Dalili za malaria

Kasuku Mdogo

Member
Jun 2, 2016
14
23
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea. Vimelea vya malaria vinavyoitwa Plasmodia huingia katika mfumo wa damu kupitia kuumwa na mbu jike aitwaye kwa kitaalamu kama ‘Anopheles’.

Dalili zake ni pamoja na
Kupatwa na homa
Kuhisi baridi
Kutokwa na jasho
Mavumivu ya kichwa na mwili
Kichefuchefu na kutapika

Dalili hizo zinaweza kuonekana ndani ya masaa 48 mpaka 72, kutegemea ania ya vimelea na muda ambao mtu amekuwa na ugonjwa.

Ugonjwa wa malaria endapo hautibiwa unaweza kusababisha upungufu wa chembe chembe za damu na hivyo kuhatarisha uhai. Kabla ya dalili hizo kuwa mbaya hata zaidi, tafuta matibabu haraka, hasa inapohusu watoto na akina mama wajawazito.
 
Na pia ndio ugomjwa unaochukuliwa kuwa wa kawaida sana huwezi amini kuna watu wanaogopa kuugua mafua kuliko malaria, alafu pia ndio ugonjwa unao ongoza kwa kusababisha vifo vya watu hususani huku afrika kusini mwa jangwa la sahara..
Kingine ndio ugonjwa wenye dawa nyingi za kuutibu na ukaondoka kabisa kuliko ugonjwa mwingine wowote.

Mkuu kama unasumbuliwa na malaria hata usiangaike kukodi boda boda etii unaenda hospitali dawa unayo hapo hapo nyumbani kwako.
 
Funguka hiyo dawa tuliyonayo majumbani mkuu.
 
Back
Top Bottom