Shida ni kwamba waliokasimiwa jukumu la vehicle inspection Wana agenda nyingine...... Na Sina uhakika na weledi wao kwa kazi hiyo, kama wamepitia mafunzo yahusuyo ujuvi wa gari na inavyofanya kazi na yapi makosa ya kuonya na yakuadhibu papo kwa papo??!!!
Nadhani Kuna haja ya kuzalisha Vehicle inspectors wakutosha Ili wawe wengi barabarani badala ya hawa watumishi wanaoamka kwenda kukusanya hela za vikoba au mchezo.
Ukitoka masaki to gongo lamboto, Jamaa wananyoosha mkono tu gari Inapita inasimama mbali kule wanaendelea na stori zao konda anashuka na 2000 chap anaenda kukabidhi kwa aloyenyoosha mkono anarudi mnaondoka..... (2000 msasani shule, 2000 moroko, 2000 magomeni hospital, 2000 kigogo round Abt, 2000 Msimbazi center na kamera juu, 2000 Daraja la Veta, 2000 vingunguti/jet, 2000 u/ndge au banana, 2000 goms kwenyewe.
Kama ilivyo ngumu ngamia kupenya tundu la sindano ni ngumu pia kupita walipo usipingwe mkono ........ Kwa mantiki hiyo unadhani madaladala mabovu yataisha
Nadhani jambo la msingi ni mafunzo sahihi lakini pia uelewa wa taratibu na Sheria za usalama barabarani kwa wasimamizi, sisi wananchi tunaenda na msimamo wa serikali, wakisimamia ipasavyo tutageuka ila wakiendekeza upatu tutacheza nao lakini maisha ya watu yanaendelea kuwa hatarini hususani abiria..
Wazo langu, nashauri wawe na cheki point Maalum za kukaa na pafungwe kamera zinazoungwa na na mabango ya matangazo kwa eneo Hilo mtu anayepita anaweza kushuhudia wanachofanywa .... Wakipokea tuwe tunaona, gari ikisimamishwa tuwe tunaona wanachokagua na endapo wanaingia ndani kuona hali ya daladala, huenda ikapunguza ubovu wa vyombo na Kisha upatu kuisha.