RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 54,833
- 119,882
Naomba mnisome kwa umakini,maanake bila hivyo hamtanielewa, na ambae hujawahi kuendesha kwenye Motorways,Autobhan unaweza usinielewe kabisa.
Ni hivi exits za hili daraja ni za kimagumashi na ni hatari sana kwa madereva. Kwa mfano unatoka chuo cha uhasibu/uwanja wa taifa unataka kuingia daraja la Kigamboni exit iko kulia! Na kabla ya exit hio unakutana na magari yanayotoka darajani yanaingia hapo hapo kulia! Hii ni hatari sana na haikutakiwa kuwa hivi.
Mimi sio mhandisi wa barabara lakini kwa kutembea na kuendesha hapa na pale nimeona 'exits' za motorways na flyovers nyingi sana. Kwa sisi tunaoendeshea upande wa kushoto exits inatakiwa iwe kushoto, yaani ukitokea uhasibu/uwanja wa taifa na unataka kwenda daraja la kigamboni ilitakiwa uchepukie kushoto ambapo kulitakiwa kuwe na flyover ambayo ingekufanya uingie kwenye daraja kushoto bila kusumbua magari yanayoendelea kuelekea bandarini.
Tuangalie ukiwa unatoka kigamboni kuelekea bandarini[kuna kibao]. Wamejenga flyover ambayo inaenda kuingia kulia mwa barabara inayoenda bandarini, kwahio ukifika pale inabidi usimame uangalie magari ndio uingie! Hii ni hatari na italeta foleni kama si ajali. Kilichotakiwa hapo hio flyover iruke hio barabara kabisa na ikaungane nayo kwa kuingia kushoto kwake.
Ukitoka Kigamboni kwenda uhasibu au uwanja wa taifa exit iko perfect kabisa. Ninachokiona hapa wakandarasi wamekwepa jukumu la kujenga flyover mbili muhimu na kutumia shortcut. Kwa maoni yangu ni hatari kwa watumiaji wa hii barabara/daraja.
Angalia hio exit kutoka darajani kuingia barabara inayokwenda bandarini imeingilia kulia ambapo magari ya kwenda kigamboni yana exit katika umbali mdogo sana. Ni hatari sana kwanini hizo flyovers hazikuruka hio barabara kabisa?
Angalia mstari wa kijani na mwekundu.