Dalili za mapenzi kunyauka 1,2,3...

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
1260424051_black_couple1.jpg


Kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya ndoa na mapenzi inaelezwa kwamba wapenzi wanaoachana huwa hawana sababu za msingi, hii inatokana na ukweli kwamba wanaoachana hawafahamu kiini kilichowatenganisha katika makubaliano muhimu na ya kwanza kabisa ulimwengu wa watu kufikia hatua ya kupeana utu wao.

Inasemwa hivyo kwa sababu ukilinganisha matatizo yanayotenganisha watu hayabebi hoja zinazokubalika na wapenzi wote. Kwa mfano kama wapenzi watasema wameachana kwa sababu wamefumaniana na wakadhani hiyo ni sababu wanakuwa wanaudanganya zaidi umma kwa maana kuna wanaofumaniana, wanaodhalilishana, wanaotukanana, wasioheshimiana kabisa, lakini bado wanadumu katika ndoa zao bila kuachana.

Kwa ulinganifu huo, wachunguzi wa mambo ya ndoa wanasema, kuachana si zao linaloota na kukua kwa siku moja, bali ni migogoro isiyoshughulikiwa kwa muda mrefu ambayo huwaachanisha wanandoa taratibu bila wao kujua.

Kwa maana hiyo wanaoachana au watakaoachana wanatakiwa kufahamu kuwa safari yao ya talaka haianzi na kumalizika kwa siku moja, isipokuwa hufikia katika hitimisho baada ya kuwepo katika mwendo kwa muda mrefu, ambapo dalili zake huwa hizi zifuatazo:

1 : Ikiwa mmeoana na baadaye mkaanza kuonana ni watu msiohitajiana sana katika maisha
. (mapenzi kuchuja). Kila mtu anafahamu kuwa wakati wa uchumba mapenzi huwa moto moto lakini baada ya kuoana hujitokeza hali ya kuanza kuzoea. Hii inatokana na ukaribu ambao mwanzo haukuwepo au kusitishwa kwa machombezo yaliyokuwa yakiboresha uhusiano. Kwa mfano wapenzi wengi wanapokuwa kwenye uchumba hufanyiana mambo mengi yakiwemo ya kutumiana zawadi na kadi au kutoka pamoja kwa matembezi, lakini wakioana hujikuta hawafanyiani hayo, jambo ambalo huathiri mapenzi yao.

Uchunguzi unaonyesha kuwa wapenzi walio kwenye uchumba wanapokuwa pamoja hutumia muda mwingi sana kuongea kwa simu, kutumiana meseji, kuzungumza tofauti na mume na mke. Ukitaka kuthibitisha keti barabarani ukiona mwanaume na mwanamke wamo ndani ya gari hawaishi kucheka na kuzungumza wafuatilie utakuta mwisho wa safari yao wanaagana kila mmoja anakwenda kwake (ina maana si mume na mke hao). Ni nadra sana kuwakuta wanaume wakiwa pamoja na familia zao wakifurahi, jambo ambalo hupunguza upendo na kuleta mazoea na hisia za kutohitajiana sana. Hili halifai likiwepo ni ishara kuwa mapenzi yanakaribia kunyauka.

2 : Mkiwa hamsameheani na kusahau mnapokoseana.
Si watu wengi ambao wako tayari kusamehe na kusahau makosa. Wapenzi wa dunia ya leo wakisema nimekusamehe haina maana wamefuta kosa bali hiliweka kando na kulikumbushia wakati mwingine. ‘Hili ni kosa la tatu tarehe fulani ulinifanyia hivi, wiki iliyopita na jana kulinijibu hivi hivi sasa leo siwezi kukuvumilia”

Kauli kama hizi hutoka kwenye vivywa vya watu ambao hawako tayari kusamehe, kosa la mwaka juzi litakumbushwa tena na tena na kuzidi kuchochea ugomvi hata uliokuwa mdogo na kuoneka mkubwa kwa sababu tu umehusishwa na makosa yaliyopita. Inashauriwa kuwa uhai wa mapenzi lazima uambatana na kusameheana kama wanadamu na kusahau makosa. Hili lisipofanyika ni rahisi kuua penzi na kuwafanya watu kuachana. Ni vema kila mmoja wetu akajichunguza tabia yake na kuacha kukumbusha makosa yaliyopita.

3 : Msipokubali kuwekeana mipaka ya kiutawala.
Kuna suala linatambulishwa sana siku hizi na wanaharakati, linaitwa usawa wa kijinsia, jambo hili limekuwa likichangia sana migogoro ya ndoa hasa baada ya kutumiwa vibaya na wahusika. Hakuna ubishi mila za kiafrika zinaongozwa na mfumo dume, kuubadili mfumo huu kwa haraka kumekuwa kukiharibu uhusiano mwingi wa kimapenzi kutokana na ukweli kwamba ni wanaume wachache sana ambo wako tayari kuishi na wanawake wanaovutana nao kimamlaka.

Hivyo ili kunusuru hili lisiwe kikwazo katika mapenzi tunashauri kila mwanandoa kuheshimu mipaka yake na kujali zaidi utu na si usawa kama inavyotambulishwa (haya ni mawazo yangu). Watu wanaojali utu katika familia watakuwa tayari kuwapa heshima wanaoishi nao kwa kusikiliza mawazo yao na kutokutumia nguvu kuwakandamiza wengine. Ni vema mwanamke akachunguza nafasi yake kwa mumewe na mume naye akamuheshimu mke kwa utu wake.
4 : Msipozungumzia vikwazo vya maisha.
Matarajio ya watu wengi wanapoingia katika uhusiano wa kimapenzi huwa ni kupata faraja, ni wachache kati yao hufikiria kukutana na vikwazo vya kimaisha. Tafiti zinaonyesha kuwa wakati mtu anapotafuta mpenzi huamini toka moyoni kuwa akiwa na waridi wake matatizo ya upweke, kukosa msaada wa hili na lile yatakwisha lakini baadaye anakuja kubaini kuwa aliyokusudia kuyapata hayapati tena na hivyo kujuta kwa kauli kama hizi. “Kama ningejua kama mwanaume mwenyewe yuko hivi nisingekubali kuolewa.”

Kauli kama hizi mara nyingi hutokea kwa watu ambao hawazungumzii matatizo na vikwazo wanavyokutana navyo katika mapenzi na kuviondoa. Kama mpenzi wako ana matatizo unasubiri nini kuyatafutia ufumbuzi au kama maisha hayaendi sawa ukimya wa nini kwa mwenza wako, kaeni chini muambizane kuwa mnaupungufu wa fedha na dhiki kadhaa wa kadhaa, ili kama kutatokea kukosa mahitaji muhimu liwe ni jambo linaloeleweka na wote kuwa linatokana na kipato kushuka. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi wanapokukwama kiuchumi hupunguza matumizi kimya kimya jambo ambalo huwafanya wanawake wengi kubaki wakitumikia zana potofu kuwa huenda wananyimwa baada ya kuwepo kwa nyumba ndogo.

5 : Msipokuwa na mipango ya pamoja na uwazi wa matumizi ya pesa.
Nina ushahidi wa kutosha juu ya kuwepo kwa wapenzi hasa wenye kipato kutokuwa wawazi katika mipango yao ya kimaisha na matumizi yao ya pesa. Natambua baada ya kufanya uchunguzi wangu kuwa pesa za baadhi ya wanawake huwa hazina matumizi ya wazi, badala yake wanaume hubanwa kwa kisingizio kuwa wao ndiyo wana wajibu wa kutunza familia.

Hali hii imekuwa ikileta migogoro mingi sana kwenye familia na kushusha upendo kwa vile upande unaohudumia familia hapa haijalishi mume au mke huwa unajikuta ukikereka kwa kukosa msaada wa upande wa pili na hivyo kuondoa mapenzi ya kweli. Kama hilo halitoshi vijana wengi wa kiume siku hizi wamejikuta wakiahirisha mapenzi yao kwa wasichana baada ya kukosa ushirikiano wa kimapato na matumizi yao.

“Ninashida ya kuonana na wewe mpenzi wangu, vipi nikufuate kazini?” Jibu linakuwa “Hapana niko bize sana leo.” Inawezekana kabisa mtu akawa hayuko bize lakini kwa sababu anaogopa kukamuliwa kipato na yeye mambo yake hayako sawa anaamua kukacha ahadi. Lakini ukiwepo ushirikiano wa kimatumizi husaidia kudumisha mapenzi.

Inashauriwa kwamba kama wapenzi wote wana kazi na wanapokea mishahara ni vema vipato vyao vyote vikatumika katika kutunza na kuendeleza familia. Tabia ya mwanamke kumtegemea mwanamume kimatumizi huku yeye akitumia pesa zake kwa manunuzi ya vipodozi na nguo au kufanyia mambo yake kwa siri haijengi badala yake inanyausha mapenzi kama siyo kuyaua kabisa.

6 : Mkiacha kujaliana na kupeana haki katika tendo la ndoa.
Tendo la ndoa ni muhimu kwa wanandoa kwa vile linahusika na hisia za mwili. Matatizo mengi ya usaliti kwa mujibu wa uchunguzi, yanatokana na wapenzi kutotoshelezana wakati wa tendo la ndoa. Kwa kutokutambua madhara au kwa uzembe, wapenzi wengi wamekuwa wakiacha kutimiziana tendo hilo bila kuwepo kwa sababu za msingi. “Mimi nimechoka siwezi kufanya mapenzi.”

1tr81v.jpg

- To Be Continued...​
 
nakubaliana na ww yote ulosema ni mambo yanayotendeka sana kwenye ndoa nimejifunza jambo jipya na ninakubaliana nalo kwamba sababu zitolewazo na wanaoachana sizo sababu alisi
 
Ni kweli kabisa uliyosema, na kwa kuongezea ni kuwa watu wengi katika mapenzi hasa wanawake (Sorry I'm not biased) inapotokea issue ya kuwasiliana wao wanaona/fikiri kuwa mwanaume ndiyo mwenye jukumu la kuwasiliana naye kama kumtakia hali, salam hata kupiga simu.

Wanasahau kuwa mawasiliano kwa wapenzi ni kwa pande zote mbili na siyo upande mmoja (Communication should be in reciprocity and not one sided).

Thanks
 
Back
Top Bottom