Dalili ya Serikali Inayotaka Kufilisika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili ya Serikali Inayotaka Kufilisika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Losambo, Dec 1, 2011.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika siku za hivi karibuni kumeibuka shutma kubwa ya serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete kufilisika, kigezo kikubwa kilichotumika na baadhi ya watu wanaohalalisha kufilisika huko ni serikali;

  1. Kuchelewesha malipo wa watumishi wake hasa wale ambao ni lazima fedha zao zianzie makao ya hazina D'Salaaam. Juu ya kuchelewesha mishahara ya watumishi hili ni kweli kwa maana karibu asilimia kubwa bado hawajapata ukitoa TISS, JWTZ na wale wa Halmashauri ambao mishahara yao haianzii Hazina Kuu D'Salaam kama mifumo ya mingine inayotumiwa na wizara mbali mbali kama afya, elimu, mambo ya ndani n.k Mpaka sasa baadhi ya wizara imeshapelekewa taarifa kwa watumishi wake kuwa wavumilivu wakati tatizo lililoelezwa ni mtandao hazina likipatiwa ufumbuzi.
  2. Kushindwa kwa serikali kupeleka migao ya fedha kwa idara zake nyingi karibu miezi miwili bila sababu ya misingi nako kunaelezwa ni ukata ulioikumba serikali. Tatizo hili linadaiwa kuzidishwa na miaka 50 ya uhuru ambayo haijulikani kama kweli kipindi bajeti inapita nayo ilikuwemo kwenye bajeti!!! Fedha nyingi zinadaiwa kukimbizwa huko na kuacha huduma nyingine serikalini hoi.
  3. Kuongezeka kwa deni la taifa kwa maana ya serikali kukimbilia kukopa kama mbadala wa chanzo cha fedha ili mradi inakopesheka.
  4. Kushindwa kulipa madeni ya ndani na nje kwa muda mrefu. Mfano serikali kushindwa kulipa madeni ya wazabuni mbali mbali kama wakandarasi, madai ya muda mrefu ya watumishi hasa walimu, askari, waaguzi na madaktari n.k
  5. Kuchelewesha malipo bila sababu za msingi.
  Yote kwa yote, naomba kuuliza kwa wanaJF wenzangu je sababu hizo ambazo zimetajwa tajwa hapo mtandaaoni sana je zinatosha kusema serikali yetu ipo njiani kufilisika?

  Na ni zipi hasa dalili za serikali inayotaka kufilisika au iliyofilisika? Maana kauli ya Mh. Zitto Kabwe akiwa bungeni alitoa kauli kuwa serikali imefilisika kauli iliyokanushwa vikali na waziri wa fedha Mh. Mkullo lakini hali inaonekana ni mbaya kiasi fulani serikali.

  Naomba mnikwamue na hata wengine wasioelewa tuelewe mtu hasa anaposema serikali imefilisika anakuwa anatumia vigezo gani?

  Nawasilisha.
   
Loading...