DAR: Utaratibu mbovu wa zoezi la uhakiki wa TIN, foleni bado ndefu

MduduWashawasha

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
1,653
603
Wadau

Pamoja na kuwa leo ni siku ya mwisho na nikikiri kwamba sijahakiki TIN number yangu, nichukue nafasi kueleza kutorodhishwa na namna zoezi hili lilivyoendeshwa.

Kikubwa hapa ni namna gani hasa sisi waajiriwa tutajigawa katika ya muda wa mwajiri na muda usiojulikana ambao utapaswa kushinda ofisi za TRA ukihakiki TIN number yako.

Kwanini kusingekuwa na namna ya kupanga muda maalum kwa makundi flani ya watu au tudownload au kujaza fomu za uhakiki katika tovuti ya TRA na kuzituma kwao tukichangua na kituo kitakachotumika kufanyia zoezi hilo.

Then TRA wanapanga muda na mhusika unajua kwamba tarehe flani saa flani nitapaswa kwenda kuhakiki TIN yangu.

Mtu ni daktari au muongoza ndege utoke tu uende ukashinde ofisi ya TRA masaa manne.Kazi unamwachia nani ?

HALI ILIVYO LEO:

TRA Ilala wanawalazimisha watu kununua form za uhakiki kwa sh 500, Kuna stationary pembeni ndio imepewa tenda zoezi la uhakiki linaishia leo kwa mujibu wa matangazo lakini Hata watu wa siku 3 zilizopita bado hawajafanyiwa uhakiki wa tin namba zao. Watu walio katika foleni ni wale wa siku 3 zilizopita.

2802b6eb-befa-4eda-b037-df387d79bf73.jpg

Hao wanalipia 500 katika stationary ili wapate form za taarifa ya mhakiki. Lakini bado tunaaminishwa TIN ni bure. Kwanini Serikali isiweke miundombinu ya kuhakikisha huduma zinakuwa bure.

Kwakweli leo foleni za TIN namba ni ndefu sana hata kwa Ofisi za TRA Dar es Salaam, Nashauri waongeze muda. Kwanza wafanyakazi wanafanya kazi taratibu sana.
 
Ni kweli kabisa. Mimi nilienda jana nilipoona ile foleni nikaamua kuahirisha. Nimewnda tema leo pale Mwenge nimeishia nje maana hata parking tu ya magari haipo.

Swali kubwa la kujiuliza, usajili huu na uhakiki ni kwa faida ya TRA na mteja wake au mteja wake tu?

Maana nilimsikia jana kiongozi wa TRA akionge kwa jeuri kuwa hawataongeza muda tena as if ni kumkomoa mteja.

Mimi nadhani wazo lako ni zuri. Waruhusu uhakiki wa online pia, itapunguza foleni.

Hivyo waongeze muda na waruhusu online regitration. Ukienda TRA ni kuchukua gamba lako tu
 
Wadau

Pamoja na kuwa leo ni siku ya mwisho na nikikiri kwamba sijahakiki TIN number yangu, nichukue nafasi kueleza kutorodhishwa na namna zoezi hili lilivyoendeshwa.

Kikubwa hapa ni namna gani hasa sisi waajiriwa tutajigawa katika ya muda wa mwajiri na muda usiojulikana ambao utapaswa kushinda ofisi za TRA ukihakiki TIN number yako. Kwanini kusingekuwa na namna ya kupanga muda maalum kwa makundi flani ya watu au tudownload au kujaza fomu za uhakiki katika tovuti ya TRA na kuzituma kwao tukichangua na kituo kitakachotumika kufanyia zoezi hilo. Then TRA wanapanga muda na mhusika unajua kwamba tarehe flani saa flani nitapaswa kwenda kuhakiki TIN yangu. Mtu ni daktari au muongoza ndege utoke tu uende ukashinde ofisi ya TRA masaa manne.Kazi unamwachia nani ?

Na unaamini watakufuta? Pole
 
Mi mwenyewe nimeshaamua...liwalo na liwe...hamna namna...
Maana sioni mantiki...ndani ya mwaka mmoja lazima...lazima kila mwenye TIN atembelee TRA...kwa nini wasisubiri nikienda lipia road licence nimalize kila kitu badala ya kuturundika...

Afu nimeshangaa jana yule msemaji wao aliposema zoezi kwa Dar ndio linaisha...wanaamia kwingine...eeehhhh...ni mkoa kwa mkoa...basi ntaenda Moro kuhakiki...

Kuna jamaa yeye amenichekesha..amesema ataomba TIN mpya...maana wamesema watafuta za wasiohakiki....mi hata sielewi mantiki ya hili zoezi kwa kweli...au ndio fasheni...kila ofisi inahakiki...TRA utumishi...sijui wapi...
 
Ni kweli kabisa. Mimi nilienda jana nilipoona ile foleni nikaamua kuahirisha. Nimewnda tema leo pale Mwenge nimeishia nje maana hata parking tu ya magari haipo.

Swali kubwa la kujiuliza, usajili huu na uhakiki ni kwa faida ya TRA na mteja wake au mteja wake tu?

Maana nilimsikia jana kiongozi wa TRA akionge kwa jeuri kuwa hawataongeza muda tena as if ni kumkomoa mteja.

Mimi nadhani wazo lako ni zuri. Waruhusu uhakiki wa online pia, itapunguza foleni.

Hivyo waongeze muda na waruhusu online regitration. Ukienda TRA ni kuchukua gamba lako tu
kinachobadilika ile karatasi yao inamaua maua
 
Ndio shida ya watumishi wa serekali.Wanafanya vitu kwa kukomoa wananchi .Issue ya kulipa kodi ni huduma kama huduma nyingine wamefanya watu wanaona TRA kama kituo cha polisi kiasi kwamba ukiona mtu anakwepa kodi udhubutu kutoa taarifa.Mbadilike ,mhamasishewatu waelimisheni wapeni elimu na sio vitisho.Nchi zilizoendelea wamefika hapo walipofika kwa huduma safi kwa wananchi wao na sio vitisho.Wananikera sana
 
Ni kweli kabisa. Mimi nilienda jana nilipoona ile foleni nikaamua kuahirisha. Nimewnda tema leo pale Mwenge nimeishia nje maana hata parking tu ya magari haipo.

Swali kubwa la kujiuliza, usajili huu na uhakiki ni kwa faida ya TRA na mteja wake au mteja wake tu?

Maana nilimsikia jana kiongozi wa TRA akionge kwa jeuri kuwa hawataongeza muda tena as if ni kumkomoa mteja.

Mimi nadhani wazo lako ni zuri. Waruhusu uhakiki wa online pia, itapunguza foleni.

Hivyo waongeze muda na waruhusu online regitration. Ukienda TRA ni kuchukua gamba lako tu
Atakuwa hajitambui huyo ofisa uchwara...atakuwa na licheti feki ...utamkomoaje mlipa kodi
 
zoezi lilikuwa na muda mrefu muda ulipoongezwa watanzania tuka relax, kuna kipindi ulikuwa mtu ukienda unatumia dakika tano tu unamaliza
 
Kuhakiki huku ni kwa faida ya nani? Maana jamaa wa TRA ameongea kwa bashasha kabisa kuona zoezi limefikia mwisho kwa Dar na hali ya kuwa bado kuna wahakikiwa...na kasisitiza hawatoongeza muda tena.

Kama nimemsikia vizuri alichoongea ni kama alimaanisha kwa Tin ambazo hazijahakikiwa watazichukulia kuwa haziexist tena. Hii haiwezi kuwa ni upenyo kwa wale wenye madeni na hawakufanikiwa kuhakiki tin zao? Au baadae wakiomba tin mpya watanyimwa?

Watafute namna ya kufanya hili zoezi kuwa endelevu kwa Dar, hasa ukizingatia Dar inawalipa kodi wengi kuliko mkoa wowote Tanzania.
 
Back
Top Bottom