PreGE2025 Daniel Mwangili atangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kalenga

PreGE2025 Daniel Mwangili atangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kalenga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Iringa Ndugu Dr Daniel Mwangili ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kalenga Mkoani Iringa, Mwangili ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Luhota Jimbo la Kalenga ameeleza nia hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mwangili ameeleza kuwa anao utayari na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kalenga.

Ameeleza pia anao uwezo wa kuitafsiri ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025 - 2030 Kwa vitendo katika Jimbo la Kalenga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Ameweka wazi kuwa tarehe 28/06/2025 atachukua Fomu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya Chama.

 
Back
Top Bottom