Daladala Morogoro zimegoma kupakia abiria

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
42,451
Reaction score
50,183
Wandungu, nimeingia mji kasoro bahari leo, kinachoshangaza hakuna usafiri wa daladala kama ilivyozoeleka, usafiri pekee ni bodaboda, kilikuu na bajaji, nimeuliza watu kadhaa wanasema wenye daladala wamegoma.

Je, nini kimeshindikana kuzungumzika mpaka kufikia adha hii!?

-----
Kwa zaidi ya saa nane wakazi wa mkoa wa Morogoro wamekosa huduma ya usafiri wa daladala kutokana na mgomo wa madereva kwa madai ya bajaji kupakia abiria

Kwa zaidi ya saa nane wakazi wa mkoa wa Morogoro wamekosa huduma ya usafiri wa daladala kutokana na mgomo wa madereva kwa madai ya bajaji kupakia abiria kinyume na utaratibu waliowekewa hivyo kuwaathiri kibishara.

Madereva wa daladala wanalalamikia walichodai wingi wa bajaji kunakobabisha wao kukosa abiria na kwamba wameamua kurudisha magari yao kwa wamiliki kutokana na kufanya kazi bila maslahi, ingawa baadhi ya mabasi yameonekana kubeba abiria na kuwashusha katika standi hiyo ya daladala.

Kufuatia mgomo huo wa madereva, mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk,Kebwe Steven Kebwe ameagiza mkuu wa wilaya kutoa elimu kwa kwa madereva wa bajaji ili wafanye kazi kwa mujibu wa leseni zao na wanaokiuka kuchukuliwa hatua stahiki .
 
upo morogoro gani mkuu ?

hapa mjini mbona daladala za kumwaga mkuu
labda kama uko matombo
 
Kwani bajaji hazina leseni za kupakia abiria?
Wauze mabasi wanunue bajaji.
 
Kodi tunalipa sisi tulio kwenye orodha ya walipakodi. Hao Bajaj wanapiga pesa ndefu, lakini hakuna kodi yoyote. Daladalka kodi kibao, teksi kodi kibao, halafu wanaachwa hao wenye bajaj watambe tu. Hakuna usawa hapo. Malalamiko ya daladala ni sahihi.
 
Hawa madreva wasenge Sana.. Kwahyo wao peke yao ndio wanataka fursa ila wengne wastahili..
 
Hata sisi bajaji tunalipia
Sumatra, bima,ushuru wa parking, stika ya manispaa, posho kwa bosi n.k je kwani sisi sio watanzania kama nyie?
Hatuna majukumu kama nyie?
Acheni wivu, uvivu,husuda na roho za chuki kwa wenzio.
 
Jengeni mazingira ya kuwashawishi abiria kupenda daladala kama vile wanavyopenda bajaji, sioni sababu kwanini msishindane kwa ubunifu.

Imagine daladala zinajaza abiria kupita kiasi hadi hewa inakosekana ndani ya bus, kwanini mtu asipande bajaji ambayo ni spacious na hewa ipo ya kutosha
 
Hata sisi bajaji tunalipia
Sumatra, bima,ushuru wa parking, stika ya manispaa, posho kwa bosi n.k je kwani sisi sio watanzania kama nyie?
Hatuna majukumu kama nyie?
Acheni wivu, uvivu,husuda na roho za chuki kwa wenzio.

Great!!

Hoja waliyotoa waliogoma ni ya kitoto kabisa, haina tofauti na wanasiasa wanaosema "watu wangu" mteja ana uhuru wa kuchagua huduma anayotaka, hivi leo hii waarabu wagome kuzalisha mafuta ati kwasababu wameona kuna teknolojia ya magari kutumia umeme!!
 
Hawa madreva wasenge Sana.. Kwahyo wao peke yao ndio wanataka fursa ila wengne wastahili..

Yaelekea akili zao zinashida, hawatembei kwenda kujifunza kwenye miji mingine, they can not think outside the box, sasa ndiyo najifunza kwanini watu wa mji huo ni wabishi sana, siku moja nimeshuhudia ubishi mkubwa pale stand kuu wakidai ile round about karibu na stand ndiyo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na kati
 
njoeni dar nyinyi
IMG-20181015-WA0018.jpeg
 
Great!!

Hoja waliyotoa waliogoma ni ya kitoto kabisa, haina tofauti na wanasiasa wanaosema "watu wangu" mteja ana uhuru wa kuchagua huduma anayotaka, hivi leo hii waarabu wagome kuzalisha mafuta ati kwasababu wameona kuna teknolojia ya magari kutumia umeme!!
Watu wanaenda kufuatana na mabadiliko ya kimazingira ama teknolojia, sio lazima MTU akae stand masaa kibao kusubiria gari ijae ilihali anahitajika haraka sehemu husika.
Bajaji zimekuwepo kwa sababu ya uhitaji kama daladala zilivyokuwa zinahitajika hapo kabla. Ila serikali nayo ndio inayochangia hii migomo coz kama biashara imeshuka kwa nini wasiwapunguzie mapato?
 
Back
Top Bottom