Tatizo ni kuwa tulifungua Ubalozi baada ya Uhuru wa Angola 1975; Ikumbukwe kuwa Tanzania tulikuwa upande wa Savimbi kwanza na alipoenda Msituni kuanza Vita ikabidi serikali ya Tanzania kuufunga huo Ubalozi.
Lakini mambo yalibadilika baada ya ushawishi wa Kenneth Kaunda, USSR na China; Nyerere akamtambua Agustino Neto na serikali yake; na Tukamuacha Savimbi, lakini hatukufungua Ubalozi...