Habari wana MMU?
Kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya ndoa na mapenzi inaelezwa kwamba wapenzi wanaoachana huwa hawana sababu za msingi, hii inatokana na ukweli kwamba wanaoachana hawafahamu kiini kilichowatenganisha katika makubaliano muhimu na ya kwanza kabisa hata kufikia hatua ya kupeana utu wao.
Daalili zifuatazo zinaashiria huenda penzi linaanza kunyauka na kufikia kufa kabisa:
1 : Ikiwa mmeoana na baadaye mkaanza kuonana ni watu msiohitajiana sana katika maisha.
2 : Mkiwa hamsameheani na kusahau mnapokoseana.
3 : Msipokubali kuwekeana mipaka ya kiutawala.
4 : Msipozungumzia vikwazo vya maisha.
5 : Msipokuwa na mipango ya pamoja na uwazi wa matumizi ya pesa.
6 : Mkiacha kujaliana na kupeana haki katika tendo la ndoa.
7 : Mkibeba fikra binafsi kwa kila mtu kutaka mafanikio yake.
8 : Mkiwa watu wa kutoa siri zenu nje.
9 : Msipokuwa wawazi katika kuzungumzia upungufu wa kibinadamu mlionao na kusaidiana.
10 : Mkiendekeza nguvu katika kutwaa madaraka ndani ya familia.
11 : Mkiwa watu msioheshimiana mbele za watu na kupenda zaidi kusema kuliko kusikiliza.
12 : Msipokuwa tayari kukubali kosa na kujirekebisha.
13 : Msipokuwa watu wa kuitafuta furaha pale inapokosekana.
14 : Msipozingatia kuombana msamaha bila kujali nani mwenye kosa.
15: Msipokuwa tayari kukumbushana wajibu na mwenendo wenu
16: Kuacha kumcha mola
Namba tano (5) haiwahusu wale .
Ukiwa vizuri hapo kwenye kuzingatia hayo na kutafuta majibu, aaaaaah! Waishi vyema wewe!
Kila lakheri katika kuishi vizuri.
Chanzo: http://richmanyota.blogspot.com/2010/08/dalili- za-mapenzi-kunyauka.html