Elections 2010 Damu Yanukia Moshi.

Dec 5, 2009
65
23
Nimeifuma habari hii ya kutisha kuhusu aina ya siasa zinazofanyika katika jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Wastaarabu someni TAMKO hili la Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro na tuchambue yaliyotokea huko kwa lengo la kulinda mustakabali wa nchi yetu









CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)


Mkoa wa Kilimanjaro


P.O BOX 933, MOSHI



20/6/2010


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



UVUNJIFU WA AMANI ULIOFANYWA NA CCM MJINI MOSHI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Kilimanjaro kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya kinyama yaliyofanywa na CCM katika kata za Longuo A na Longuo B za wilayani Moshi.

Mnamo tarehe 18/6/2010 majira ya saa 10 jioni vijana zaidi ya 300 wa Chama Cha Mapinduzi waliokuwa wamevalia sare rasmi za chama chao (kijani na njano walikuwa katika maandamano wakitokea Mweka walikofanyia semina ya wiki moja nzima walikokuwa wakifundishwa mbinu za kukabili uchaguzi mkuu na kushinda jimbo la Moshi Mjini.

Mambo waliyofundishwa katika semina hiyo na watu waliokuwa wakifundisha huko si tatizo kubwa kwetu ingawaje tuna taarifa ya kila jambo lililofanyika huko. Tunasubiri hatua muhimu chache za kutangaza maelekezo ya kinyama yaliyokuwa yakifundishwa na kutolewa na viongozi wa ngazi za juu wa CCM katika kambi hiyo.

Tunachotaka kukemea leo ni vitendo vilivyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/6/2010 vijana hao walipokuwa wakirudi kutoka kambini.

Vijana hawa walipita katika barabara kuu itokayo Mweka kuingia mjini Moshi wakiimba na kuonyesha ishara ya dole gumba ambayo hutumiwa na chama chao. Kila walikopita na kukosa kushangiliwa na pengine kupungiwa kwa alama ya vidole viwili vya ushindi alama inayotumiwa na CHADEMA walisitisha maandamano na kuwafuata watu hao na kuwapiga sana.

Katika utekeleza wa maagizo hayo ya kujeruhi na kuwatisha wakazi wa mji wa Moshi wamewajeruhi watu kadhaa na kupora mali zao. Huu ni uhuni ambao hatujauzoea mjini Moshi vijana wa chama wanapora simu kutoka kwenye sidiria ya mama mtu mzima? Hatuwezi kunyamazia udhalilishaji wa kijinsia uliofikia kiwango hiki.

CHADEMA mkoa wa Kilimanjato imesikitishwa sana na kitendo cha wahuni hawa kuingia katika majengo ya kitengo cha damu salama cha hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi na kuwapiga wafanyakazi wote waliowakuta mle, wakavunja vifaa na vioo vya magari na hivyo kusababisha huduma ya kugawa damu salama kukosekana kwa siku hiyo.

Ni watu wangapi wamefariki kutokana na kukosekana kwa damu siku hiyo?
Je CCM wameamua sasa hata kumwaga damu iliyotolewa na wasamaria wemu kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wenzao? Kiu ya Damu ya CCM inaiwakia nchi kwa makali makubwa. Sasa wanaitaka damu hadi kuifuata katika kituo c ha damu salama.

Taarifa zenye uhakikia tulizo nazo ni kuwa katika msafara huo walikuwepo viongozi wa chama na pia msafara uliongozwa na askari wa usalama barabarani. Wakati vitendo vya vurugu vikifanyika askari hawakuchukua hatua yoyote zaidi ya kutuliza mambo kwa wanaojeruhiwa na kuharibiwa mali zao.

Tunajiaminisha kuwa kiburi cha vijana hawa wa CCM hakitokani tu na mafunzo waliyopewa bali maagizo waliyopewa na viongozi wa chama chao na serikali. Vijana hawa wamehakikishiwa kuwa hakuna mtu wa kuwafanya lolote watakapovunja sheria za nchi.

Hadi sasa jeshi la polisi wilayani Moshi halijachukua hatua yoyote dhidi ya CCM wala wahuni hawa.

CHADEMA mkoani Kilimanjaro inaamini kuwa ni jukumu la Polisi kulinda raia wote na mali zao. Jukumu hili linatokana na ukweli kuwa raia wote wanalipa kodi ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kutoka katika idara zote za serikali.

CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro inazo taarifa kuwa viongozi wa ngazi za juu serikalini na katika Chama Cha Mapinduzi wamekuwa wakiwachochea vijana hawa kufanya vurugu eti kwa lengo la kuwatisha wakazi wa Moshi Mjini kutokana na msimamo wao wa kuichagua CHADEMA.

Mathalan Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Yusuph Rajab Makamba alifika mjini Moshi na kufikia kutaja majina ya viongozi waandamizi wa CHADEMA ambao atawashughulikia yeye binafsi. Aliendelea kutamba kuwa yeye ndiye mwenye serikali na wanaweza kufanya lolote bila kuhojiwa. "Sisi tunaiagiza serikali kufanya kitu bila kuhojiwa" alijitapa.

Mtunza hazina wa CCM taifa Amos Makala akifungua kambi hiyo ya vijana aliwaagiza vijana hao kuwa "Mtu wa CHADEMA akikupiga ngumi moja wewe mpige kumi"

Taarifa tulizo nazo ni kuwa Mhe. Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM taifa akiwa katika ziara mkoani kwetu aliwahakikishia vijana wa CCM kuwa yeye ndiye mwenye serikali na kwamba analitaka jimbo la Moshi |Mjini kwa gharama yoyote.

Kwa kauli hizi za viongozi ambao wote si wazaliwa wala wakazi wa Moshi ni wazi kuwa hawajali umwagaji damu unapofanyika mjini hapa. Wanajua wazi kwa kauli zao zitaishia kusababisha umwagaji damu lakini hawaogopi kwani familia zao haziko hapa. Wala hawana ndugu yeyote aishiye mjini Moshi.

CCM wanajitapa kuwa wametengeneza jeshi lake la kupambana kulinda maslahi yake. Sisi CHADEMA tunauliza je sheria ya vyama vya siasa inaruhusu umiliki na uendeshaji wa jeshi kufanywa na chama cha siasa.
Kama CHADEMA nasi tukaamua kuunda jeshi letu la kupambana na uonevu wa CCM tutaepuka vipi umwagaji damu?
Kwa nini CCM hawataki kufanya siasa za kistaarabu? Kwa nini hawataki tushindani kwa kujinadi kwa wananchi?

Tunasubiri majibu na hatua zitakazochukuliwa na jeshi la Polisi hapa Moshi ili nasi tutangaze msimamo wetu na namna tutakavyowalinda watu wa Moshi na mali zao.
Tutatoa pia maelezo ya kila jambo lililotokea na kuwapelekea wahisani wa nchi yetu na jumuia za kimataifa endapo serikali haitachukua hatua za kuturidhisha dhidi ya wahuni hawa.

HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE

SIGNED

..........................
Basil Lema
KATIBU (M)
 
mambo kama haya yananiumiza moyo sana, Mungu nisaidie na uliponye Taifa letu.
 
Where are we Going?????? I love Moshi.....I lived There.....its the most clean Town I have ever seen......Would love Chaggaz to Live in piece as they have always been........

God bless Moshi God Bless Tanzania.
 
Kwa akili ya Makamba na viongozi waandamizi wa CCM walioko madarakani hivi sasa, umwagaji damu hauepukiki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. CCM aliiweza Mangula tu. Hawa waswahili waliopo sasa ...!! Naungana na CHADEMA kuwaita hawa (CCM) ni wahuni na nitamuunga mkono katibu wa CHADEMA mjini Moshi kwa ajili ya Revenge iwapo serikali haitatoa tamko juu ya uhuni na uvunjifu wa amani uliofanywa na hao wanachama wa chama cha mafisadi.
 
Dawa ni ndogo sana, ili kuondoa ubishi ningewasihi viongozi wa vyama vya upinzania kuwa na security cameras, ambazo mtu hawezi kuziona ziwe zinavaliwa under cover, na kuchukua matukio yote kama haya. Vinginevyo tutaendelea kuwa mchezo uleule wa kutupiana lawama na kusema ni pandikizi wa chama fulani. Kama kuna video itakuwa mwisho wa ubishi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwaweka CCM na propagandists wao accountable.
 
Dawa ni ndogo sana, ili kuondoa ubishi ningewasihi viongozi wa vyama vya upinzania kuwa na security cameras, ambazo mtu hawezi kuziona ziwe zinavaliwa under cover, na kuchukua matukio yote kama haya. Vinginevyo tutaendelea kuwa mchezo uleule wa kutupiana lawama na kusema ni pandikizi wa chama fulani. Kama kuna video itakuwa mwisho wa ubishi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwaweka CCM na propagandists wao accountable.

Ndugu yang Hofstede: Kama polisi wetu na vyombo vyote vya sheria ni watetezi wakuu wa CCM hizo picha utampelekea nani akusikilize?

Tukio hilo laoinyesha wazi kuwa CCM iko hoi kabisa katika jitihada za kulichukua jimbo hilo na hivyo kilichobakia ni kufanya unyama wakisaidiwa na polisi! Hao vijana 300 hawawezi kufanya vitendo hivyo kwa hiari yaom bila shaka wamelipwa vijisenti vichache. Bila malipo, CCM haina wafuasi wa kutisha Moshi.
 
Kama nakumbuka vizuri ni kwamba wakati wa uchaguzi mdogo wa Bunda CCM waliacha tu kuua Watanzania pale waliona fika kwamba CHADEMA inalinda wananchi.

Tungependa sana tuwe na amani, lakini uzoefu unaonyesha CCM wana msimamo wa kutaka kumwaga damu kama itabidi kufanya hivyo ili "kushinda".

Ni vema CHADEMA Moshi wakafanya maandalizi ya kuwahakikishia CCM kwamba kama wakipiga wananchi, basi CHADEMA itapigana nao. Lazima kutayarisha Youth Wing ya CHADEMA Moshi.

Kam huwezi kutegemea kulindwa na Polisi si lazima ujilinde mwenyewe?

In some situations, the only way to maintain peace is to adopt the doctrine of mutual assured destruction. I never knew it would come to this in Tanzania. But I never knew CCM would want to rule at any cost either!
 
Damu ina nukia au ina nuka?

.....panapofuka MOSHI iko moto. Makuwadi wa akina Makamba wanajulikana. Kina Aggrey na kundi lake la wahuni wamo. They reflect sura za chama chao. Ingawa CHAMA ni sera na si watu, hawa jamaa fikra zao ni muflisi kabisa. MOTO wa MOSHI utawachoma kisawasawa maana hawajui wanachokonoa nini. Salama yao wapeleke upuuzi wao hukooo kwa walowatuma. Huko USWAHILINI kwao kwa WASWAHILI kulosheheni porojo za kila namna.
Mtanzania hana budi atambue na akubali UKOMBOZI wake ni hapo atakapoachana na USWAHILI. WASWAHILI sio jina la kabila ila wale wote wanaoendelea kuivalisha Tanzania huu MKENGE!!! CCM wamo!
 
Hapa nimegundua watu wanachangia kwa jazba bila ya kuhakiki yaliyoandikwa.Siungi mkono machafuko yoyote hata kama yatafanywa na mtoto mdogo,ila ninachotaka kusema ni kwamba iwapo mtu anavunja sheria inakupasa wewe unayemuona ukamchukulia sheria zinazostaili na si kukaa na kulalamika kwani kulalamika si suluhisho la kutatua matatizo.Pili iwaje ccm wapite barabarani halafu wewe chadema ukamwonyeshea alama ya chama chako,uoni kuwa hilo ni kejeli ambayo itakulazimu kuilipa kwa namna yoyote ile.Tatu chadema wanasema eti viongozi wa ccm (akina Makamba,Makala na Kikwete)hawatoki na wala hawaishi moshi,kwani moshi ni ya wachaga tuu na wengine hawaruhusiwi kuishi na kutembelea huko,je huyo jamaa haoni huko ni kuvunja katiba ya TZ yakuwa raia yoyote anaruhusiwa kuishi mkoa wowote ili muradi havunji sheria?
Acheni mambo ya ukabila na ujimbo huo nao ni uhuni kama ambavyo hao vijeba wa ccm walivyofanya.Ninachokijua mimi viongozi wengi wa upinzani ndio wavunja sheria wakuu ila mwakiguswa tuu uanza kulalama kama mtoto wa miaka 2.Kuweni waangalifu hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani wengi wanataka hisani na huruma ya watu toka nje ya TZ.
Mwisho wote waliojihusisha na uchafuzi wa mazingira hayo wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya TZ(Hao waliopiga watu,walioingilia msafara wa wenzao kwa kuonyesha vidole 2 na hata walioona na wakakaa kimya)
Mungu ibariki Tanzania(tuachane ne ukabila).
Najua nitachukiwa kwa kusema ukweli ila inabidi ukweli utamkwe hata kama unauma!!!
 
Hapa nimegundua watu wanachangia kwa jazba bila ya kuhakiki yaliyoandikwa.Siungi mkono machafuko yoyote hata kama yatafanywa na mtoto mdogo,ila ninachotaka kusema ni kwamba iwapo mtu anavunja sheria inakupasa wewe unayemuona ukamchukulia sheria zinazostaili na si kukaa na kulalamika kwani kulalamika si suluhisho la kutatua matatizo.

Pili iwaje ccm wapite barabarani halafu wewe chadema ukamwonyeshea alama ya chama chako (Iweje CCM wapite maeneo ambayo likely yako mostly dominated na CHADEMA (matokeo ya uchaguzi uliopita yanathibitisha hilo) waonyeshe alama ya CCM),uoni kuwa hilo ni kejeli ambayo itakulazimu kuilipa kwa namna yoyote ile (Kwa hiyo Kejeli hiyo inalipwa kwa kupiga watu? Gimme a break).

Tatu chadema wanasema eti viongozi wa ccm (akina Makamba,Makala na Kikwete)hawatoki na wala hawaishi moshi,kwani moshi ni ya wachaga tuu na wengine hawaruhusiwi kuishi na kutembelea huko,je huyo jamaa haoni huko ni kuvunja katiba ya TZ yakuwa raia yoyote anaruhusiwa kuishi mkoa wowote ili muradi havunji sheria? (Hii argument yako inaonyesha jinsi unavyoshindwa kuchambua mambo, viongozi wa CHADEMA hawakatazi mtu kuishi Moshi bali wanawashangaa watu wasio wakazi wa eneo hilo kuchochea vurugu. Ukweli ni rahisi tu wao hawatakuwa affected)

Acheni mambo ya ukabila na ujimbo huo (Hii hoja ndiyo hasa imenifanya niamue kuchangia thread hii, mkuu nani ameleta ukabila au ujimbo? Mbona watu mnakuwa wepesi sana kuparamia viegemeo visivyokuwa na msingi? Yaani katika hiyo press release wewe unachokiona ni ukabila???? Simply kwa sababu imesemwa Makamba na Makala si wakazi wa Moshi? To you wakazi wa Moshi ni wachaga si ndiyo??? ) nao ni uhuni kama ambavyo hao vijeba wa ccm walivyofanya.

Ninachokijua mimi viongozi wengi wa upinzani ndio wavunja sheria wakuu ( Kumbe tayari ulishahukumu? Shame on you!!!!!!) ila mwakiguswa tuu uanza kulalama kama mtoto wa miaka 2.Kuweni waangalifu hususani katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani wengi wanataka hisani na huruma ya watu toka nje ya TZ.

Mwisho wote waliojihusisha na uchafuzi wa mazingira hayo wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya TZ(Hao waliopiga watu,walioingilia msafara wa wenzao kwa kuonyesha vidole 2 na hata walioona na wakakaa kimya)
Mungu ibariki Tanzania(tuachane ne ukabila - Inaonyesha wewe ndiye mkabila and very likely ndiyo silaha yako ya arguments).
Najua nitachukiwa kwa kusema ukweli ila inabidi ukweli utamkwe hata kama unauma!!!


Haya mambo ya kukonkludi ukabila na udini naona sijui ndiyo imekuwa fasheni ya JF siku hizi??????, Too low and too simplistic.
 
Haya mambo ya kukonkludi ukabila na udini naona sijui ndiyo imekuwa fasheni ya JF siku hizi??????, Too low and too simplistic.

Nilijua toka awali kuwa watu wa aina yako wata'comment' kwa staili hiyo,lakini haitaacha kutoa dosari ulizonazo wewe na wenzako kuhusu hali halisi ya kisiasa hapa TZ.Nitaendelea kusisitiza hata kwetu Sumbawanga watu kama nyinyi mpo lakini tumeweza kuwaelimisha kuachana na ukabila kwani chama hakiendeshwi kwa misingi ya ukoo,unyumba na hata uvunguni!
Iwapo hujaelewa basi wewe ni miongoni mwa waliopitia na kumaliza vyuo vikuu vya dunia lakini..........
 
CCM yakiri vijana wake kufanya vurugu Moshi Send to a friend

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro, kimetoa tamko rasmi kufuatia kundi la vijana zaidi ya 300 wa CCM kuwashambulia wananchi wakiwemo wafanyakazi wa kitengo cha damu salama katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Katika tamko lake hilo , CCM kimekiri vijana wake kufanya vurugu hizo lakini kikajitetea kuwa sio vijana wote waliohusika na vurugu hizo bali ni wachache waliokosa maadili ambao walijichomeka katika kundi la vijana safi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Moshi, Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Steven Kazidi alisema chama hicho kimechukua hatua ya kuwabaini waliofanya vurugu hizo na tayari kimepokea baadhi ya majina.

Kazidi alisema vurugu hizo zilisababishwa zaidi na ushabiki wa kisiasa lakini akasema tayari polisi wameshaanzisha uchunguzi na majina ambayo yaliyokwishatajwa yatakabidhiwa kwa vyombo vya dola.

Hata hivyo, Kazidi alikanusha vikali vijana wake hao waliokuwa wametoka kambini Kibosho kuwapiga wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC, lakini akakiri kwamba waliwashambulia wafanyakazi wa kitengo cha damu salama.

Wakati CCM kikitoa tamko hilo , Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party(TLP), Agustino Mrema amemuomba Rais Jakaya Kikwete kukemea matukio ya vurugu na vitendo vya kihuni vinavyofanywa na vijana wa CCM.

Mrema alisema anachokiona yeye ni kuwa CCM Kilimanjaro kimepagawa na zaidi ya Sh 200 millioni zilizochangwa katika harambee iliyoendeshwa na Rais Jakaya Kikwete na ndizo zinazotumika kuandaa mazingira ya vurugu.

"Rais ndiye mkuu wa amani nchini anatakiwa atupie macho Mkoa wa Kilimanjaro maana tunaandaa vijana wa aina hii bila kujua halafu tunajikuta tunakuwa na jeshi kama Janjawidi kule Sudan ambalo linaisumbua serikali,"alisema Mrema.

Mrema alisema ni vyema Rais akaonyesha msimamo wake katika tukio hilo kama mwenyekiti wa Taifa wa CCM, vinginevyo wananchi watashindwa kutofautisha kama hayo ni matendo binafsi ya mtu au ni maelekezo ya CCM.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko amekaririwa akithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha lilichochewa zaidi na ushabiki wa kisiasa.

"Ni kweli jana(juzi) walikuja watu kadhaa polisi kutoa taarifa ya kupigwa na kundi la vijana wa CCM waliokuwa wakitokea Kibosho kuelekea ofisi za CCM na inavyoonekana limechochewa na ushabiki wa kisiasa,"alisema.

Kamanda Ng'hoboko alisema polisi wameanzisha uchunguzi wa tukio hilo ikiwamo kuwabaini wale waliokuwa kiini cha vurugu hizo na kuwasaka pia waliotekeleza mashambulizi kwani kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria.

Habari zaidi zinadai kuwa tukio hilo lilitokea saa 10:30 jioni wakati vijana hao wakitembea kwa maandamano kurejea Moshi mjini wakitokea Kibosho na kuwashambulia watu waliokuwa pembezoni mwa barabara ya KCMC-Moshi.

Inadaiwa wakati wakipita katika barabara hiyo, vijana hao walikuwa wakishangilia kwa kuonyesha alama ya dole gumba lakini baadhi ya wananchi waliwajibu kwa kuonyesha alama ya V inayotumiwa na chama cha Chadema.

Habari zinadai kitendo hicho kiliwaudhi vijana hao ambao walianza kumshambulia kila mwananchi aliyekuwa pembezoni ya barabara lakini kubwa zaidi waliwashambulia wafanyakazi wa kitendo cha damu salama KCMC.

Taarifa zilizopatikana zimedai kuwa vijana hao walikua waklitokea kwenye kambi ya mafunzo maalum ya ukakamavu na kufundishwa kuwa na kauli moja na msimamo moja kuelekea uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

ChanzoP Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom