Bunge na wizara 2015

Darasa la Saba kuongoza Bunge na wizara 2015

Bukya

Senior Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
196
Reaction score
121
DARASA LA SABA KUONGOZA BUNGE NA WIZARA TANZANIA 2015.

Na Onyango George

Tanzania ni Nchi ambayo inakuwa na kubadilika kiuchumi, kisiasa, kijamii na kitamaduni. Kijamii tumepiga hatua kubwa tangu Uhuru hadi leo. Wakati wa Uhuru, Tanzania ilikuwa na Chuo Kikuu kimoja tu (Chuo kikuu cha Dar es salaam) na baadhi ya Shule chache za Sekondari. Uchache wa shule na vyuo ulisababisha wasomi kuwa wachachae sana ukilinganisha na idadi ya watu. Hali hii ilisababisha hata ofisi nyeti za Serikali kuongozwa na wenye elimu ndogo, yaani wenye elimu ya Shule ya msingi.

Uhaba huu wa wasomi ulisababisha kulegeza masharti na sifa ya kugombea Ubunge, kuwa ni Mtanzania asiye na elimu, ila tu awe anaweza kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza. Sifa hii inatolewa na ibara ya 67(a) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara.

Na hapa nanukuu "pamoja na maelezo mengine katika ibara hii mtu yeyote atakuwa na sifa ya kuwa Mbunge …… kama ni raia wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwenye umri wa miaka 21, ambaye anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza" mwisho wa kunukuu (Tafsiri kutoka kiingereza kwenda Kiswahili ni ya kwangu).

Lengo langu ni hii sifa ya kujua kuandika na kusoma lugha ya Kiswahili au kiingereza. Naomba ifahamike kuwa hata ambaye hajakanyaga shule ya chekechea anaweza kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza, kwa kuwa hizi ni lugha tu kama vile Kijaluo, kimanda au kiha.

Kwakuwa ni haki ya kikatiba kugombea Ubunge ukiwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika tu, nilifundishwa na Mwalimu wangu wa hesabu ( Hisabati) juu ya "probability", kuwa ukirusha shilingi kuna uwezekano wa upande wa kichwa au mwenge kutokea. Kwa maana hiyo ninaona kuwa kunauwezekano mkubwa tu wa wabunge wenye elimu ya darasa la saba au ambao hawaja kanyaga shule ilimradi wanauwezo wa kusoma na kuandika Kiswahili kuongozwa Bunge na Wizara za Tanzania mwaka 2015. Na ikitokea hivyo basi hawawezi kukabili changamoto za ulimwengu wa leo unaongozwa na wasomi pamoja na wanataaluma wa hali ya juu. Kwa kuwa ibara ya 55(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyo fanyiwa marekebisho mara kwa mara inampa rais uwezo wa kuteua mawaziri kutoka kwa Wabunge, basi wabunge wakiwa na elimu ya darasa la saba hata na mawaziri watakuwa hao hao mambumbumbu kitaaluma.

Ninaamini kuwa hawa wasio na elimu watachaguliwa kuwa wabunge kwasababu kwanza wenye kujua kusoma na kuandika Kiswahili ni wengi Tanzania, pili kulingana na chaguzi zetu zinagubikwa na tuhuma za rushwa kuna uwezekano mkubwa wa wenye pesa kuchaguliwa na kuwa na pesa haiangalii elimu ya mtu. Hata katika Bunge la sasa na amini kuna idadi kubwa tu ya darasa la saba, mfano mzuri ni Mbunge Fulani aliyejitangaza wazi wakati wa Kapeni za uchaguzi wa mwaka 2010 na kwa bahati nzuri yeye ndiye aliyeshinda.

Ni kweli kwamba wakati kifungu hiki kilipotungwa wasomi walikuwa wachache kiasi kuwa kuna baadhi ya majimbo ilikuwa ni vigumu kupata wenye elimu ys Sekondari. Lakini kwa sasa wasomi ni wengi Tanzania karibia kila kata kuna wahitimu wa shahada mbalimbali, na kama hawapo basi kuna wahitimu wa kidato cha nne. Zingatia shule za sekondari zipo karibia katika kila kata zote za Tanzania.

Wala siyo nia yangu kulinganisha Tanzania na nchi nyingine katika sifa za kuchagua mbunge na siamini, kuwa mabadiliko mpaka yaanze kwa jirani ila naamini kubadilika ni kwasababu muda wa mabadilko umefika, na kwa Tanzania muda huo ulishafika lakini hawataki kubadilika. Katiba yetu imefanyiwa marekebisho mara kwa mara, lakini ibara hii ya 67(a) inaachwa kama ilivyo sijui kwa sababu Wabunge ambao ni wahusika ndiyo wanafanya marekebisho haya au la.

Ninafahamu na kutambua haki za binadamu, na hata haki ya mtu kuwa kiongozi katika nchi yake. Kila mtu ana haki ya kikatiba yakuwa kiongozi lakini lazima tuangalie ni nafasi gani mtu anaweza kuongoza kulinga na elimu yake. Vilevile sisemi kuwa darasa la saba hana busara na hekima ya kutawala la hasha bila kujali elimu, hata wapo wasomi ambao pamoja na usomi wao hawawezi uongozi, lakini kulingana na changamoto za kukua kielimu na taaluma mbalimbali basi tunahitaji wabunge wenye hekima, busara na elimu.

Tunataka wabunge wasomi kutokana na unyeti wa nafasi na kazi zao. Kwanza kutokana na Wabunge ndiyo mawaziri hupatikana, na hawa mawaziri ndiyo hutekeleza shughuli za Serikali ndani na nje ya nchi. Hivyo tunapaswa kuwa na mawaziri wenye uwezo wa kielmu wanaoweza kuingiliana hata na wenzao wa nchi tofauti, na kuweza kuongoza hata wasomi na wasio wasomi wa hapa nchini. Pili kwa kuwa wabunge ndiyo watunga sheria za nchi, leo Mbunge asiye na elimu ndiye umpe kazi ya kitaaluma kama hii, hivi tutakuwa na sheria za namna gani? Kama si sheria zenye "lacunas".

Pamoja na hayo, hao hao wabunge shughuli ya kukagua na kudhibiti kazi za serikali. Kazi hii hufanywa kupitia kamati za kudumu za bunge. Sasa leo hivi mbunge asiye na elimu amkague mtendaji wa Serikali ambaye sifa yake ya ajira ilikuwa ni elimu ya juu, Je inawezekana kweli? Na hata katika bunge la sasa sina uhakika kama wenye elimu ya darasa la saba wanaongoza kamati hizi, kama hawaongozi ni kwanini?

Kazi nyingine muhimu ni kupitisha bajeti ya Seerikali, bajeti ambayo huaandaliwa kwa ufundi mkubwa wa kitaaluma na wasomi. Naomba ieleweke kuwa kujua kusoma na kuandika siyo kujua mahesabu ya "simultaneous equation"au "quadratics". Kwa hiyo hawawezi kujadili taarifa ya bajeti ya serikali hivyo kupitisha bila kujali athari yake.

Tofauti na hayo bunge hutatua migogoro mbalimbali ndani na nje ya nchi. Chukulia mfano wa mgogoro wa ununuzi wa rada nchini Uingereza, yawezekana kamati iliyoundwa na bunge haikuongozwa na darasa la saba na ni kwanini? Hii inaonesha kuwa muda wa wabunge wanaojua kusoma na kuandika kiswahili imepitwa na wakati. Na kama haujaamini futilia wabunge walioomba nafasi kuchaguliwa kuwa wabunge wa Afrika mashariki na bunge la Afrika kama kuna aliye na sifa ya kujua kusoma na kundika tu. Na kama hakuna ni kwanini? Kwa kifupi naomba niishie hapa kwa kuishauri Serikali ya Tanzania kuwa muda ni muafaka kwa kufanya mabadiliko makubwa kutoka katika bunge la wenye kujua kusoma na kuandika Kiswahili au kiingereza na kuwa na bunge la wasomi.

Kama hata idara ya mawasiliano wanafanya mabadiliko kutoka "analogy" kwenda "digital" kwanini isiwe bunge ambalo ni miongoni mwa mihimili mikuu ya Serikali? Mbona mihimili mingine ili kupata kazi kuna kigezo cha sifa ya elimu? Mfano Mahakamani hauwezi kupata kazi eti unajua kusoma na kuandika Kiswahili, hata kwenye Serikali mtendaji wa kijiji sharti awe na elimu ya kidato cha nne. Basi na bunge nalo angalau mbunge awe na elimu ya kidato cha sita kama siyo shahada ya kwanza.

Chanzo: Ruco Mirror, July 2012
 
Siasa ni kipaji, mtu anazaliwa nacho, hakisomewi popote, elimu yetu ni kukariri, nyie nyie ndio mnaoilaum elimu haimuandai mtu kukabiliana na maisha ya kawaida, mtu akisoma akikosa ajira kwisha habari yake, leo hii unaoiona inafaa tena,

Watu wana uwezo wao vipaji vyao, waache wagombee
 
Bora la saba na wasanii ndio wawe wabunge,sema wasomi walio katika bunge na kwenye wizara wanafanya nini,zaidi ya kutuingiza katika mikataba isiyo eleweka,kujilikimbizia mali,kutanguliza siasa hata mahali pasipohitaji siasa.mimi naona kiongozi poa tu ata akiwa la saba mradi atapokea ushauri toka kwa wataalamu walopewa kazi kuliko hawa wachumia tumbo wanoingilia maswala ya wataalamu.Nnch hii bora bungeni tuwajaze wasanii kuliko hao wasomi walogeuza bunge kuwa sehemu ya mipasho.kupinga vitu vya msingi kisa wanatetea vyama vyao ,watu waloshindwa kuheshimu taaluma zao na kutaka kutwangana hadharani,wanaotaka posho kubwa wakati shule hazina madawati ya kutosha.bora la saba wataokuwa na uchungu wa nnchi hii.
 
Kwa kuwa wabunge ndiyo watunga sheria za nchi, leo Mbunge asiye na elimu ndiye umpe kazi ya kitaaluma kama hii, hivi tutakuwa na sheria za namna gani?
 
Back
Top Bottom