DAR: Mwanafunzi UDOM anyongwa

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,464
INAUMA sana! Mrembo Happyness Fredric ‘Happy’, mkazi wa Yombo-Kanisani jijini Dar ambaye alikuwa ni denti wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), anadaiwa kuuawa kikatili kwa kunyongwa na kamba nzito hadi kufa, Uwazi lina mkasa wa kukutoa machozi.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia ya Happy, mpenzi wa mrembo huyo, Idrissa Mwangobola yupo matatani akihusishwa na tukio hilo.

BABA ASIMULIA

Akilisimulia Uwazi mkasa huo, baba mzazi wa Happy, Fredrick Mbode alisema kuwa, tukio hilo lililojiri hivi karibuni limemuumiza mno kwani mwanaye alikufa kifo cha mateso kupita kiasi.

ALIMKATAZA LIKIZO

Mbode alisema kuwa, kwa kuwa hii (ya mwezi Machi) ilikuwa ni ya muda mfupi, alimsihi mno Happy akae tu chuoni hadi likizo kubwa ikifika ndipo arudi nyumbani, lakini mwanaye huyo alisema amewakumbuka nyumbani hivyo angeomba kurudi na yeye alimkubali.

“Nafikiri kama mwanangu angefuata ushauri wangu niliomwambia, sidhani kama angekutana na kifo hiki, lakini aling’ang’ania kurudi,” alisema baba huyo kwa uchungu.


DDT.pngSIKU YA MAUAJI

Baba huyo alieleza kuwa, likizo ya Happy ilimalizika hivyo siku moja kabla ya kurudi chuoni, mwanaye huyo alimuomba fedha kwa ajili ya kwenda kukata tiketi na kununua vitu vyake ya chuoni.

Alisema alimpatia kisha wakaagana kuwa wangeonana jioni ya siku hiyo. “Kama ilivyo kawaida, mwanangu likizo ikiisha, huwa ninamkatia tiketi na ninampa fedha kwa ajili ya kununua mahitaji yake mengine ya chuoni na ndivyo nilivyofanya siku hiyo,” alisema baba huyo. Alisema kuwa, kwenye majira ya saa 10:00 jioni, Happy alimpigia simu na kumwambia kuwa gari alilokuwa akitaka kupanda, tiketi zilikuwa zimekwisha.

Akiwa anazungumza naye, mara alisikia kama kuna mvutano fulani kwenye simu, lakini hakutia shaka kwa sababu alijua yupo sehemu ya makelele kama inavyokuwa Stendi ya Ubungo. “Kwa vile mwanangu aliniambia akitoka Ubungo atakwenda Kariakoo kununua vitu vyake, nikajua wazi ni makelele ya huko kama ilivyozoeleka siku zote kunakuwa na fujo kutokana na pilikapilika na wingi wa watu,” alisema.


WAGUNDUA AMENYONGWA


Baba wa mwanafunzi huyo aliendelea kusimulia kuwa, kila wakati alikuwa akitazama simu anakutana “missed calls” za Happy na alipojaribu kumpigia simu ilikuwa haipokelewi hivyo hakumpigia tena akijua atamkuta nyumbani.

Baba Happy alisimulia kuwa, baada ya kufika nyumbani, majira ya jioni alimuulizia, akaambiwa hajarejea hivyo aliendelea na shughuli zake akijua kwa vile anaondoka kurudi chuoni, basi atakuwa amepita kwa rafiki zake kuwaaga.

“Nilikaa hadi saa 4:00 usiku bila Happy kurejea, nikaingia kujipumzisha nikijua akirudi atagonga mlango na kufunguliwa maana tulivyoona amechelewa mimi na mama yake tulipiga tena simu yake, lakini haikupokelewa,” alisema Baba Happy.

Huku akionekana kuwa na machungu, baba huyo alisema kuwa muda ulivyozidi kwenda mama yake alimtumia meseji ya kumuuliza yuko wapi mbona anawafanya washindwe kulala na baada ya muda mfupi meseji ilijibiwa;

“Kwaherini wazazi wangu, sipo kwenye mikono salama, sitakuwa nanyi tena.” “Kwa kweli baada ya ujumbe huo, mke wangu alidondoka na kuzimia na mimi hapohapo nikaanza kuita watu ili tuzunguke huku na huko.


DDT2.png

“Tulianzia Kituo cha Polisi cha Sigara kisha Tandika bila mafanikio. “Tulirudi tena Kituo cha Sigara ambapo tulivyowaelezea askari, wakatuambia kuna msichana ameokotwa majira ya saa 2:00 usiku maeneo ya jeshini, lakini anaonekana ni msichana mdogo,” alisema baba huyo.

Aliendelea kusema kuwa baada ya askari kumueleza alivyo, aligundua atakuwa ni mtoto wake, lakini alijipa moyo hadi alipofika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe na kuambiwa kuwa waende kwanza Hospitali ya Temeke kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kujua kama ndiyo huyo.

“Muda huo ilikuwa ni usiku wa saa 8:00. Tulipofika pale walikiri kupokea maiti mbili, moja ya msichana na nyingine ya mwanaume, lakini walisema ni vyema turudi kwesho yake. “Tulifanya hivyo, kulipokucha asubuhi yake tulikuwa pale na nilivyoingia tu kuangalia zile maiti, nilimgundua mtoto wangu. Lakini usoni alitapakaa damu, nikajua wazi labda alipigwa, lakini uchunguzi ulipofanyia tuligundua alinyongwa,” alisimulia baba huyo.


IDRISSA AJITOKEZA


Baba huyo aliendelea kusimulia kuwa, wakati wakiwa wanafanya taratibu za mazishi huku uchunguzi wa Polisi ukiendelea, baadhi ya wanafunzi wenzake walipata taarifa ya msiba mapema na aliyekuwa akiwajulisha ni huyo Idrissa aliyedaiwa kuwa mpenzi wake, jambo lililowatia shaka maana wanafunzi hao walipata taarifa mapema kabisa hata kabla ya wazazi wake.

Cha ajabu mama mzazi wa kijana huyo alifika msibani na kusema ameambiwa na mwanaye kuwa Happy alikuwa amefariki dunia maana walikuwa wakifahamiana.

“Tulipogundua kuwa sisi ndiyo tulikuwa wa mwisho kujua kifo cha mwanangu huku baadhi ya marafiki zake wakijua mapema walikuwa wanatafuta mawasiliano yetu na aliyewataarifu ni yule kijana. “Hivyo tulijaribu kupanga mikakati ya kuzungumza na marafiki zake wamvute hadi msibani na kweli alijitokeza kwenye kuaga kanisani huku mama yake mzazi akilala siku mbili msibani,” aliendelea kusimulia baba huyo.


IDRISSA AKAMATWA

Baba Happy alisema baada ya kijana huyo kufika kanisani, askari nao walifika kisha kumkamata ambapo hadi gazeti hili linakwenda mtambaoni kijana huyo alikuwa chini ya jeshi la polisi.

KAMANDA TEMEKE

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Amon Kakwale alipopigiwa simu na kuulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa, watuhumiwa wote walishakamatwa. Gazeti hili linatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Happy na tunaamini polisi watafanya kazi ya kuhakikisha waliohusika na mauaji hayo wanachukuliwa hatua kali.Muda huo ilikuwa ni usiku wa saa 8:00. Tulipofika pale walikiri kupokea maiti mbili, moja ya msichana na nyingine ya mwanaume, lakini walisema ni vyema turudi kwesho yake.
 
Huenda wakiwa ghouse, husband to be alipitia simu ya wife to be akakuta vitu na sms zisizofaa. Katika prukushani, husband to be akawa amakamata mtandio wa mpenzi wake kiasi ukatelezea shingoni kuwa km anamkaba. Binti kuona anakabwa ( ingawa ilikuwa tisha toto), akahamaki na kumng'ata kikwelikweli husband. Husband akatapatapa na kukaza kidogo mtandio ili wife asiendelee kumng'ata. Kukawa na kusukumana huku na huku kiasi mtandio ukakaza zaidi...........Pole yao. Mungu aepushie mbali haya!!!
 
Back
Top Bottom