DAR: Moto mkubwa wazuka soko la Mbagala rangi tatu

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Kuna Jamaa yangu, kanipigia simu kunijulisha kuwa soko la mbagala rangitatu linaungua,

Mwenye updates atujulishe...

=======

Leo saa moja asubuhi umezuka moto katika soko la Mbagala Rangi 3. Sehemu iliyoathirika zaidi ni ya wauza mitumba. Imefika gari ya jeshi la zima moto na kuzima moto huo bila mafanikio. Mpaka naondoka eneo la tukio hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo inadhaniwa ni hitilafu ya umeme.

====

UPDATES:
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Temeke Emmanuel Likula amesema kuwa Moto ambao umezuka leo katika Soko la Mbagala Rangi tatu na kuteketeza Mabanda ya wafanyabiashara umeanza kwenye kibanda cha muuza samaki wabichi na kisha kusambaa kwenye vibanda vingine

Tarehe 6 February 2018, moto pia uliunguza maduka Mbagala na sababu ikidaiwa ni Hitilafu ya umeme. Habari zaidi, Soma=>Dar: Moto waunguza Maduka Mbagala rangi tatu
 
Ni kweli limeshaungua nusu soko mpaka sasa ....na fire IPO moja maji yameisha halijazimika wameenda kupata maji hivyo moto bado unaendelea
 
Poleni wahanga wa moto...kuna ndg yangu anafanyia biashara hapo ngoja nimtafute
 
Leo saa moja asubui umezuka moto katika soko la Mbagala rangi 3. Sehemu iliyo athirika zaidi ni ya wauza mitumba. Imefika gari ya jeshi la zima moto na kuzima moto huo bila mafanikio. Mpaka naondoka eneo la tukio hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa. Chanzo cha moto huo inadhaniwa ni hitilafu ya umeme.
 
Kuna Jamaa yangu, kanipigia simu kunijulisha kuwa soko la mbagala rangitatu linaungua,

Mwenye updates atujulishe...

=======

Leo saa moja asubuhi umezuka moto katika soko la Mbagala Rangi 3. Sehemu iliyoathirika zaidi ni ya wauza mitumba. Imefika gari ya jeshi la zima moto na kuzima moto huo bila mafanikio. Mpaka naondoka eneo la tukio hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo inadhaniwa ni hitilafu ya umeme.
Poleni sana wakuu
 
Wiki kama mbili zilizopita kuna maduka yaliungua yote....Njia ya kwenda chamazi hko
Poleni wana mbagala

Ova
 
Back
Top Bottom