Daladala katikati ya Jiji mwisho Mei 2

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,852
Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi(DART) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar-es-salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Mabrouk amesema wamiliki wa daladala zinazofanya safari zake katika ya Jiji walishalipwa fidia ya kubadili route.

"Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu December mwaka jana, hakuna anaedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,"alisema Mabrouk.

MY TAKE:
Jiandaeni kusikia wengine wanalalamika hawajalipwa na wataamua kupinga agizo hili hata kwa kwenda mahakani.

=========

MPANGILIO WA RATIBA ZA MABASI YA MWENDO KASI KESHO.

MABASI YATAANZA SAFARI SAA KUMI NA MBILI KASORO ROBO KUTOKEA DEPOT YA JANGWANI KWA MPANGILIO UFUATAO.

1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.

2. RUTI YA KIMARA - KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO - KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.

5. RUTI YA UBUNGO - MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

6. RUTI YA MOROCCO - KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)

3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

JUMLA.NI MABASI HAMSINI (50)
 
Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa kuondoka ifikapo Mei 2.

Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.

“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk.

Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.
 
Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi(DART) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar-es-salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Mabrouk amesema wamiliki wa daladala zinazofanya safari zake katika ya Jiji walishalipwa fidia ya kubadili route.

"Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu December mwaka jana, hakuna anaedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,"alisema Mabrouk.

Chanzo:Mwananchi online

Jiandaeni kusikia wengine wanalalamika hawajalipwa na wataamua kupinga agizo hili hata kwa kwenda mahakani.

Heading inasema May 2, ndani habari ni May 10.
 
Hii Habari Haina Supu. Katikati Ya Jiji Mwanzo Na Mwisho Wapi? Halafu Kuna Hii Ruti Ya Ubungo Mnazi Mmoja. Ni Jipu. Na Hii Itakumbwa Na Operesheni Hii?
 
Hayo magari ya mwendo kasi yanapita njia zote..? Gomz..?? Mbagala.?? Mbona njia za mwendo kasi haziko maeneo hayo...au? ??
 
Hayo magari ya mwendo kasi yanapita njia zote..? Gomz..?? Mbagala.?? Mbona njia za mwendo kasi haziko maeneo hayo...au? ??
Nadhani ni zile mkoa ambazo tayari miundombinu yake imekamilika. Kimara-Ferry/k.koo na Morocco-Ferry/k.koo.
Nilisikia wakisema kuna feeder busses, sijui hizo zitaoperate vipi. Ngoja tuone.
 
Huu mradi wasipokuwa makini utaleta balaa kubwa, hawa Dart ni kweli wana capacity ya ku-handle wakazi kuanzia Kiluvya mpaka Magomeni?
 
kwa maana22 kwamba hayo magari ya mwendo kasi peke yake ndio yatamudu abiria wote wanaoingia mjini?
nashangaa ukizingatia ubungo basi za mkoa zinaondoka saa12. watu huwa wanaanza kuingia saa10. watakuwa wanapqnda basi zipi
 
Back
Top Bottom