Dar, matumizi ya nguzo za umeme kusitishwa, nyaya za umeme kupita chini ya ardhi

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,685
1.png

Wataalam kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), wanaendelea kupiga hesabu kabla ya kuja na majawabu ya kushusha bei ya umeme.

Aidha, Profesa Muhongo alisema, kwa mara ya kwanza, wanataka nyaya zote za umeme jijini Dar es Salaam hususan katikati ya jiji, zipite chini ya ardhi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema jana bungeni kwamba bei hiyo itashuka kwa mchakato huo (wa kupiga hesabu) na si kwenye majukwaa.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) aliyetaka kufahamu hatua ambazo serikali imefikia katika uzalishaji, usambazaji na umeme kwa ubia.

“Kuhusu bei ya umeme, wengine wanasema nilisema ishuke haijashuka nilisema tunapiga hesabu. Bei huwezi kuongea kwenye majukwaa. TANESCO na Ewura wanapiga hesabu tunataka kushusha bei na si kwenye majukwaa,” alisema.

Kwa upande wa nyaya za umeme, alisema mkandarasi ameelekezwa ifikapo Aprili mwaka huu, serikali iachane na kesi za nyaya kuanguka kwa kuwa zitakuwa zimepitishwa chini ya ardhi.

“Kwa mara ya kwanza, Serikali inataka nyaya zote za umeme zipite chini ya ardhi,” alisema na kufahamisha bunge kwamba, maeneo ya Mbagala na Temeke, inajengwa transfoma kubwa.

Pia kwa upande wa Jimbo la Kibamba, inaondolewa transfoma yenye kilovolti 100 kuwa na yenye kilovolti 2000.

Alisema Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu ambapo inatarajia kuwa na umeme wa megawati 10,000. Profesa Muhongo alisema serikali inaendelea kukaribisha wawekezaji na kwamba Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu.

Akizungumzia suala la usambazaji umeme, alisema kuna miradi kadhaa inaendelea kutekelezwa na serikali kwenye maeneo mbalimbali nchini. Profesa Muhongo alisema umeme uliopo hivi sasa hauvuki megawati 1,500 na ili kufikia lengo wanahitaji kufikia megawati 10,000.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, alisema ukarabati wa miundombinu katika jimbo hilo, unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao na kukamilika Juni, mwaka huu.
 
Kwa miundo mbinu ya Dar sahau hiyo kitu.

Mara ngapi tumeoneshwa Ramani ya Kigamboni City?

Mara ngapi tumeoneshwa picha ya Flyovers za Tazara?

Mwendo kasi kila mwezi tunaambiwa zitaanza.

Hiyo tunaita changamsha genge.
 
Zaidi ya asilimia 80 ya Dar kwa mfano ni squatters.
Hilo litakuwa gumu kutekeleza. Kwa sehemu zilizopimwa inawezekana kabisa na kitu kizuri mno.
 
Kwa miundo mbinu ya Dar sahau hiyo kitu.

Mara ngapi tumeoneshwa Ramani ya Kigamboni City?

Mara ngapi tumeoneshwa picha ya Flyovers za Tazara?

Mwendo kasi kila mwezi tunaambiwa zitaanza.

Hiyo tunaita changamsha genge.

ni vyema kuwa na mipango pamoja na kufikiria mipango mbadala kuliko kuwa na mpango ule ule duni na hafifu ktk utekelezaji.

~ lisemwalo lipo, kama halipo laja ~
 
Hili likitokea itakuwa kiama. Hebu imagine nyaya ziwe exposed na mafuriko wakati bado hazijawa disconnected!!
Zingatio la kwanza la Umeme ni Safety Hapo lazima tuhakikishe safety ipo ikiwa patatokea mafuriko au Uharibifu tutafunga special breakers kwa ajili ya ku discharge line panapotokea Faulty yoyote
 
Nakataa hilo, hatuna miundombinu ya kupitisha Nyaya Chini ya Ardhi... Hii ilipaswa kuandaliwa wakati wa ujenzi wa barabara kwa kuacha tunnel ya kuaccomodate hizo huduma.
Hebu fikiria Dawasco wamechimba chini kivyao, Jamaa wa simu pia wakaja wakachimba na kukata bomba, leo Tanesco pia wachimbe na kukata nyaya za simu na maji, badae gesi ije itafute njia yake.
Hapana labda tuvunje na hizo barabara tuanze upya.
Barabara ya nwenge kwa Mfano inapaswa kua Designed kwa huduma hizo.
 
View attachment 319899

Wataalam kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), wanaendelea kupiga hesabu kabla ya kuja na majawabu ya kushusha bei ya umeme.

Aidha, Profesa Muhongo alisema, kwa mara ya kwanza, wanataka nyaya zote za umeme jijini Dar es Salaam hususan katikati ya jiji, zipite chini ya ardhi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema jana bungeni kwamba bei hiyo itashuka kwa mchakato huo (wa kupiga hesabu) na si kwenye majukwaa.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) aliyetaka kufahamu hatua ambazo serikali imefikia katika uzalishaji, usambazaji na umeme kwa ubia.

“Kuhusu bei ya umeme, wengine wanasema nilisema ishuke haijashuka…nilisema tunapiga hesabu. Bei huwezi kuongea kwenye majukwaa. Tanesco na Ewura wanapiga hesabu tunataka kushusha bei na si kwenye majukwaa,” alisema.

Kwa upande wa nyaya za umeme, alisema mkandarasi ameelekezwa ifikapo Aprili mwaka huu, serikali iachane na kesi za nyaya kuanguka kwa kuwa zitakuwa zimepitishwa chini ya ardhi.

“Kwa mara ya kwanza, Serikali inataka nyaya zote za umeme zipite chini ya ardhi,” alisema na kufahamisha bunge kwamba, maeneo ya Mbagala na Temeke, inajengwa transfoma kubwa.

Pia kwa upande wa Jimbo la Kibamba, inaondolewa transfoma yenye kilovolti 100 a kuwa na yenye kilovolti 2000.

Alisema Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu ambapo inatarajia kuwa na umeme wa megawati 10,000. Profesa Muhongo alisema serikali inaendelea kukaribisha wawekezaji na kwamba Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu.

Akizungumzia suala la usambazaji umeme, alisema kuna miradi kadhaa inaendelea kutekelezwa na serikali kwenye maeneo mbalimbali nchini. Profesa Muhongo alisema umeme uliopo hivi sasa hauvuki megawati 1,500 na ili kufikia lengo wanahitaji kufikia megawati 10,000.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, alisema ukarabati wa miundombinu katika jimbo hilo, unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao na kukamilika Juni, mwaka huu.
Aisee huu mziki sio mchezo na sio rahisi kama wengi tunavyochukulia kwa kuangalia viongozi wakitumia maneno mepesi sana, hii inahitaji serikali iangalie kwanza miundombinu ya jiji lote la dar then ndio lifikiriwe hili maana kwa hali ilivyo hapa dar panahitaji pamp nyingi sana tena automatic vinginevyo sijui ni mfumo upi unaotarajiwa kutumika. Kwenye hivi vituo vingi vya kufua umeme hapa dar cables zote zimepitishwa underground lakini zimefungwa pamp kubwa sana ndio zinawezesha hizo chanels muda mwingi kuwa kavu.
 
Back
Top Bottom