Huu ni ujumbe umfikie ndugu waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba popote alipo na ni tahadhari kwa wageni wanaosafiri kuja Dar es salaam na wengine wenye makazi yao katika jiji la Dar es salaam.
Kwa wale wanaoishi jijini Dar es salaam na hata wageni wanaosafiri kuja Dar es salaam mnahitajika kuwa makini sana kwa usalama wenu hasa mida ya usiku wapo "watoto"/vijana wenye umri wa makamo wa kuanzia miaka 15 - 30 hivi hawa vijana huwa wanatembea na silaha ndogondogo yani mapanga, visu nk.na kutishia watu ili waweze kupora mali zao.
Unapotembea hakikisha unakuwa umejihadhari kwa kujilinda vizuri sana dhidi ya chochote kile uwe umekamilika (njia hii ni kwa wale wanaoweza kufanya hivi tu na kama hauko vizuri usitumie hii ni hatari) au vinginevyo tumia njia ya kuepukana na shari kwa kutokutembea kabisa mida ya usiku au hakikisha unawahi kurejea kwenye makazi yako mapema sana kabla ya giza halijaingia.
Mimi huwa lazima nitembee usiku hii ni kutokana na kazi zangu ninazofanya natembea kuanzia saa 5.00 PM + haya nakutana nayo sana na niliapa kukabiliana na hawa vijana wahalifu ili tu kujihakikishia usalama wangu .
"I AM A FIGHTER, AND I WILL DIE IN THE FIGHT AGAINST INJUSTICE".
Hatuezi tu kukubali pale dhulma zinapotamalaki dhidi ya HAKI kwenye jamii hatuezi kubaki tu kimya wote sababu kubaki kimya katika hujuma na dhulma dhidi ya asiye na hatia hii maana yake ni kukubali kusitishwa kwa uhai wetu sote.
Huwa napenda sana kutenda HAKI na napinga yale yote mabaya iwe yametendwa na raia wa kawaida, kiongozi wa kidini, kiongozi serikalini au na yeyote yule kama anatenda uovu unaohatarisha utu, usalama na uhai wa wengine wasio na hatia nitampinga bila mimi kuvunja sheria za nchi.
Ndiyo, mtenda maovu nitampinga ingawa nafahamu kwa kupenda kwangu kutenda HAKI kunanifanya niwe hatarini daima sababu watenda maovu hawapendi kupingwa.
Naomba waziri husika mwenye dhamana yani waziri wa mambo ya ndani ndugu Mwigulu Nchemba usikie na uchukue hatua inakuaje watu wanaishi kwa hofu na wasiwasi ndani ya nchi yao wenyewe?
Hii sio vizuri kabisa hata kwa ustawi wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Cc Mwigulu Nchemba.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.