Darasa la mahusiano na mapenzi ! Changia chochote unachoamini itasaidia kujenga mahusiano mazuri !

PowerWithin

JF-Expert Member
Mar 8, 2014
646
501
Naona thredi nyingi sana wadau wake kwa waume wakilalamika kuhusu mahusiano. Sasa twendeni taratibu tupeane uzoefu wa haya mambo ya mahusiano.

Mimi ninaanza kama hv:

Kwa wanawake na wanaume:

Sharti la kwanza:
Fahamu dreams za mpenzi wako kinagaubaga.

Dreams zake ndo maisha yake. Ndio utamaduni wake. Ndicho anachopenda kusikia. Ndicho anachopenda kuongelea. Jitahidi kuwa sapoti kubwa katika eneo hilo.

Kuna uzi humu mdau RRONDO kauweka ikidai wanawake have nothing else to offer to men more than sex. Huo uzi kwa mwanamke ni fikirishi sana. Hata kwa wanaume inatufikirishi kwamba kama ni kweli Je kuna haja gani ya kugharamika kwa wanawake kwa ajili ya sex pekee? Inafikirisha.
 
Tunaendelea na sharti la kwanza hapo juu:

Kuna mtu humu hajawahi kusoma darasa la kwanza hadi la saba? Hakuna.

Sasa sikia. Jikumbushe kipindi kile wale vipanga wa darasa lako walivyokuwa na mvuto kwa wenzao darasani wake kwa waume. Unadhani sababu ni nini? Ni kwa sababu wale vipanga wana mchango muhimu na mkubwa sana katima kufanikisha ndoto za hao wenzao japo kimasomo.

Mahusiano nayo yapo hivyo hivyo yaani principle ni hiyo hiyo.
 
Sharti la pili:

Dhamani yako.

Sikia hii hapa. Unamfahamu Bacary sagna yule mchezaji wa zamani wa Arsenal. Unamjua demu wake? Bacary ni mweusi balaa yaani anatisha jamaa ni kama usiku ni zaidi ya lami kwa weusi. Ila ana demu kisu si mchezo. Mweupe peeee. Nadhani unafahamu ubaguzi wa wazungu kwa watu weusi.

Achana na Bacary. Twende kwa Super Mario yaani Mario Baloteli. Huyu jamaa ni mwehu ni mwehu hv fulani, lakini pamoja na hayo ana demu wakali wa kizungu si mchezo.

Unadhani siri ni nini? Dhamani yake. Yaani mafanikio yake.

Mahusiano yanafuata principle hii hii. Kuzaliwa handsome ama beautiful ni one thing lakini kujenga dhamani yako yaani kuwa na mafanikio ni another extra ordinary thing.

Kwani dhamani ya mtu ni nini? Ni mafanikio. Kipimo cha mafanikio ni nini? Ni Uwezo wa kukabili na kutatua changamoto za kimaisha hasa eneo la elimu, uchumi, afya, imani na upendo. Sitajata pesa hapo. Hahahahahaha. Assume una pesa lakini huna upendo, au una pesa lakini huna imani ya Ki Mungu, ama una pesa lakini huna afya njema, au una pesa lakini hata familia yako hawapati elimu bora. Japo bila shaka SI Unit ya mafanikio kwa watu wengi ni pesa.

Fikiri hv. Kama una mafanikio na wadau wanakupenda maana yake wanapenda mafanikio yako na sio wewe kama wewe. Ama fanya hv wewe ni mkuu wa kitengo fulani na unaheshimika sana ukiwa bado kwenye hio nafasi, lakini ukishatoka ndio basi tena heshima hio hutoweka na kubaki kwa anayeshika hio nafasi yako. Na hio ndo dhamani yako. Maintain it.
 
Ninachoamini mapenzi hayana formula,unaweza kuwa mvumilivu mwenzako anakuona boya tu,ukiongea unakua Padua kichwa,ukiwa mpole unaonekana pia lofa mwenzio anachukulia advantage. So,mapenzi ni mioyo kusemezana na kushibana
Hahha kabisa asee.... mapenzi sio ya kujipa moyo kabisa, ka unapenda penda at yor own risk
 
Sharti la tatu:

Mchango wako katika kuziba weakness ya mwenzako.

Hakuna mtu aliyekamilika. Watu wengi smart wanajua pahali wana mapungufu makubwa na madogo. Sasa alichofanya Mungu ni kumuumba mwanamme asiyekamilika na mwanamke asiyekamilika pia. Ni kama bolt na nut somehow yaani hamna mtu screw, ni aidha mmoja ni nut na mwingine ni bolt!

Sasa unapoingia kwenye mahusiano, ni wajibu wa kila mmoja kubaini wapi weakness za mwenzake na uwezo wake wa kuzi cover.

Tuongee kibiblia hv. Kuna mtu alpha na kuna mtu omega, yaani mtu mzuri sana wa kuanzisha jambo lakini si mzuri wa kuliendeleza ama mzuri wa kuliendeleza lakini si mzuri wa kulianzisha. Sasa hawa watu wanapokutana kwenye mahusiano automatically wanajikuta wanajifit. Hizi kama karma hv.
 
Note Bein:

Other things remain constant (ceteris peribus). Mfano suala la usafi kwa wapendao, uaminifu, sex drive ama sexual satisfaction, na kuendelea
 
Back
Top Bottom