Habarini Ndugu Wanajf
Baada Ya Uzi Wa Wa Biashara Ya Ufundi Simu Na Laptop
Habari Zenu Wakuu, Natumaini Leo Mko Vyema. Lengo La Nyuzi Hii Ni Kupeana Ushauri, Maoni Na Mbinu Za Uthubutu Katika Biashara Ya Ufundi Simu Na Laptop Kwanza Mimi Ni Mmoja Wa Mafundi Waliojifunza Na Ku Master Phone And Laptop Repair Kutoka Google Na Youtube, Yaani Self Made Technician...
www.jamiiforums.com
Nilipata Jumbe Nyingi Sana Kila Mtu Akihitaji Mwanga Wa Kujifunza Hii Kitu
Nikaona Sio Mbaya Kama Tutaanzisha Darasa La Laptop Repair Humu At Least Vipindi Vitatu Kwa Kila Wiki.
Tutajifunza Katika Njia Ya Maelezo Kwa Kiswahili, Picha Na Discussion Na Supportive Link Kama Zitahitajika.
Darasa Litakuwa Na Part Mbili
Part 1
(Hapa Tutajifunza Softwares Tu, Mfano: OS Zote Za Windows, Recovery, Tech Tools, Forensic Tools, Recovery Tools, Partition Wizards, Drivers Installations And Troubleshooting, Wireless Network Troubeshooting Na Vinginevyo)
Part 2
(Hapa Tutajifunza Laptop Hardware Tu, Na Kwangu Hii Ndio Most Paid Job Kwenye Laptop Repair, Tutajifunza Kuhusu Laptop Assembly and Disassembly, Identification Of Laptop Hardware Components, General Power Rails Of Laptop, Power Signals, Chipset Level And Behaviours, Tools And Component For Laptop Motherboard Repair, Matatizo Mbali Mbali Ya Laptop Na Utatuz Wake Upande Wa Hardware Na Vinginevyo)
Tutakuwa Na Vipindi Vitatu Vitatu Kwa Kila Part Ya Somo
J3, J5 Na Jmosi.
Vitu Vya Kuzingatia
1. Tujitahid Kutumia Lugha Za Kistaarabu Kueleweshana
2. Kama Kuna Mahali Haujaelewa Uliza Tu Utajibiwa Hata Mara 100
3. Mafunzo Ya Haya Ni Bure Na Hayana Malipo Yoyote, Malipo Ni Likes Na Baraka Zako.
Tukutane Jmosi Kwa Part 1 Ya Software Na Hardware.
Wasalaam.