Kuna siku nimekwenda pale ofisi zao za Arusha kusafirisha bahasha ya A4 iliyokuwa na cheti nikamwomba dada aliyekuwa hapo hiyo bahasha asiikunje akaniambia hawezi kunihakikishia kuwa haitakunjwa basi nikamwambia kama ni hivyo anipe nikajaribu kutuma kwa kutumia kampuni nyingine. Yule dada wakati huo alikuwa kesha anza kuandika detail za mzigo akairusha ile bahasha chini kwa hasira akaniambia kwenda huko...dah nilitoka mnyonge sana na sijawahi tena kurudi Dar express hiyo ni kama miaka minne sasa imepita...nilijiapiza sitatumia huduma zao milele