Dar es Salaam inanuka maji taka

Dar es Salaam inanuka maji taka

Nkungulume

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,987
Reaction score
1,210
Ndugu wana jamvi,

Wakati Dar ikijiandaa ili liwe jiji lenye hadhi na safi ni jambo la kusikitisha kuona chemba za maji taka zinatiririsha mitaani maji hayo machafu katika maeneo mbali mbali.Ukianzia kata ya Kisutu hadi Mnazi Mmoja maeneo yaliyoathirika zaidi ni mtaa Jamhuri Barabara ya Lumumba maeneo yote hayo yamekuwa yakitiririsha maji kwa takribani mwezi mmoja sasa.

Ni aibu kubwa sana kuona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa mpaka sasa kuhakikisha tatizo hili linakwisha.Nadhani Mkuu wa Mkoa angekaa na watendaji wake mkaandaa mikakati mizuri itakayowezesha maeneo kuhudumiwa kwa utaratibu mzuri.

Badala ya kufanya mabonanza ambayo kwa mtazamo wangu mimi haya tija baada kufanya hayo mabonanza huishia kwenye hayo mabonanza na hakuna kinachoendelea baada ya hapo.

Ni dhahiri kuwa bila kuchukia hatua za makusudi na kujipanga katika kutekeleza jambo hili jiji litaendelea kuwa chafu kila siku.

Nawakilisha wanajamvi ili nanyi mchangie na kutoa mawazo yenu.
 
Wameanza kwanza kusafisha majipu
Watafikia subiri
 
Siku ya usafi watu wanaongozana na mkuu wa mkoa kwenda kufagia leaders club, badala ya kuzibua chemba za maji taka.
 
Huyu "kondakta" inabidi atumbuliwe kama vipi .....haiwezekani maji kata yamezagaa halafu yeye yupo ofisini kama haoni vile.
 
Harufu yao wameshaizoea mpaka Pua imeshindwa kunusa kuwa Ndani mwa Pua kunatoa harufu.

Ngoja Tuwaache na Dar yenu msije sema tunawaonea Wivu.
 
Siku ya usafi watu wanaongozana na mkuu wa mkoa kwenda kufagia leaders club, badala ya kuzibua chemba za maji taka.
Ni jambo la kushangaza sana inatakiwa kila mtu awajibike sehemu yake
 
Hapo lumumba sio taka tu zinakuka kuna jengo hapo bora mavi
 
Ni ukweli pale Mwenge kutazamana na efata benki na pia old bagamoyo road lazima uugue mafua

hapa kazi tu
 
Miundombinu ya majitaka haiendani na uongezeko la watu.
Miundombinu ni ya kuhudumia idadi ya watu wa mwaka 1970.
 
Back
Top Bottom