Dalili za mwanamke mjamzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili za mwanamke mjamzito

Discussion in 'JF Doctor' started by kvelia, Dec 15, 2011.

 1. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wataalamu naomba kujuzwa ni muda gani baada ya mwanamke kupata ujauzito huanza kuona mabadiliko ya nje kama vile kutema tema mate, kubagua vyakula n.k. na inawezekana dalili hizi zikaanza kutokea mapema kabla ya huo muda, na nini kifanyike kama itakuwa hivyo?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Kujua wakati una mimba


  Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama:
  • Hedhi yako itakoma/itakuwa nyepesi
  • Utasikia uchefuchefu/utatapika (ugonjwa wa asubuhi – ‘morning sickness’ – na inaweza kutokea wakati wowote wa siku pia).
  • Matiti yako yataanza kuwasha, kufura au yataanza kuwa makubwa.
  • Chuchu (ncha ya titi) na sehemu zilizokaribiana zitaanza kuwa nyeusi na zizizoweza kuvumilia.
  • Itakubidi kwenda haja ndogo mara kwa mara.
  • Utasikia uchovu
  • Kusokotwa na tumbo
  Kama umeona baadhi ya dalili hizo, unaweza kuwa na mimba. Pata jaribio/uchunguzi kipimo cha mimba ili kupata yakini! Unaweza pimwa bure katika kliniki iliyokaribu nawe au ununue kifaa vya kujipmia nyumbani kutoka duka la dawa. Daktari wako anaweza kukupima pia au atakuelekeza kwa mtaalamu kama hauna.

  Vipimo vya mimba

  Vipimo hivi huchunguza kuwepo kwa Human Cherionic Cronadotropin (HCG) kwa mkoja au damu. HCG wakati mwingine hitwa ‘Pregnancy Hormone’ na huwa kwa mwanamke tu wakati ana mimba. Kuna aina mbili ya vipimo: kipimo cha mkojo na kipimo cha damu.

  Kipimo cha Mimba cha Mkojo
  Wanawake wengi hutumia kipimo hiki ambacho pia huitwa cha nyumbani (HPT-home pregnancy test) kwa sababu ni rahisi kutumia na bahasa (rahisi kibei) kuna aina nyingi za vipimo hivi. Kwa kimoja, utakwanya mkojo wajo kwa kikombe na kukitumbukiza ‘kijiti’ huko na kwakingine utaweka ‘kijiti’ hicho kwenye viungo vya mkojo. Njia iliyobora ni itakayokuonyesha kiwango cha HCG, hivyo tafuta moja katika kiwango cha hCG kutoka 15 hadi 30. Utasaidiwa na mhudumu wako dukani la dawa au kliniki.

  Vifaa hivi hufaa kwa asilimia 97-99 kuyakirisha uwepo wa mimba vinapotumiwa ipasavyo. Hivyo kufuata maagizo ni muhimu. Pia angatia wakati wa kuharibika wa kifaa kwani kifaa kilichoharibika hakitakupatia matokeo unayotarajia.

  Kama utapata matokeo yasiyofaa/yasiyo hakika
  Kama utajipima/utapimwa bado kidogo*, unaweza kuona kwamba hauna mimba ili hali unayo. Aina nyingi ya vipimo vya nyumbani hukushauri ujipime baada ya siku kadha bila kujali matokeo uliyopata awali. Kama unaendelea kupata matokeo yasiyofaa nab ado unashuku una mimba, ongea na daktari/mkaguzi afya waka.

  Kama utapata matokeo yafaayo/yahakika
  Kama utapata matokeo ya hakika, fanya miadi na mkaguzi afya wako punde tu. Mkaguzi wa afya yako atayakinisha kama una mimba kupitia kipimo cha damu na ukaguzi mwingine (pelvic exam) na atakwambia chaguzi uliza nazo.

  Kipimo cha Damu
  Kama wataka kipimo cha damu badala ya kite cha nuymbani, fanya miadi na mkaguzi afya wako/dakatari wako.   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kujua lini inategemea na ukali wa manii za mwanaume.....zangu in two hours unakuwa ushajua!...na baada ya masaa sita unaanza kutema mate
   
 4. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shukrani sana mkuu
   
 5. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kusokotwa na tumbo hutokea wakati gani wa umri wa ujauzito. Maana mke wangu tumbo linamsokota kwelikweli, Je, ni dalili ya ujauzito maana kwa mahesabu yetu kama ni ujauzito basi ni wa wiki mbili. Na kama ni mojawapo ya dalili je, kuna dawa ya kusokotwa kwa tumbo au huwa linatulia lenyewe baada ya muda fulani?

  Msaada tafadhali wenye uelewa na mambo haya.
   
 6. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160

  NAONA UNAJIFAGILIA MKUU
  :lol:
   
Loading...