DAR: Hospitali zinaziendelea kuzuia maiti kwa sababu ya deni zaonywa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku hospitali kuzuia maiti kwa sababu mgonjwa alishindwa kulipa deni na badala yake wakabidhi mwili kwa Ndugu wa marehemu kwaajili ya kuzika wakati taratibu nyingine zinaendelea.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea Malalamiko ya Wananchi juu ya baadhi ya hospital Mkoani humo kuendelea na utaratibu wa kuzuia maiti licha ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kukataza uzuiaji wa maiti.

Kutoka na hilo RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya Chini ya Wakuu wa Wilaya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii Katika Maeneo yao.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanazingatia suala la Matibabu kwa Wazee ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu kwaajili ya Wazee.

Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni.
 
Hapo serikali mkiri tu kuwa mnawasukumia watumishi mzigo. Ukweli ni kwamba hakuna atakaeweza kufuatilia madeni hayo mtaani. Hapo ni kuwapa kazi watumishi ambazo hazistahili. Wana kazi kubwa sana hawa watu. Kote kuchungu, huwezi kuzuia mwili kwa kigezo cha deni, hii ipo wazi, lakini pia si rahisi kudai gharama za matibabu baada ya ndugu kumzika ndugu yao. Ili kupunguza ukubwa wa tatizo, hakikisheni huduma za matibabu zinakuwa nafuu ama bure kabisa (mnafanyaje, hiyo si kazi yetu raia,hivi vitu ndiyo mlivitumia kuomba kura). Acheni kujifanya kuwa watumishi ndiyo wabaya kwa kuzuia miili ya watu wakati ule upungufu wa dawa na gharama za matibabu mnawahoji.
 
Mi mwenyewe nawashangaa wanasiasa. Wanatoa majibu mepesi tu. Jambo ni moja tu, kama mtu mmeshindwa kumtibu basi na bili mshindwe kudai. Ila na sisi wanachi hatukomi aisee, Lisu alisema matibabu yangekuwa bure sisi tukachagua madaraja🤣🤣
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku hospitali kuzuia maiti kwa sababu mgonjwa alishindwa kulipa deni na badala yake wakabidhi mwili kwa Ndugu wa marehemu kwaajili ya kuzika wakati taratibu nyingine zinaendelea.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea Malalamiko ya Wananchi juu ya baadhi ya hospital Mkoani humo kuendelea na utaratibu wa kuzuia maiti licha ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kukataza uzuiaji wa maiti.

Kutoka na hilo RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya Chini ya Wakuu wa Wilaya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii Katika Maeneo yao.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanazingatia suala la Matibabu kwa Wazee ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu kwaajili ya Wazee.

Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni.
Kwann hayo madeni yasilipwe!?
 
Back
Top Bottom