Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Usitulishe matango pori humu mkuu hakuna upumbavu kama huo katika sheria ulifuatilia pale mahakama ya kusutu kuhusu hyo kesi na mtuhumiwa alienda na nin?
 
Wanajivunia hizo gun zao kwa vile wamefundishwa kupiga risasi tu na siyo kulenga shabaha!
Hata hivyo haikuwa mpango wa Mungu kumuua mwanajeshi ndo maana alibaki na huyo sijui nani kulwa akapitiwa kama ile risasi ilokuwa inaenda kwa mbowe ikapaa juu halafu ikakata kona kurudi kwenye daladala na kumpitia akwilina.

aitiviiiiiiii,maraaaaa!!!
 
Humu hakuna polis humu wewe leta hoja zenye mashiko mtu akiongea ukweli mnasema polisi mbona hao walio upande wa jw hamsemi jwtz

Acha ujuha huo nyinyi ndio wale wale mnaongozwa akil na mange kimambi
 
Wewe bila ubishi ni Polisi....

Ukitaka idara yenu ya Polisi iheshimiwe ni pale mtakapoacha kutumiwa na Wanasiasa
Hakuna kitu kama hicho huwa naheshimu saana watu wanao risk maisha yao kwa ajili yetu wakati tunakula mvinyo

Mm sio wew usiekuwa na maarifa ya kutosha kichwani
 
askari wa jeshi la police na wale wa jwtz ni kama kaka na dada wa tumbo moja kwa maana lengo lao ni moja nalo ni kulinda usalama wa taifa letu hili pendwa kwa njia tofauti tofauti.
hizi tofauti ndogondogo (skirmishes) huwa ni za kibinadamu sana kwa watu wa familia moja, hata ninyi leo hakuna mmoja wenu anayeweza kusema hakuwahi kugombana na ndugu zake angali anakaa na wazazi wake. tusiwe tunapenda kukuza mambo madogo na kuyafanya yanakusa ni issue kubwa sana zisizo na faida zozote zile za msingi.
 
Nchi yeyeto ile polisi siyo lolote siyo chochote mbele ya Jeshi. Kikinuka polisi wanaamriwa KAENI KAMA RAIA! Amini usiamini polisi wanavua magwanda na kwenda kujificha mvunguni mwa vitanda vyao. Jeshi siyo polisi bwana.
 
Jeshi ni Kitu sensitive sana katika nchi! Jeshi ni zaidi ya mapigano leo unataka kupeleka failure uko Utangamiza nchi wewe, Taifa lolote Swala la Security na Elimu ni lazima lipewe kipaumbele kikubwa sana.
 
We jamaa ni askari au mwanafunzi wa 4th year??
 
Bhana waende zao...pole mjeda...Nimekumbuka tukio moja la yule Traffic alikuwa anavua koti ili amwajibishe mshikaji walikuwa kama watatu kama sijakosea akampiga jamaa akawa ametulia tuu.Sasa angekuwa mjeda yule traffic angeisoma namba

Nakumbuka matukio polisi wakija mtaani kwetu wamekuta vijana wamekaa nje usiku wanapiga soga kama unavyojua uswahilini huwa tunakaa nje usiku maana ndani joto...wakija wanavamia tunakula virungu wakati hatuna hatia wala silaha yoyote tuna pandishwa kwenye defender lao tunapelekwa kituoni hapo umesha sachiwa kama una pesa imeenda na maji.

Ukifika kule kituoni waanza kukuangalia mdomo na mavazi(muonekano) ili wajue wakupe kosa gani...Ukiwa mweusi mweusi tayari wewe mvuta banghi....Ukiwa umekonda konda utasikia huyu anatumia madawa ya kulevya. Sasa jifanye hata kunyanyua mdomo uone virungu utakavyo pigwa.

Najua jeshi la polisi na polisi mpo huku viovu vyote mnavyo vifanya ni mnapandikiza chuki kwa raia...Mfano mdogo ni hata maoni mnayo yaona sasa ni kutokana na chuki ya jamii juu yenu. Raia wanawaombea mabaya kuliko mazuri.

Tatizo kubwa kwenu ni ELIMU TU....Elimu humfanya mtu kustaarabika na kujua kumanage mazingira ya aina tofautitofauti kwa resources zinazomzunguka. Sasa nyie ubabe,ulimbukeni,majivuno na masifa ndio yamewajaa

Mfano umenikuta ATM natoa pesa nina haraka nawahi hospital kumuuguza mwanangu...Wewe Askari ukaja ukaniambia Samahani mzee tunaomba tukukatishe unachofanya tunashusha mzigo wa pesa ni hatari kwa raia wa kawaida kuwepo karibu nasi....Unafikiri nitaacha kukupisha??

Sasa nyie mnaenda Weee wee toka hapo haraka...sogea kule....ptuu mimi kwa sababu sina hata bakora nitasogea nikiwa nasononeka moyoni BUT ningekuwa mjeda Wallahi ningetaka mtumie lugha nzuri kuniondoa .
 
Haka kagazeti uchwara ila kameandika vizuri mimi huwa sisomi hivi vipeperushi
 
Jeshi ni Kitu sensitive sana katika nchi! Jeshi ni zaidi ya mapigano leo unataka kupeleka failure uko Utangamiza nchi wewe, Taifa lolote Swala la Security na Elimu ni lazima lipewe kipaumbele kikubwa sana.
Huko hakuna shida sbb ukiingia vitani ni mwendo wa kuua tu. Huyu failure unamuachia kulinda raia na mali zao si ataendelea kuua tu. Angalia kwa Akwilima, angalia kwa mwandishi yule aliyeuwawa.
Huyo aliyempiga risasi mwenzake unafikiri alikuwa sahihi?
Yaan hata km raia umepewa bunduki, unaweza kumsogelea adui mpaka karibu? Wanashindwa hata technics wanazotumia majambazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…